Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.
Naomba majibu ya maswali yangu
Yapo page no 5

Hebu jibu acha kupiga blabla tu hapa!

Page no 5 ya Samsung Note II si sawa na page no 5 ya HP ENVY Touchsmart.

Huku inaweza kuwa page number 5 kule ikawa page 15 kutegemea na pagination ya device, screen size etc.

Usiwe simpleton kufikiri pages ni uniform.

Toa post number na specific questions.
 

Mbona mkuu Stephano Mtangoo ameishatoa jibu kuhusu hili! Amesema kuwa binadamu tumepewa na MUNGU a free will, kuchagua kati ya mema au mabaya. Hata wewe Kiranga uko uliko yawezekana kuwa unaishi vizuri tu na jamii iliyokuzunguka regardless of you being an Atheist.
 
Last edited by a moderator:
Hahaa yaani binadamu yuko compassionate zaidi ya mungu!

Ndo maana nishasema ukiamua kuamini hizi habari za mungu ni lazima ujitoe fahamu walau kidogo la sivyo utaishia kuona dhani nzima ni a bunch of BS tu.

Bill Gates mabilioni yake yanahesabika, upendo wake una mipaka na ujuzi wake una mipaka lakini kagawa sehemu ya fortune na muda wake ili watoto wa nchi masikini wapate chanjo za polio.

Mungu ambaye ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote angeweza kuweka ki gene tu katika damu kikawa automatic vaccination kwa kila mtoto anayezaliwa hajafanya hivyo.

Kwa nini?

Huyu mungu yupo kweli jamani?

Au tunapigana kamba tu?

Kama yupo mbona hata Bill Gates anamshinda?
 
Mmmh; Kiranga, mwaka huu kazi unayo!

Kweli!

Anatakiwa athibitishe vinginevyo haya madai

Mpaka sasa hajafanya hivyo
Na kuthibitisha vinginevyo sio kukataa tu
Unaposema gari hili halijatengenezwa na Paulo inabidi utuambie ni nani ametengeneza

Sio kusema hujui
Kama hujui kwanini unakanusha?
 

Na mimi nimeuliza.

Kama mungu anathamini sana free will kwa nini hakuniuliza mimi nichague kwa freewill kama nataka kuzaliwa dunia hii au sitaki?

Huyu mungu mbona anathamini free will selectively?

Halafu utasemaje mungu anathamini free will wakati tunaambiwa kila kitu ni kwa neema yake tu?

Which is which now? Vitu tunafanya kwa free will au kwa neema yake tu?

Maana tunaambiwa alishayajua maisha yetu mwanzo mpaka mwisho kabla hatujazaliwa, na alichokijua hakibadiliki.

Sasa kama alichokijua hakibadiliki, na hatuna jinsi ya kukiepuka, free will inakujaje hapo?

Naomba nijibu mawili hayo.

Kama mungu anathamini free will sana, kwa nini hakuniuliza kama nataka kuzaliwa dunia hii?

Pia, kama kila kitu ni kwa neema yake tu, yeye kayajua maisha yetu mwanzo mwisho, free will inatoka wapi hapo?
 
The problem of evil remain unanswered.

I need not go further until this problem is solved.

wakati mwingine huwezi kupata jibu kwa kuwa we huna imani ya uwepo wa Mungu. Hatuwezi kuyajua maovu kwa usahihi kwa kuwa hata hatujui kwa yakini chanzo chetu nini. Wala hatujui kwa yakini hatima yetu ni ipi. Kifupi hatuko huru kwa kuwa hatuujui ukweli. Na kwa kuwa tunauliza kuhusu uovu ni wazi hatuujui ukweli. Jema au baya tumeyajua kwa matokeo yake, na labda kwa kusoma au kuambiwa. Kuujua ukweli ndio tiketi ya kujua uovu ni nini. Ni nani aujuaye ukweli?
 

Argument from design tume i demolish a hundred times and more here.

