Mungu Yuko wapi?

Sijasema wanatafuta majibu ya mungu kuwepo, nimesema wanatafuta majibu ya maswali magumu ya maisha na wanayapata. Throughout time wazungu wamevumbua vitu vingi ambavyo sisi tulikuwa hatuna majibu na kusema god did it
Bado hawajapata majibu kuhusu Mungu?
 
Kusali unaweza Sali hata nyumbani, so hio sio point,
Kwani aliyekuambia kuwa ukiamini MUNGU lazima usali ni nani? Na ndo maana unakaza mishipa kusema ukishasema kuna MUNGU basi wewe ni mjinga fulani usiyewekeza kwenye sayansi na waliofanikiwa ni wasioamini uwepo wa MUNGU.
 
Dunia inazunguka jua ipo kitambo kwenye maandiko
Okay. Explain to me mungu kuumba vegetation kabla ya jua, au walioandika walikuwa hawajui photosynthesis, na jua na mwezi ziliumbwa siku ya tatu. Hizo siku mbili zimepitaje?
 
Bado hawajapata majibu kuhusu Mungu?
Wamepata kwamba biblia ni story za kutunga na za uwongo. So mungu wa biblia hawezi kuexist na ndo mungu unayemuamini, ambae hapendi ngono, hapendi watu watafiti ukweli kuhusu vitabu vya uwongo etc
 
Kwani aliyekuambia kuwa ukiamini MUNGU lazima usali ni nani? Na ndo maana unakaza mishipa kusema ukishasema kuna MUNGU basi wewe ni mjinga fulani usiyewekeza kwenye sayansi na waliofanikiwa ni wasioamini uwepo wa MUNGU.
So wewe unaamini mungu yupi mwenye sheria zipi na anayetaka Nini? Ni jibu bila kutumia dini yoyote
 
Mkuu
Kwanini watu huwa mnalazimisha majibu mepesi?

Hautoi nafasi ya hata kidogo kuwa si lazima mtu awepo aliyefanya hivo?
 
Lakini kuna mambo mengi wanasayansi wanavumbua miaka hii hlf wanakuta kitaambo yashaandikwa kwenye hivi vitabu, tena ktk wkt ambao hakuna teknolojia, vifaa wala wasomi wakubwa.
Ujue kuna watu psychology zenu bhana huwa zinahitaji umakini ili kuendana nazo. Mpo tyari kutumia kila hila ili mjinasibu na muoneshe kuwa kilichoandikwa kwenu ni sahihi.
Inakusaidia nini hiyo mkuu?
Kwanza kabisa naomba huo mstari wa quran ili tuthibitishe dai lako.
Bila kuuona huo mstari, ntasema wewe ni muongo.

Unauhakika kabsa hzo mbegu za kiume zinazalishwa kwenye uti wa mgongo na si kama ulivyofundishwa sekondari?

Wao wanasayansi wanakiri "elimu" hii hawezi kua nayo mtu wa kawaida ambaye hakusoma kbs, hivyo kuna namna ya ukweli wa maneno hayo kutoka seheme yenye nguvu "inayoamnika".
Naomba niweke kituo kwanza.
Kwahiyo wewe unamuamini mtu ambae hakuwa anajua kusoma na kuandika badala yake unaacha Science hii tuionayo leo kwa shuhuda na proof tele?
 
Mungu yupo?

Au unaamini yupo?
 
Mkuu
Kwanini watu huwa mnalazimisha majibu mepesi?

Hautoi nafasi ya hata kidogo kuwa si lazima mtu awepo aliyefanya hivo?
Si lazima awepo mtu aliyefanya ndiyo ila kuna nguvu inayowezesha hayo, Haya wewe nikuulize tuu swali mimi naweza kutumia maandiko ya vitabu vya dini kuthibitisha uwepo wa Mungu haya na wewe unathibitisha na nini kwamba hayupo?
 
Hii dunia hata kwa akili za kawaida tu, ina chanzo. Na hiko chanzo ndio tunakiita MUNGU.

Shida kubwa hapa ni dini. Haswa ukristu na Uislam. Ni sheeda.
Kwanini hufikirii kutumia akili zisizo za kawaida?

Kama Dunia ina chanzo, huyo Mungu yeye atakuwa katoka wapi
 
Nakataa unaponiambia kuwa mimi sisemi hakuna Mungu kwa sababu ya hiyo contradiction kwa sababu nasema hakuna Mungu kwa sababu ya hiyo contradiction.

Bila ya contradiction nisingejua Mungu hayupo.

1. Hujaondoa contradiction.
2. Hujathibitisha Mungu yupo
3. 1 na 2 hapo juu ni kwa sababu Mungu hayupo.
4. Kama unabishia 3, kamilisha 1 na 2 hapo juu.
 
Si lazima awepo mtu aliyefanya ndiyo ila kuna nguvu inayowezesha hayo, Haya wewe nikuulize tuu swali mimi naweza kutumia maandiko ya vitabu vya dini kuthibitisha uwepo wa Mungu haya na wewe unathibitisha na nini kwamba hayupo?
Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Maandishi hayo ya hadithi si vitu halisi mkuu, ni hadithi tu.
Hadithi za kutungwa na watu haziwezi kutumiwa kama uthibitisho.
 
Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo.

Maandishi hayo ya hadithi si vitu halisi mkuu, ni hadithi tu.
Hadithi za kutungwa na watu haziwezi kutumiwa kama uthibitisho.
You mean kwamba wakina Isaac Newton tumewasoma kwenye maandiko hayohayo na ndo walibuni vitu hadi sasa tunatumia pia ni uwongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…