Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,167
- 5,613
Nimeifuatilia kwa Muda kiasi nyuzi hii https://www.jamiiforums.com/jamii-i...-maswali-haya-ili-nikubaliane-na-kiranga.html ambayo imekutanisha watu wa aina mbalimbali. Kwa kuwa nina ufahamu kiasi fulani ningependa kuanzisha mjadala huu tena. Swali unaloweza kujiuliza ni kwa nini nianzishe mjadala mpya? Majibu ni kama ifuatavyo
Moja, mjadala husika una mambo anuai ambayo mwandishi wake anataka majibu na ni kutoka kwa mtu fulani (Kiranga). Pili ni mjadala mbao ni "too general" yaani "kuhusu Mungu". Kama nitakavyoaiisha baadae hili linafanya mjadala uwe mgumu kama unavyoonekana na usifikie tamati. Lakini mwisho pia binafsi sijaona swali maalum au lengo ambalo likipata majibu mjadala unafika ukingoni.
a. Ufafanuzi
Kabla sijaweka pwenti zangu ningependa kuweka msingi wa tunachokijadili hapa na mipaka yake. Suala la Mungu ni pana sana na hata vitabu vyote havitoshi kujadili, kwa hiyo kwa nafasi fnyu kama forum, tunahitaji kuweka mipaka.
Kwanza ninaposema Mungu ninaongelea "Mungu kama anavyoelezwa ndani ya Biblia". Hapa hatutazungumzia (ktk mada hii) kuhusu Biblia, ila Mungu wa Biblia. Usiniulize kuhusu imani nyingine maana mimi nakubali Mungu wa Biblia na ninaweza kukujibu kuhusu Mungu kama inavyoeleza Biblia. Kwa habari ya imani nyingine, subiri wafungue uzi au fungua kuwauliza watakujibu vizuri tu (ninaamini hivyo).
Pili ninaposema asiyeamini nina maana yeyote asiyekubali kuwa Mungu kama Biblia inavyomsema aliumba Ulimwengu wote, Mbingu na Nchi (Universe) ikiwajumuisha "atheists" na "agnostics". Hawa wawili ni walengwa wakuu ingawa sio pekee wa uzi huu.
Tatu ninaposema sayansi nina maana ya sayansi iliyotuletea ndege, Tv, upasuaji, n.k. Hii ni ile sayansi inayofuata hatua tano za kisayansi (Identification of problem, Hypothesis formulation, Experimentation, Observation, Data analysis Conclusion).
b. Ninachotaka kufikia katika Uzi Huu
Ninachotaka kuonesha katika uzi huu ni kuwa watu hawa wasioamini katika Mungu wa biblia wako hawawezi kupinga uwepo wake kwa kutumia mantiki (logic) ingawa hujificha sana nyuma ya logic. Sababu nitazitoa hapo chini. Ultimately watu hawa hukataa uwepo wa Mungu wa biblia kwa kuwa IMANI yao haiwaruhusu kukubali na si kwa sababu za kisayansi au kimantiki. Kusisitiza tu ninachotaka kuonesha ni kuwa watu hawa wana Imani, kama ambavyo wakristo wana imani. Tatizo lao ni kuwa kwanza wanakataa kuwa "Mungu hayupo" ni tamko la imani ya dini yao na kuwa wanaliamini pasipo sababu za kimantiki au kisayansi bali kiimani. Imani ya Wakristo ni juu ya Mungu wa biblia lakini wao imani yao ni imani upofu na haina pa kuegemea. Ni imani katika utupu (void faith/faith in nothing). "Argument" zao ni matamko ya imani kwa kiasi kikubwa.
Kifupi katika uzi huu nimelenga kuonesha kuwa:
c. "Arguments" zangu Kinyume nao
1. Ndugu zangu hawa hawaamini kama Mungu yupo wakisema kuwa hakuna ushahidi wa kuonesha uwepo wake. Na wanafikia hitimisho kuwa kwa sababu hii (kuwa hakuna ushahidi) Mungu hayupo na hivyo wote wanasema yupo wanasema kwa imani tu. Tukibadili juu-chini na kuwadai ushahidi thabiti (absolute evidence) ya kuthibitisha hakuna Mungu, hawana. Kwa kufuata mantiki yao wenyewe wao pia wanaamini kuwa hakuna Mungu...ni tamko la Imani
2. Watu hawa wanaamini kuwa kuamini Mungu yupo ni kukosa mantiki, na ni jambo la kiimani lililo kinyume na sayasi kabisa na hazivumiliki kwa yeyote aliye na akili ya kufikiri. Lakini watu hawa hawa wenye akili za kufikiri baadhi yao wanaamini kuwa ghafula kulikuwa na mpasuko, utupu (nothing) ulipasuka na katika mpasuko huu tunapata mpangilio wa sayari na jua, na wanadamu na mito na maziwa.