Kama unasema complexity ni lazima iwe imeumbwa, kilichoiumba ni complex zaidi, nacho ni lazima kiwe kimeumbwa, ad infinitum ad absurdity. Huwezi kusema kiti cha ndege ni lazima kiwe kimeumbwa lakini Jumbo Jet linalopaa angani na viti kwa mamia halijaumbwa.Huwezi kusema binadamu kaumbwa, lakini muumbaji wake hakuumbwa. Na ukishasema muumbaji wake kaumbwa, unaingia katika chain ya waumbaji isiyoisha.


Same complexity argument as above Sayansi gani hiyo? Unaweza kutaja theory moja au experiment moja kuthibitisha kwamba maneno haya yanatokana na sayansi na si hocus pocus ? Halafu ukishasema "unaamini" unaondoka kwenye mada.Unaruhusiwa kuamini chochote, dispute ipo kwenye ujuzi, si imani.

ani. Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aumbe viumbe wake awape mateso ya magonjwa na ujinga na njaa na matetemeko ya ardhi na vilema dunia hii? Wengine wanazaliwa na vilema tangu watoto? Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aruhusu hili?

Yesu angekuwep leo watu wa PETA (People for the Ethical Treatment of Animals) wangempiga lawsuit kwa kuwa hana ethics na compassion kwa wanyama. Kwa nini aliyatoa majini kwa kichaa na kuyapeleka kwa nguruwe waliokufa majini?

Kwa nini aliulaani mti mtini kwa kutozaa matunda wakati nema ya kuzaa matunda inatoka kwa mungu?

Halafu mbona aliwafunga kamba washkaji kwamba atarudi katika kizazi chao, jamaa wakauza majumba na mashamba yao wamsubiri, kajikata jii mpaka leo hajarudi?
 

Angalau wewe umesema kwamba hatujui ukweli.

Na kutojua ukweli huku kunajumuisha kutojua kwamba mungu yupo kwa uhakika.

Ila watu wabishi tu, kwa sababu washamfanya mungu kama kimbilio pasipo na kimbilio.

it is a psychologically comforting thought to think that there is a big man responsible for everything.
 
Nimejifunza mengi kupitia uzi huu, lakini kikubwa zaidi nimepata kuifahamu Imani ya Kiranga na wenzake, japo hawataki kujiweka wazi kuwa ni Waumini wa Imani hiyo.
 
Bado unapiga blaa blaa tu hapa, wewe jibu swali, NI NANI ALIYEKUAMBIA (or rather, UNA UTHIBITISHO GANI) kuwa huyo mungu wako ndiye Owner wa hii dunia kiasi kwamba atukuzwe kwa kuacha a-set lolote atakalo?
Sasa wewe unayekataa Mungu sio owner tuambie mmiliki wa dunia hii? Mi nimeshakwambia ni Mungu.
Umeona dini yenu inavyowafanya vipofu?
 
Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" maishani mwako?
Soma zaidi hapa Immanent critique - Wikipedia, the free encyclopedia

Lete majibu ya hoja husika badala ya link. Kwa mtu unayedai kufanya mambo kwa fikra siktarajii link bali majibu mujarabu. Link waachie wengine.

Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.
Mimi nina pa kuanzia wewe huna. Mimi naanza na Mungu na kutoka hapo napata Mantiki kwa sababu nimeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenye mantiki. Napata sheria za kimaadili (Moral laws) kwa sababu nimeumbwa kwa mfanow wa Mungu aliye chanzo cha sheria hizo. Ninatumia sayansi kwa sababu Mungu ameweka uniformity na kufanya sayansi iwezekane.

Wewe unaelea tu. Huna pa kusimamia. Una argue kwa kutumia logic, lakini huna sababu kwa nini utumie logic. Unajaribu kumkosoa Mungu kuwa ana makosa ya kimaadili bila kutuambia unapataje maadili katika dini yako ya hakuna Mungu. Unaongea sana kuhusu sayansi lakini katika dini yako ya hakuna Mungu unapataje sayansi?

Inabidi uibe kutoka kwa Mungu unayemkana... What a proof for God's existence!

No hii sio mechi wala sio majaribio. Ni kitu kiko halisi na kina madhara kukubali au kukataa.
Kwa hiyo sioni haja ya kuhangaika na majaribio yako. Ni aidha unakataa au unakubali. Na ukikataa, ishi consistent na dini yako ya hakuna Mungu. Hiyo ndiyo maanaya kuwa na utashi!

