min -me
JF-Expert Member
- Jul 20, 2022
- 61,672
- 178,673
Asante sana master nasubiri kwa bashashaKuna vitu vingi vyenye mkanganyiko hapo, nitaijibubkwa nukuu.
Asante sana master nasubiri kwa bashashaKuna vitu vingi vyenye mkanganyiko hapo, nitaijibubkwa nukuu.
Unaposema kitu kipo na kingine hakipo una maana gani?Unabidi kujua kuwa dini hazipo Ila Mungu yupo kwakuwa dini zimekuja juzi juzi hapa na zinatumika Kama njia ya kupotosha na sio kujenga .
Ukifatilia kiundani utagundua kuwa IPO nguvu moja Ila unaweza kuamua uitumieje .
Dah majibu ya haya maswali sijui niseme yanayohitaji tafakuru ya kina ama ukweli wa mambo🤔Unaposema kitu kipo na kingine hakipo una maana gani?
Kuwepo ni nini?
Kwa nini unasema dini hazipo halafu unasema zimekuja juzi juzi hapa? Kitu ambacho hakipo kimekujaje juzi juzi hapa? Huoni kuwa hiyo ni contradiction?
Nguvu moja unayoisema ni ipi? Kwa nini ni moja si mbili, tatu au zaidi?
Thibitisha kimantiki Mungu yupo.
Mi nadhani kigezo cha kwanza cha kuamua Mungu aliye sahihi ni uthibitisho wa uwepo wake.
Unaposema kitu kipo na kingine hakipo una maana gani?
Kuwepo ni nini?
Kwa nini unasema dini hazipo halafu unasema zimekuja juzi juzi hapa? Kitu ambacho hakipo kimekujaje juzi juzi hapa? Huoni kuwa hiyo ni contradiction?
Nguvu moja unayoisema ni ipi? Kwa nini ni moja si mbili, tatu au zaidi?
Thibitisha kimantiki Mungu yupo.
Hii ni tafakuru ya kina sana 🤔 ndio maana mimi mda mwingine nafikiri mungu kwa umoja wake inaweza kuwa kila kitu katika muktadha tofauti tofauti , mawe, kinyesi milima mabonde , wafu , walio hai na kila aina ya kilichokuwepo na hata vinavyosadikika kutokuwepo , ila hii ni kwa akili zangu za kilevi tu🤔Mi nadhani kigezo cha kwanza cha kuamua Mungu aliye sahihi ni uthibitisho wa uwepo wake.
Kwasababu baadhi ya dini kuthibitisha Mungu yupo inaweza kuwa ishu simple, ukaletewa ng'ombe ukaambiwa huyo ndio Mungu.
So tutapima hali ya uwepo wake una influence gani katika chanzo cha ulimwengu na vilivyomo.
Ikiwa Mungu hana dini huo ukweli wake tutaupata kupitia njia gani?Ukweli ni kwamba Mungu hana dini na wala hajali kuhusu dini yoyote ile isipokuwa ni muhimu kwake kwamba wandamu wanaufahamu ukweli wake.
Ni mapungufu ya wanadamu kuelewa UKWELI. Pia ni strategy ya "shetani" kuleta mvurugano kati ya wanadamu.
Hukumu itakuwa kwa kila mtu kadiri ya anachojua na kufanya. Kimsingi kila mtu anacho kitu moyoni mwake kama ubao wa sheria hivi na utahukumiwa kwa hicho na watu watashangaa sana kwamba dini kwa kiasi kikubwa ni hadaa!
Miungu ya Ki-africa? Kimsingi Mungu ni Mmoja aliye Mwenyezi na baada ya hapo ni miungu ambayo ni viumbe tu wa yule Mwenyezi. Na sio Waafrika pekee huabudu miungu, hata wazungu na wachina pia na hii huweza kuitwa mizimu na ndiyo imechukua sehemu kubwa Africa.
Ni kweli miungu hii haina nguvu ikilinganishwa na Mungu Mwenyezi. Hatupaswi kujiweka chini ya miungu hii dhaifu.
😁😁😁😁 inafikirisha Mkuu umetishaHii ni tafakuru ya kina sana 🤔 ndio maana mimi mda mwingine nafiki mungu kwa umoja wake inaweza kuwa kila kitu katika muktadha tofauti tofauti , mawe, kinyesi milima mabonde , wafu , walio hai na kila aina ya kilichokuwepo na hata vinavyosadikika kutokuwepo , ila hii ni kwa akili zangu za kilevi tu🤔
Sio kweli bado sio mlango wa mwisho wa fikra🤣😁😁😁😁 inafikirisha Mkuu umetisha
Ikiwa Mungu hana dini huo ukweli wake tutaupata kupitia njia gani?
