Mungu Yuko wapi?

Mungu Yuko wapi?

Hivi huu msimamo wa kwamba "hakuna Mungu" umejengwa kwenye msingi gani? Yani kipi kinabeba huu msimamo na kufanya kuwa ni uhakika kuwa Munguni hayupo tu na si vinginevyo?
Nani kasema Mungu yupo au hayupo. Tumesema Biblia na Quran ni story za kutunga.
 
Nitakujibu kulingana na kitabu cha mwanzo
Mwanzo 1-2:3
Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Mungu ni roho fulani ambayo ilitokea majini kulingana na andiko ilo Wanakuambia Maji yalikuwepo kabla ya Mungu
Alicho kifanya roho hiyo akatenganisha Maji Yale katikati kukapatikana anga
Nipe evidence sio vitabu vya hadithi.
 
Hujasoma kitabu vizuri rudi kasome, akili za wengi zimeaminishwa na dunia na ulimwengu kuwa MUUMBA ndo anaua watu.

KERUBI aliyekuwa malaika wa sifa kabla ya kuasi ukisoma Isaya 14:13-15 utakuta kwanini alitupwa chini.
Mi sijasema anaua watu...Ila kwenye story za Bible kaua watu kuliko shetani
 
Mi sijasema anaua watu...Ila kwenye story za Bible kaua watu kuliko shetani

Kwenye KITABU imeandikwa ivyo na sio bahati mbaya sababu hata waandishi walikuwa chini ya mvamizi hivyo vingne vilipachikwa lakini hakuna mzazi anazaa mtoto alafu anataka afe never.
 
JamiiForums hapa pia mtasema nachochea ugomvi wakati ni mjadala tu au mtasema maanisha uzi,

hakuna MUNGU nje ya DINI, ukiondoa DINI na madhehebu hakuna unapomuona MUNGU
Na hivyo ndio nmemaanisha

Ingekuwa hakuna MUUMBA nje ya DINI kusingekuwa na tofauti ya kiimani. Lakni MUUMBA ni mmoja na yeye haangalii dini wala dhehebu bali kutenda kwa haki.
 
Kwenye KITABU imeandikwa ivyo na sio bahati mbaya sababu hata waandishi walikuwa chini ya mvamizi hivyo vingne vilipachikwa lakini hakuna mzazi anazaa mtoto alafu anataka afe never.
So kamuumba shetani ili atutese...na ukisema alikuwa malaika...Mungu ni muweza na mjua yote it means alijua atamuasi na angeweza kumzuia. Lakini hajataka...ameamua kumuachia atese binadamu baadae amuunguze yeye na binadamu wengi(vitabu vinasema watu wengi wataenda motoni isipokuwa watu 144k duniani).Afu bado unaniambia huyu ni sterling wa movie. Aliyefurika dunia nzima kuuwa panzi watoto wazee ili familia moja ya mlevi na watoto wanaobaka baba zao waishi.
 
Ingekuwa hakuna MUUMBA nje ya DINI kusingekuwa na tofauti ya kiimani. Lakni MUUMBA ni mmoja na yeye haangalii dini wala dhehebu bali kutenda kwa haki.
We unajuaje Ni mmoja...mbona wengine Wana waumba wengi ..we dini yako ndo inasema yupo mmoja. So bado hujaseparate dini na Imani.
 
So kamuumba shetani ili atutese...na ukisema alikuwa malaika...Mungu ni muweza na mjua yote it means alijua atamuasi na angeweza kumzuia. Lakini hajataka...ameamua kumuachia atese binadamu baadae amuunguze yeye na binadamu wengi(vitabu vinasema watu wengi wataenda motoni isipokuwa watu 144k duniani).Afu bado unaniambia huyu ni sterling wa movie. Aliyefurika dunia nzima kuuwa panzi watoto wazee ili familia moja ya mlevi na watoto wanaobaka baba zao waishi.

Umeaminishwa kwamba atapeleka motoni watu wote kasoro 144k lakini ungejua falme na malmlaka za giza walitaka kila mtu hahukumiwe ili MUUMBA asibaki na chochote na lakini kwa uheri alisema katika
Isaya 43:25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.”

Hivyo wengi hudhani kuna kiama mara mwisho wa dunia kwa nadharia walizofundishwa wasijue mwisho ulishafika na MUUMBA anawakomboa watu wake kwa kila anayekubali msamaha wa bure.
 
We unajuaje Ni mmoja...mbona wengine Wana waumba wengi ..we dini yako ndo inasema yupo mmoja. So bado hujaseparate dini na Imani.

MUUMBA ni mmoja kubali kataa panda shuka kwenye izo dini na dhehebu lakini kweli itabaki kweli aliyeumba ni mmoja DINI ndo zilileta utengano na kupotosha kweli.
 
Umeaminishwa kwamba atapeleka motoni watu wote kasoro 144k lakini ungejua falme na malmlaka za giza walitaka kila mtu hahukumiwe ili MUUMBA asibaki na chochote na lakini kwa uheri alisema katika
Isaya 43:25 “Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.”

Hivyo wengi hudhani kuna kiama mara mwisho wa dunia kwa nadharia walizofundishwa wasijue mwisho ulishafika na MUUMBA anawakomboa watu wake kwa kila anayekubali msamaha wa bure.
So Isaya ni ya kweli Ila Ufunuo ni uwongo. Why coz umesema tu... Bac mi nasema Biblia nzima ni uwongo. Si unaamua tu kupotezea sehemu zingine unafata zinazokuvutia...ndo ukristo huo.
 
MUUMBA ni mmoja kubali kataa panda shuka kwenye izo dini na dhehebu lakini kweli itabaki kweli aliyeumba ni mmoja DINI ndo zilileta utengano na kupotosha kweli.
Unajuaje Ni mmoja na sio kiwanda Cha watu.
 
Usitake kuonekana mwelevu kufanya kufuru ili ufurahishe watu au kikundi fulani nakushauri usijitafutie laana kwa haya maandiko yako maana hasira ya Mungu ni kali sana tubu jiepusha na hizi kauli (acha kumfanyia kazi shetani kupotosha kondoo wa Mungu ) usipo sikia ipo siku na saa utakumbuka maandishi haya
Acha mikwara wewe
 
Lakini ukinunua gazeti ukisoma si unalielewa bila mtafsiri. Lakini unahitaji mtafsiri akusomee Biblia. Acheni uoga Biblia sio neno la Mungu ni neno la walimtunga Mungu ndo maana kila kukicha utaskia dhehebu linatokea kwa sababu ni kitabu Kama Malaya kinatafsiriwa kivyovyote vile coz hakijaandikwa vizuri..
Gazeti moja mhandishi mmoja ila wasomaji tofauti Jiulize wasomaji wote wanaweza kuwa na mawazo Sawa na mhandishi wa hoja hizo ?
Na iweje huyo mtafsiri aelewe na wewe usielewe kama unavyoelewa gazeti ?
 
Back
Top Bottom