Hii inafanya maswali yako yawe meaningless!

Kwa sababu dini yake imeshindwa kutoa hata tafsiri ya uovu umeamua kuhamia kwa Mungu kwa muda?
No free lunch. Aidha unamkataa au unamkubali... nukta!


Naona somo zima la "immanent critique" limekupitia mbali.
Wala hata sio la muhimu kama unavyodhani!

Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.
And that makes whole thing silly!

Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri. Hapo hujamhitaji mungu.
Lets see!

Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.
Hitler aliua watu million 6+ kwake lilikuwa Jema. Stallin, Mao na wengineo wakaua mamilion. Wao waliona sawa ni mema. Je unakubaliana nao kuwa walifanya mema. Au unadhani mabaya?

Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.
Kwa wale wanaojisikia fahari kubaka watoto wadogo nao vipi wako sahihi? Wanafanya mema au mabaya?

Kipimo chako cha mema na mabaya ni nini? Nataka kujua mizani unayotumia!

Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.
Fallacy! Sio kweli, hatujaona popote!

Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu

Secular morality - Wikipedia, the free encyclopedia
Hamna kitu hapo! Huwezi kuwa na morality bila kuwa na Moral laws and laws never pop from nothing. They demand Law giver. Kiranga whay can't you get it...soo simple!

This explanation fits you well. Dini yako ya hakuna Mungu imekufanya udhani kuwa kweli hakuna na kuwa "yote yawezekana kwake aaminiye hakuna Mungu".

Msome Albert Einstein hapa
Einstein kakusaidia hapo jinsi ya kupata moral code ambayo haimtegemei mungu.
Hizo ni assertion za Einstein. Hajatuambia ni jinsi gani elimu inatupa Moral law wala jinsi social ties zinavyolete Moral law na hivyo ni empty assertion.

Unakataa kuamini Mungu ambaye ameumba braini ya Einstein lakini unashindwa hata kuhoji upumbavu wa Einstein.
Sijui kama unapata picha ni kiasi gani dini yako hii imekupiga upofu!



Huu uongo wa "mungu ameacha mabaya kwa kuwa anapenda uhuru wa kuchagua" nilisha u debunk.
Hii ngano mbona haipo katika maneno uliyonukuu. Umeitoa wapi?

Kwanza jua Mungu ninayemwongelea sio mdoli wala mtumwa. Ni Mungu mwenye mamlaka ya kuamua, Alipoamua kuumba kwa mfano wake hakuomba ushauri. Kwa hiyo Mungu hakuumba mungu mwingine bali mwanadamu aliyebeba mfano wake. Kama mwanadamu na yeye akiwa Mungu kuna limits. Na moja ya limits ndio hizo.
Huna namna. Kama ambavyo utakufa na hna cha kufanya na hilo ni vivyo hivyo


Straw man argument!
Umetengeneza mungu bandia halafu umemdili sawasawa lol 🙂
Hayo yote Mungu wangu hajawahi kuyafanya! Get facts straight!


False premises, false conclusion!

Uwezo wa mwanadamu kumuasi mungu mwanadamu aliutoa wapi? Mungu alipoumba ulimwengu kwa nini aliruhusu uasi uwezekanike? Kama mungu kaumba ulimwengu na kuweka parameters zote, kwa nini aliruhusu parameters za ubaya kuwezekana?
Unapata shida kwa kuwa hutaki kukubali ukweli kuwa "Hapo Mwanzo Mungu..."
Tatizo ni dini yako ya hakuna Mungu...vinginevyo ni swali rahisi tu. Mungu aliumba mtu kwa mfano wake akiwa na uwezo wa kuchagua.... kutii au kuasi. God of Love made men with choice.

Huwezi kuelewa hili usipotaka kutoka huko gizani uliko aisee!

Usiniambie kwa sababu alitaka mwanadamu awe na chaguo, kwa sababu mimi hakunipa chaguo nizaliwe au nisizaliwe, na nizaliwe wapi, vipi, niishije etc. Huyu si mungu anayependa viumbe wake wawe na chaguo
Utasema hakukupa chaguo kwa kuwa hakukuruhusu ukalie kiti cha Mamlaka yake ya Uungu... silly argument!




