Kama yupo ndani yako huyo si Mungu huyo ni akili yako na fikra zako na ukifa na ye anakufa
Watu wanapenda kujidanganya kwamba wanajua kila kitu.
Na pale ambapo hawana jibu, wanapenda kuweka jibu la Mungu, ambaye hayupo.
Nia yao wawe na jibu tu, hata kama si la kweli.
Hawataki kukosa jibu.
Ukiwauliza maswali kuhusu mambo ambayo hawana majibu, kama kifo, waseme "kazi ya Mungu, haina makosa".
Dhana ya kuwepo Mungu ni hadithi ya kutunga ili liwepo chaka la kutupia maswali yote ambayo hatuna majibu yake.
Halafu tukipata majibu, tunayatoa katika chaka hilo polepole.
God of the gaps.
Ndiyo maana jamii zilizopiga maendeleo ya kielimu kama Ulaya ya Kaskazini, watu wanaacha kumuamini huyu Mungu kwa kasi kubwa sana.
Hawahitaji hili chaka tena, elimu yao imeondoa maswali mengi kutoka kwenye hili chaka.
Wakati huohuo, jamii ambazo zina matatizo ya elimu kama Africa, imani ya Mungu iko juu sana.
Mtu wa Ulaya Kaskazini anapata elimu kirahisi, anajua mengi, akiumwa ana mfumo wa afya ya jamii anaoweza kuutegemea. Hahitaji kuomba Mungu.
Wewe mtu masikini wa Africa, huna elimu, huna huduma bora za afya, ukiumwa ni lazima uombe Mungu tu.