Mungu yupi ni sahihi? Karibu tujadili

Mungu yupi ni sahihi? Karibu tujadili

Uchambuzi wa kina

1. "Kama Mungu ni mmoja mbona kuna dini nyingi?"

Kihoja: Hili linauliza juu ya mkinzano kati ya dhana ya Mungu mmoja (monotheism) na uwepo wa dini mbalimbali duniani.

Kiuhalisia: Dini hutofautiana kwa sababu ya tamaduni, historia, siasa, jiografia, lugha, na mapokeo ya watu mbalimbali.

Kifalsafa: Inaibua swali—Je, dini ni njia tofauti za kuelekea kwa Mungu mmoja? Au ni tafsiri za binadamu juu ya nguvu isiyoonekana?


2. "Mbona sheria zinapingana?"

Hii inahusu tofauti za maadili, sheria za kidini na sheria za kijamii au kitaifa.

Mfano: Katika dini moja jambo fulani ni haramu kabisa, lakini kwa jamii nyingine ni la kawaida.

Maswali ya kina: Sheria hizi ni sauti ya Mungu au ni tafsiri ya binadamu juu ya yale wanayodhani ni mapenzi ya Mungu?


3. "Nini hatima na hukumu ya watenda dhambi ikiwa kila dini na sheria yake?"

Swali la kiroho: Ikiwa kila dini ina mbingu na moto wake, je, hatima ya mtu inategemea dini aliyozaliwa au aliyoichagua?

Swali hili linaathiri wazo la haki ya kimungu na upendeleo. Je, Mungu anaweza kumhukumu mtu kwa kufuata njia aliyorithi bila kujua nyingine?


4. "Je ni kweli miungu ya Afrika haina nguvu au imepuuzwa?"

Kihistoria: Dini za Kiafrika zilitumika kabla ya ujio wa dini za Kimagharibi (Ukristo, Uislamu).

Swali la kiutambulisho: Je, kupuuzwa kwa miungu ya Kiafrika ni matokeo ya ukoloni wa kiroho?

Falsafa: Kama miungu hiyo ilikuwa na nguvu, je bado inafanya kazi, au miungu yao ilikuwa haina nguvu

Karibuni.
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
Mungu anaye ongelewa na kutetewa na binadamu badala ya yeye kujitetea mwenyewe ni Mungu wa kutungwa na binadamu.

Mungu ni dhana uchwara iliyotungwa na binadamu ndio maana siku zote ni binadamu tu, wanahangaika kumwelezea, kumtetea na kumwongelea huyo Mungu wa kutunga.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kujitetea mwenyewe, kujidhihirisha mwenyewe na kujiongelea mwenyewe.

Mungu ni fictional character.

Hakuna Mungu.
Kama hakuna Mungu je Binadamu ametokana na nini Mkuu ?
 
Ni miungu yupi huyo ambayo ilikua na nguvu Afrika au mnataka kusema Mungu aliye muumba Mwafrika na Mzungu ni tofauti?
 
Kama hakuna Mungu je Binadamu ametokana na nini Mkuu ?
Je ni lazima binadamu awe ametokana na kitu fulani?

Kwani binadamu hawezi kutokana na yeye mwenyewe?

Binadamu anatoka kwa binadamu.

Simba anatoka kwa Simba🦁

Chui anatoka kwa chui.

Nyoka anatoka kwa nyoka.

Hakuna chochote kinachotoka kwa huyo Mungu.

Vitu vyote vinatoka hapahapa ulimwenguni vyenyewe tu.
 
Kama hakuna Mungu je Binadamu ametokana na nini Mkuu ?
Kama kila kitu lazima kiwe na Muumba, basi Mungu mwenyewe alitokea wapi – au yeye ndiye kitu pekee kisicho na chanzo? Kama Mungu anaweza kuwepo bila kuumbwa, kwa nini na ulimwengu usiwe hivyo hivyo?”
 