Maswali haya nimejibu kitambo ila unayaleta kwa staili tofauti essentially ni yaleyale!
Na lengo lako ni kuondoka katka hoja za msingi ambazo so far hujajibu hata moja. Kiranga huwezi kutetea kitu ambacho kinapingana na mantiki, sayansi na hata akili ya kawada tu!
Utaishia kufanya vituko unavyofanya hapa!

Nani kakwambia naamini dini ya random and chance?
Mwanadamu alifikaje hapa alipo? Ulimwengu ulifikaje hapa ulipo?
Unaamini evolution ni ukweli au uongo?

Ushaoneshwa hapo juu kwamba huhitaji mungu kuwa na mema na mabaya. Wewe hujaweza kutuambia kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote kauumba ulimwengu huu, mbona ulimwengu una maovu mengi sana?
Zaidi ya taralila za Einstein na visasili vya "secular ethics" hujaleta chochote cha maana.


Kwa nini mungu alimuumba Hitler na kuruhusu haya mauaji? Ina maana alishindwa kuyazuia? Kama hakushindwa kwa nini hakuyazuia? Alipendezwa nayo?
Nimeuliza swali kwako usiyeamini Mungu. Huwezi kujibu ukiwa na imani ya dini yako ya hakuna Mungu.
Ili ujaribu hata kujibu lazima ukubali uwepo wa Mungu kwanza.


Ukweli mchungu ni kwamba hujajibu swali jepesi tu la "the problem of evil".
How does evil exists in religion of no morality like atheism? Its silly to even say the word!

Kifupi hujajibu hoja hata moja katika zote ambazo nimezileta. na hii kama nilivyosema mwanzo ni kwa sababu tamko la imani la dini yenu ya hakuna Mungu haliwaruhusu na mnakuwa force kujibu bila mantinki.

Kiukweli sijawahi kuona mkana Mungu yeyote akiishi sawia na dini yakehiyo. Wote ninaowafahamu wanaishi na Christian Morals za Mungu wanaye profess kumkataa! Strange!
 
Umevamia barua isiyouhusu ndio maana hujaielewa!
"For Christian consumption only"
 
The Bottom Line is: Absence ya Mungu ni imani kama uwepo wake,; kwa maneno mengine hakuna uthibitisho wa kutokuwepo Mungu kama ilivyo kwa uwepo wake! Eti Kaunga, hiki si ndicho ulichojifunza kutoka kwenye uzi huu, au?

Tell that to atheists who deny that! I set out to prove that from very beginning


Since there is no middle ground, you have to go either said. And I have proved that No God is the most irrational thing one can ever do 🙂
 
Aisee umenifanya nicheke sana! Duh!
Kilaini tena? Hili ni jina langu halisi wala sio uongo.

Wala hauhitaji PhD ili kumwonesha mtu kitu ambacho kipo.
kadoda11 umesahau huwa tuko wote kule kwenye teknolojia. Mi Mkristo wa kawaida tu sio askofu, padri wala sichungi kanisa!
 

Nisaidie nami nijue kama wewe UNA AKILI HATA KAMA SIO TIMAMU MKUU. Kama issue ni kujua,na kujua kunahitaji ushahidi wa wazi au sio ?
 
Hakuna majibu hapa ni ngano zilezile
Angalizop la majibu hujalisoma umeishia kukurupuka tu na yale uliyokariri bila kufikiri!



Haya ni mazoea ya kutokusoma na tafakuri
Umesoma mada wewe?

Haya yanatoka wapi?
 

Umefungua hiyo page ukaona kuna nini?
 
Theists are looser bro, watu wanyongefu wasioweza kutatua matatizo yao wenyewe na kuface reality!

Great sinker, hawa Theist loosers wanaishi bara gani ? Atheist gainer wewe unaishi wapi ? unatumia PC ama SIMU kuandika natumia hivyo hivyo, kwa akili yako pungufu unajidanganya kwamba hizi ni product za Atheist, hata kukiita kichaa nitakuwa nakupendelea...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…