Mungu yupi ni sahihi? Karibu tujadili

Mungu yupi ni sahihi? Karibu tujadili

... kwanza kabisa, watu hawana tafsiri moja ya Mungu. Kwa wengine, Mungu ni yule wa Biblia au Qur’an Muumba mwenye nguvu zote, anayejua kila kitu. Kwa wengine, ni nguvu tu ya asili, au hata hali fulani ya juu ya akili. Kwa hiyo kusema “Mungu yeyote” ni kama kusema “chochote kinaweza kuwa Mungu” – lakini hilo si rahisi kulieleza kwa mantiki.
Sijauliza tafsiri ya Mungu ni nini, nimeuliza Mungu ni nini?

Umeelewa swali?
 
Thibitisha.
GOD Can not be defined,confined,bounded,limited or restricted.
GOD is infinite in power, infinite in time, infinite,infinite in space.
GOD is the ALL,There is no place outside the ALL, It's continuous in space, without Break, cessation, Separation or Interruption.
GOD is the ALL,GOD is the INFINITE LIVING MIND!!
 
GOD Can not be defined,confined,bounded,limited or restricted.
GOD is infinite in power, infinite in time, infinite,infinite in space.
GOD is the ALL,There is no place outside the ALL, It's continuous in space, without Break, cessation, Separation or Interruption.
GOD is the ALL,GOD is the INFINITE LIVING MIND!!
Umeandika shairi, hujathibitisha.
 
Uchambuzi wa kina

1. "Kama Mungu ni mmoja mbona kuna dini nyingi?"

Kihoja: Hili linauliza juu ya mkinzano kati ya dhana ya Mungu mmoja (monotheism) na uwepo wa dini mbalimbali duniani.

Kiuhalisia: Dini hutofautiana kwa sababu ya tamaduni, historia, siasa, jiografia, lugha, na mapokeo ya watu mbalimbali.

Kifalsafa: Inaibua swali—Je, dini ni njia tofauti za kuelekea kwa Mungu mmoja? Au ni tafsiri za binadamu juu ya nguvu isiyoonekana?


2. "Mbona sheria zinapingana?"

Hii inahusu tofauti za maadili, sheria za kidini na sheria za kijamii au kitaifa.

Mfano: Katika dini moja jambo fulani ni haramu kabisa, lakini kwa jamii nyingine ni la kawaida.

Maswali ya kina: Sheria hizi ni sauti ya Mungu au ni tafsiri ya binadamu juu ya yale wanayodhani ni mapenzi ya Mungu?


3. "Nini hatima na hukumu ya watenda dhambi ikiwa kila dini na sheria yake?"

Swali la kiroho: Ikiwa kila dini ina mbingu na moto wake, je, hatima ya mtu inategemea dini aliyozaliwa au aliyoichagua?

Swali hili linaathiri wazo la haki ya kimungu na upendeleo. Je, Mungu anaweza kumhukumu mtu kwa kufuata njia aliyorithi bila kujua nyingine?


4. "Je ni kweli miungu ya Afrika haina nguvu au imepuuzwa?"

Kihistoria: Dini za Kiafrika zilitumika kabla ya ujio wa dini za Kimagharibi (Ukristo, Uislamu).

Swali la kiutambulisho: Je, kupuuzwa kwa miungu ya Kiafrika ni matokeo ya ukoloni wa kiroho?

Falsafa: Kama miungu hiyo ilikuwa na nguvu, je bado inafanya kazi, au miungu yao ilikuwa haina nguvu

Karibuni.
Kila dini na dhehebu linavutia kwake ni sawa tu na mimi kuvutia imani yangu ya Kiafrika ambayo ndiyo DNA yangu, sijawahi kuomba kwa imani ya dini za kuletewa nikafanikiwa hata siku moja ila nikiomba kupitia mizimu yangu nafanikiwa na ndiyo maana sijihusishi na dini za kuletewa hata siku moja, sioni umuhimu wake kwangu.
 
Back
Top Bottom