Watu hawa wengine wao huamini kuwa mercedes benz ilitengenezwa kiwandani na haikutokea tu, lakini watu hawahawa ambao tungetarajia watumie mantiki na fikra za juu sana wanaamini mwanadamu na wanyama wote wenye mifumo tata kuliko mercedes benz aina yeyote ile walitokea kwa bahati tu. Hii ni kinyume na mantiki na sayansi. Kwa nini watu hawa wanaamini mambo haya? Je ni wajinga wasioweza kufikiri? Si kweli kabisa...Tamko la dini yao, "hakuna Mungu" linawazuia wasikubaliane na ukweli na hivyo hawaruhusiwi na dini yao kutoka nje ya fundisho lao (doctrine of no God).
3. Watu hawa ambao wengine wanadiriki kusema "Mungu hayupo, na shetani ni hadithi" wanaamini kuwa hata kesho akiruka na ndege itatua chini na kuwa akipanda juu ya mwembe atashuka tu. hafikirii katika ulimwengu ambapo hakuna Mungu (the central coordinator) hakuna ulandano (uniformity). Kwa nini kuwe na ulandano katika dunia ambayo vitu vyaenda bila mpangilio (random/chance)? Kama kuna siku kulikuwa hakuna kitu ghafla bila mtu kusababisha vitu vikatokea kwa nini asiwe na shaka kuwa kuna siku ndege inaweza kwenda isirudi? Nani anayefanya vitu hivi viendelee hivi hivi? Watu hawa wanaongelea sheria za uvutano, mwendokasi n.k. bila kutuambia mtunga hizo sheria ni nani? Wanaamini zilitokea tu bila kutungwa. Je watu hawa wana ufahamu mfinyu sana kuweza kuelewa kukataa uwepo wa Mungu ni upuuzi unaopingana na mantiki na hata sayansi? Hapana...wanajua sana ila fundisho la dini yao ni kuwa hawaruhusiwi kukubali "Mungu yupo", kwa gharama yeyote!
4. Watu hawa wasioamini Mungu yupo huamini kuwa kama Mungu angaikuwepo kusingelikuwa na magonjwa na maumivu haya yote. Hawa watu wanaamini kuwa magonjwa ni kitu kibaya, na hata maumivu. Lakini swali wanaloliruka ni kuwa ili utofautishe kati ya mazuri na mabaya lazima kuwe na sheria iliyo juu ya wanadamu wote (absolute law) iliyo juu ya wanadamu wote. viginevyo bay kwa huyu laweza lisiwe baya kwa yule. Na ili kuwepo na sheria hiyo lazima awepo mtunga sheria aliye juu ya wanadamu wote. Watu hawa wanamkataa mtunga sheria huyu (Mungu) na hivyo wanapoteza sheria yenyewe na kimantiki mambo yote yanapaswa kuwa na hali sawa (hakuna baya au zuri). sasa wanpolalamika juu ya magonjwa na matatizo wanapimaje ubaya na uzuri? Je watu hawa hawawezi kuwaza haya yote? Je ni wajinga? Hapana, ni werevu sana. Ila tamko la dini yao linadai "Mungu hayupo" na wao kukiri kinyume na hivyo ni kuikana imani yao. Wanaenda kidini zaidi na sio kisayansi wala kimantiki!