Africa hawana tofauti Sana na wanyama wa kawaida wapo vision less .
Na sio tu WAAFRICA bali weusi wote ni race yenye default kichwani ndo maana hata ukizaliwa kwa wazungu tatizo ni lile lile mifano ipo mingi sana eg 2pac,Pdidy,R kelly na ndiyo maana ubaguz wa rangi unatokea.Mimi nafuga mbuzi ila kuna ka beberu kabaya mbegu fupi nimekahasi ili kasiniharibie zizi
 
Tunaupata ukweli wa Mungu kwa kupitia njia mbalimbali kama sayansi na mafunuo ya kiroho. Haya yanaweza kupatikana kutoka dini yoyote ile ila pia nje ya dini.
Hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wa Mungu kupitia sayansi...maana Mungu bado anajificha
Mafunuo ya kiroho yametifautiana Wengine wanamwona Mungu kama kiumbe mwenye taswira ya ng'ombe, wengine wanasikia tu sauti na wote wanaamini Mungu wao ndie sahihi
 
Na sio tu WAAFRICA bali weusi wote ni race yenye default kichwani ndo maana hata ukizaliwa kwa wazungu tatizo ni lile lile mifano ipo mingi sana eg 2pac,Pdidy,R kelly na ndiyo maana ubaguz wa rangi unatokea.Mimi nafuga mbuzi ila kuna ka beberu kabaya mbegu fupi nimekahasi ili kasiniharibie zizi
Dah wewe jamaa 😁😁
 
Hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wa Mungu kupitia sayansi...maana Mungu bado anajificha
Mafunuo ya kiroho yametifautiana Wengine wanamwona Mungu kama kiumbe mwenye taswira ya ng'ombe, wengine wanasikia tu sauti na wote wanaamini Mungu wao ndie sahihi
Hakuna kitu kinaashiria uwepo wa Mungu kama sayansi. Yote ambayo sayansi huyasoma na kuyagundua ni kazi zake. Tatizo ni uelewa wa watu kufikiri kwamba Mungu amejificha na walitaka kumwona kwa macho wakati hayupo katika hali ya kuonekana. Kwani wewe umewahi kuona mawimbi ya simu kwa macho? Je yapo au hayapo?
 
Kabla hujauliza "Mungu" yupi ni sahihi ningependa kwanza utoe maana ya neno "Mungu" - kwasababu kama mimi binafsi sijui maana yake.
 
Ni Jina la Mungu.
Yohana 14:28 - Yesu anasema, "Baba ni mkubwa kuliko mimi." Hii inaonyesha tofauti kati ya Yesu na Baba, ikionyesha kwamba Yesu hakuwa akijitangaza kama Mungu.
Matayo 19:17 - Yesu anasema, "Kwa nini unaniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, yaani, Mungu." Hapa, Yesu anajitenga na sifa ya uungu.
Marko 10:18 - Katika aya hii, Yesu anasema, "Mtu mmoja akamwambia, Mwalimu mwema, ni nini mema nitaweza kufanya ili nipate uzima wa milele? Yesu akamjibu, Mbona unaniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, yaani, Mungu." Hii inaonyesha kwamba Yesu anajitenga na dhana ya kuwa Mungu au mimi sijaelewa.
 
Mungu ni nini kwanza?
Mungu ni nini kwanza?
MUNGU ni sisi,wale,hivi na vile.MUNGU ni nguvu inayotumia miili yetu kuji manifest,miili ya wanyama,miili ya wadudu,miili ya mimea mbali mbali.
Tuko katika existence kama viungo mbali mbali vya NGUVU-MUNGU.
Hiyo NGUVU-MUNGU inatenda kupitia sisi,bila uwepo wetu haiwezi kufanya chochote.
Hakuna MUNGU eti katika sura ya Mwanadamu,Ng'ombe na kadhalika.
Sisi sote(Binadamu,wanyama,wadudu na mimea),ni sehemu ya MUNGU.
 
Kabla hujauliza "Mungu" yupi ni sahihi ningependa kwanza utoe maana ya neno "Mungu" - kwasababu kama mimi binafsi sijui maana yake.
Imeshaelezewa
Yohana 14:28 - Yesu anasema, "Baba ni mkubwa kuliko mimi." Hii inaonyesha tofauti kati ya Yesu na Baba, ikionyesha kwamba Yesu hakuwa akijitangaza kama Mungu.
Matayo 19:17 - Yesu anasema, "Kwa nini unaniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, yaani, Mungu." Hapa, Yesu anajitenga na sifa ya uungu.
Marko 10:18 - Katika aya hii, Yesu anasema, "Mtu mmoja akamwambia, Mwalimu mwema, ni nini mema nitaweza kufanya ili nipate uzima wa milele? Yesu akamjibu, Mbona unaniita mwema? Hakuna mwema ila mmoja, yaani, Mungu." Hii inaonyesha kwamba Yesu anajitenga na dhana ya kuwa Mungu au mimi sijaelewa.
gu ni roho isiyo na mipaka, asiye na muda wala mwili. Sasa, anawezaje kuwa binadamu mwenye mwili, aliye na njaa, uchovu, na maumivu – bila kupoteza uungu wake?”