Na Yehova ni naniMungu ni mmoja na Yesu kristo ndio jina lake!
Amen.
Sio kweli bado sio mlango wa mwisho wa fikra🤣
... kwanza kabisa, watu hawana tafsiri moja ya Mungu. Kwa wengine, Mungu ni yule wa Biblia au Qur’an Muumba mwenye nguvu zote, anayejua kila kitu. Kwa wengine, ni nguvu tu ya asili, au hata hali fulani ya juu ya akili. Kwa hiyo kusema “Mungu yeyote” ni kama kusema “chochote kinaweza kuwa Mungu” – lakini hilo si rahisi kulieleza kwa mantiki.Mungu ni nini kwanza?
Africa hawana tofauti Sana na wanyama wa kawaida wapo vision less .MIUNGU ya Africa ilikuwa strong sema ilisimikwa kwenye vichwa vya wasio na akili ikasahaurika. Cultures dhaifu humezwa na Cultures strong ndo mfumo wa dunia ulivyo.
Africans ni viumbe dhaifu ki akili ukilinganisha na race nyingine mwarabu is next to us kwa wehu
Mungu anaye ongelewa na kutetewa na binadamu badala ya yeye kujitetea mwenyewe ni Mungu wa kutungwa na binadamu.
Naunga mkono hojaMungu anaye ongelewa na kutetewa na binadamu badala ya yeye kujitetea mwenyewe ni Mungu wa kutungwa na binadamu.
Mungu ni dhana uchwara iliyotungwa na binadamu ndio maana siku zote ni binadamu tu, wanahangaika kumwelezea, kumtetea na kumwongelea huyo Mungu wa kutunga.
Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kujitetea mwenyewe, kujidhihirisha mwenyewe na kujiongelea mwenyewe.
Mungu ni fictional character.
Hakuna Mungu.
Tunaupata ukweli wa Mungu kwa kupitia njia mbalimbali kama sayansi na mafunuo ya kiroho. Haya yanaweza kupatikana kutoka dini yoyote ile ila pia nje ya dini.Ikiwa Mungu hana dini huo ukweli wake tutaupata kupitia njia gani?
Kiuhalisia Mungu ni wengi ila Muumba ni mmoja na hana dini na hapo wengi ndipo walipigwa chenga na mifumo na falme na mamlaka wasijue wanachokiabudu hata Yesu aliwaambia wana wa israel kuwa hawajui wanachokiabudu rejea Yohana 4:22.Uchambuzi wa kina
1. "Kama Mungu ni mmoja mbona kuna dini nyingi?"
Kihoja: Hili linauliza juu ya mkinzano kati ya dhana ya Mungu mmoja (monotheism) na uwepo wa dini mbalimbali duniani.
Kiuhalisia: Dini hutofautiana kwa sababu ya tamaduni, historia, siasa, jiografia, lugha, na mapokeo ya watu mbalimbali.
Kifalsafa: Inaibua swali—Je, dini ni njia tofauti za kuelekea kwa Mungu mmoja? Au ni tafsiri za binadamu juu ya nguvu isiyoonekana?
2. "Mbona sheria zinapingana?"
Hii inahusu tofauti za maadili, sheria za kidini na sheria za kijamii au kitaifa.
Mfano: Katika dini moja jambo fulani ni haramu kabisa, lakini kwa jamii nyingine ni la kawaida.
Maswali ya kina: Sheria hizi ni sauti ya Mungu au ni tafsiri ya binadamu juu ya yale wanayodhani ni mapenzi ya Mungu?
3. "Nini hatima na hukumu ya watenda dhambi ikiwa kila dini na sheria yake?"
Swali la kiroho: Ikiwa kila dini ina mbingu na moto wake, je, hatima ya mtu inategemea dini aliyozaliwa au aliyoichagua?
Swali hili linaathiri wazo la haki ya kimungu na upendeleo. Je, Mungu anaweza kumhukumu mtu kwa kufuata njia aliyorithi bila kujua nyingine?
4. "Je ni kweli miungu ya Afrika haina nguvu au imepuuzwa?"
Kihistoria: Dini za Kiafrika zilitumika kabla ya ujio wa dini za Kimagharibi (Ukristo, Uislamu).
Swali la kiutambulisho: Je, kupuuzwa kwa miungu ya Kiafrika ni matokeo ya ukoloni wa kiroho?
Falsafa: Kama miungu hiyo ilikuwa na nguvu, je bado inafanya kazi, au miungu yao ilikuwa haina nguvu
Karibuni.