5. Nimalizie kwa sasa (japo nina mengi bado) kusema kuwa watu hawa wanadai hawaamini uwepo wa Mungu wa kuwa Yeye haonekani, wala si wa ulimwengu huu wa damu na nyama (immaterial being). Wanadai hakuna kitu zaidi ya ulimwengu huu (nothing exist beyond material world). watu hawa wanatumia mantiki kuonesha kuwa kuamini vinginevyo ni kuvunja sheria za mantiki. lakini wanasahau kuwa sheria haijitungi na kwa sheria kuwa juu a wanadamu wote (absolute to all humans) lazima itoke kwa mamlaka juu ya wanadamu kwa namna ambayo wanadamu hawawezi kuivunja bila kuwa tasked kama ilivyo kwa sheria za mantiki. lakini pili watu hawa na dai lao hili wanajisahaulisha kuwa sheria ya mantiki haionekani wala sio ya ulimwengu wa damu na nyama (Logic laws are immaterial and invisible/intangible). Watu hawa kutumia mantiki kuipinga mantiki hawaoni ni kinyume na mantiki? Je watu hawa ni wajinga kiasi hiki? La Hasha! Ila dini yao haiwaruhusu kukubali uwepo wa Mungu wala ulimwengu mwingine tofauti na "material world".
d. Kwa Nini naamin Mungu Yupo?
1. Naamini kuna Mungu kwa kuwa naona uumbaji. DNA inabeba taarifa nyingi kuliko pengine vitabu vyote ulivyowahi kusoma tangu uzaliwe hata leo. Itakuwa ni upumbavu kuamini vitabu hivyo vilijiandika vyenyewe au kuwa post hii unayoisoma haikuandika na yeyote bali ilijitokeza bahati mbaya. Je si zaidi kuamini kuwa DNA ilijifanya yenyewe na mifumo yake tata ya kurekebisha makosa?
Ninaona Jua mwezi na mifumo ya jua jinsi inavyofanya kazi kwa ustadi na naungana na Daudi Mfalme kumtukuza Mungu nikikubali kuwa "Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake"(Zaburi 19). Kwa kweli siwezi kusoma sayansi ya anga na nisione mkono wa Mungu stadi na mwenye Nguvu ukiyatenda hayo. Sioni ni kwa namna gani haya yote yanaweza tokea bila Mungu na kwangu mimi Mungu ndio jibu linaloleta mantiki na linakubalika kisayansi!
2. Naamini Mungu yupo kwa kuwa hata uwepo wa sayansi unadai Mungu awepo kwanza. Sayansi inategemea ulandano i.e Uniformity (kuwa ukifanya vipimo chini ya "condition" zilezile majibu yanapaswa kuwa yaleyale). Tunajua kuwa ili kuwe na ulandano tunahitaji kuwe na Mtu au sheria (itakayodai mtunga sheria) ya kuvifanya vikae vilivyo. Kama hakuna Mungu hakuna haja ya ulandano kuwepo bali vitu vilipaswa kuwa shaghala bhagala. inachoona ni ulandano wa hali ya juu unaoiwezesha sayansi iwepo. Hivyo huwezi sema sayansi ukamtoa Mungu. Mungu ndiye anayefanya sayansi iwezekane. Hakika naungana na mwandishi wa Waraka kwa Waebrania kuwa Mungu "akivichukua [upholding] vyote kwa amri ya uweza wake" (waebrania 1:3). Bila Mungu hakuna sayansi na bila sayansi hakuna ndege, kompyuta n,k. Kwa kuwa vyote hivi vipo, Mungu yupo pasi na shaka.
3. Ninaamini Mungu yupo kwa kuwa maumivu na mateso, na mabaya yote yanadai uwepo wake. Mungu ndiye anayeweka kiwang cha nini ni kibaya na nini ni chema. Tunajua mema na mabaya kwa kuwa tumeumbwa kwa mfano wake ajuaye mema na mabaya. Tunafikiri kwa mantiki kwa kuwa tuna sura fulani ya Yeye Mungu Muumba. Hatukuumbwa tukiwa sokwe tukabadilika bali wanadamu wenye utashi ili tutawale viumbe wengine. Kila nikiangali jinsi mwanadamu anavyotawala viumbe wengi, anavyowafunga simba kwenye "cage" au anavyowadaka mamba kwa mitego yake sina cha kusema ila kukubaliana na Musa kuwa Mungu alituumba kwa mfao wake tutawale uumbaji wake (Mwanzo 1:26-27)
4. Mwisho, Ninaamini Mungu yuo kwa kuwa Mungu mwenyewe alitembelea sayari yetu akiuchukua mwili kama wetu katika utu wa Yesu Mnazarethi, akaishi katikati yetu akijithibitisha kwa nama ambayo kila atakaye kuujua ukweli atajua, akafanyiwa ukatili na watu ambao hawakutaka kukiri kuwa Mungu amewatembelea wakidai ni mwanadamu tu wa kawaida, akauawa kifo cha aibu na viumbe wake. Katika kufa kwake akalipa gharama ya mwanadamu kuifikia ile mbingu ambayo maumivu na mabaya ambayo yaliingia kwa sababu ya uasi wa mwanadamu hayatakuwepo. Je nihitaji nini tena kuamini kuwa Mungu yupo zaidi ya hili? Si tu kwamba alitutembelea, na si kwamba tu alifanya mambo yaliyomtenga na wanadamu wengine (kurudisha uhai, kufufuka toka wafu n.k) bali alikufa ili mimi siku moja niione mbingu...what a proof!