Kifalsafa:

Hili linapingana na sifa za lazima za Mungu: ukamilifu, kutoathirika, kutojifungia kwenye muda na nafasi.

Kwa hiyo, kusema Mungu aligeuka kuwa mtu ni sawa na kusema Mungu alijikana mwenyewe
 
Uchambuzi wa kina

1. "Kama Mungu ni mmoja mbona kuna dini nyingi?"

Kihoja: Hili linauliza juu ya mkinzano kati ya dhana ya Mungu mmoja (monotheism) na uwepo wa dini mbalimbali duniani.

Kiuhalisia: Dini hutofautiana kwa sababu ya tamaduni, historia, siasa, jiografia, lugha, na mapokeo ya watu mbalimbali.

Kifalsafa: Inaibua swali—Je, dini ni njia tofauti za kuelekea kwa Mungu mmoja? Au ni tafsiri za binadamu juu ya nguvu isiyoonekana?


2. "Mbona sheria zinapingana?"

Hii inahusu tofauti za maadili, sheria za kidini na sheria za kijamii au kitaifa.

Mfano: Katika dini moja jambo fulani ni haramu kabisa, lakini kwa jamii nyingine ni la kawaida.

Maswali ya kina: Sheria hizi ni sauti ya Mungu au ni tafsiri ya binadamu juu ya yale wanayodhani ni mapenzi ya Mungu?


3. "Nini hatima na hukumu ya watenda dhambi ikiwa kila dini na sheria yake?"

Swali la kiroho: Ikiwa kila dini ina mbingu na moto wake, je, hatima ya mtu inategemea dini aliyozaliwa au aliyoichagua?

Swali hili linaathiri wazo la haki ya kimungu na upendeleo. Je, Mungu anaweza kumhukumu mtu kwa kufuata njia aliyorithi bila kujua nyingine?


4. "Je ni kweli miungu ya Afrika haina nguvu au imepuuzwa?"

Kihistoria: Dini za Kiafrika zilitumika kabla ya ujio wa dini za Kimagharibi (Ukristo, Uislamu).

Swali la kiutambulisho: Je, kupuuzwa kwa miungu ya Kiafrika ni matokeo ya ukoloni wa kiroho?

Falsafa: Kama miungu hiyo ilikuwa na nguvu, je bado inafanya kazi, au miungu yao ilikuwa haina nguvu

Karibuni.
Ni sawa na kusema kama elimu ni moja kwanini kuna shule nyingi 🤔
 
Mungu ni nini kwanza?

MUNGU ni sisi,wale,hivi na vile.MUNGU ni nguvu inayotumia miili yetu kuji manifest,miili ya wanyama,miili ya wadudu,miili ya mimea mbali mbali.
Tuko katika existence kama viungo mbali mbali vya NGUVU-MUNGU.
Hiyo NGUVU-MUNGU inatenda kupitia sisi,bila uwepo wetu haiwezi kufanya chochote.
Hakuna MUNGU eti katika sura ya Mwanadamu,Ng'ombe na kadhalika.
Sisi sote(Binadamu,wanyama,wadudu na mimea),ni sehemu ya MUNGU.
Thibitisha.
 
Mungu yupo God exist na Mungu hauwezi ukasema yupo kwa kuthibitisha Ila ni Experience za MTU na MTU .

Katika logic , ili uweze kujua Mungu hayupo lazima utambue kila kitu kina chanzo kwahiyo Chanzo cha kuwepo binadamu n.k maana yake kuna Mamlaka iliyo juu yake huyo Binadamu.

Hata wewe bwana Kiranga IPO nguvu iliyo juu yako ambayo imekuwa ikiendesha maisha yako either kwa kujua au kutokujua ndo maana baadhi ya mambo unaweza kuona yanatokea tu pasiipo kuyazuia.

Kukataa Kuwa Hamna Mungu au nguvu iliyo juu yako ni kukataa Chanzo chako .

Wewe una chanzo chako Kama binadamu
Habari ya "experience ya mtu" ni logical fallacy.

Unaelewa hilo?
 
Back
Top Bottom