e. Hitimisho
Kwa kumalizia ni kuwa, imani katika Mungu ni imani sahihi inayokubaliana na sayansi, mantiki na hata akili ya kawaida. Imani katika dini ya "hakuna Mungu" ni imani potofu na ya kiupofu amabayo inapingana na kila aina ya ufahamu (sayansi) na mantiki na hata akili ya kawaida tu....
Wanaosema hakuna Mungu ni dini yao na sio kwamba ni kweli hakuna Mungu....usidanganywe!
Peace,
S.
[UPDATED] My Final Words after good debate
Kila mjadala huwa una mwisho wake, na kwangu mimi naona inatosha. Lengo langu limetimia kwa asilimia zote.
Ya kuwa Wasioamini uwwepo wa Mungu wanafanya hivyo kwa sababu za kiimani na sio kisayansi au kimatiki. Ya kuwa Imani katika Mungu wa Biblia ndio pekee "reasonable" na kuwa wakana Mungu na dini yao sio tu wako kinyume na sayansi, bali pia wako kinyume na Mantiki na hata fikra za kawaida.
Lengo limetimia kwa kuwa waliokuwa wakisombwa na mafundisho ya dini hii potofu ya Hakuna Mungu hata wakadhani ndio sayansi wameujua ukweli kuwa ni dini ambayo inapingana na sayansi na mantiki. Kipekee niwashukuru wote mliosoma na mliochangia, hasa Kiranga na wafuasi wote wa dini hii kongwe kabisa kwa kunisaidia kuthibitisha madai yangu pasipo na shaka. pia niwashukuru wote mliojadili kwa kuheshimiana na kwa staha.
Sijafunga mjadala huu (utaendelea kuwepo mpaka utakapoacha kuwepo) lakini kwa kuwa kusudi langu limetimia ninatundika daluga. Nitakuwa nikipita na pengine kujibu hapa na pale lakini sio kwa kiasi cha kwanza. Kama kuna boiling issue nai miss, fanya wema kuni mention
Kwa mnaoamini Mungu wa biblia, imani yenu ni solid and reasonable, ishikilieni. Kwa msioamini Mungu naomba niwaache na zawadi hii hapa chini.
Mungu awabariki na mjadala uendelee

- Wakristo na wasioamini Mungu wa biblia wote wanafanya haya kwa imani
- Imani katika Mungu wa Biblia ni "sound and solid" na inakubaliana na sayansi asilimia zote
- Imani ya hawa wandugu ni ya upofu, inayopingana na sayansi na mantiki kwa namna zote

For the wrath of God is revealed from heaven against all ungodliness and unrighteousness of men, who hold the truth in unrighteousness; Because that which may be known of God is manifest in them; for God hath shewed it unto them. For the invisible things of him from the creation of the world are clearly seen, being understood by the things that are made, even his eternal power and Godhead; so that they are without excuse:
Because that, when they knew God, they glorified him not as God, neither were thankful; but became vain in their imaginations, and their foolish heart was darkened. Professing themselves to be wise, they became fools....Who changed the truth of God into a lie, and worshipped and served the creature more than the Creator, who is blessed for ever. Amen... And even as they did not like to retain God in their knowledge, God gave them over to a reprobate mind, to do those things which are not convenient...haters of God (Romans 1)
Mungu awabariki na mjadala uendelee