Ok,
First thing first,unakubali kuwa binadamu aliumbwa ili tuanze safari nyingie ya kutafiti kama aliyemuumba binadamu nae kaumbwa?
Sikubali,
Ila katika kuonesha kwamba habari ya "binadamu ni lazima kaumbwa" haiko logical, natumia "immanent criticism".
Kwa kuwa nikisema "binadamu hajaumbwa" na wewe ukisema "binadamu kaumbwa" kutakuwa na stalemate, hatutafika popote.
Kwa hiyo nakubali "for the sake of argument" kusema "let's say binadamu kaumbwa kwa sababu kitu complex kama binadamu hakiwezi kutokea bila kuumbwa".
Key words are "suppose" "let's say".
Mtu anayesema "suppose" au "let's say" hajakubali. Huyu ni mtu anayekubali kufanya thought experiment na/au immanent critique.
Sasa ndio tunaendelea kutoka hapo.
Suppose complexity ni lazima iwe imeumbwa, haiwezi kutokea yenyewe.
If follows kwamba, as long as complexity ni lazima iumbwe, complexity ndogo haiwezi kuumbwa na complexity ndogo.
Kwa hiyo complexity ndogo ni lazima iumbwe na complexity kubwa.
Lakini tushaona kwamba complexity lazima iumbwe.
Kwa hiyo tukishasema tu kwamba "mwanadamu kaumbwa na mungu", tunaona kwamba mungu ni complex kuliko mwanadamu.
Kwa hiyo, sheria ile ile iliyotufanya tufikiri kwamba mwanadamu kaumbwa (kwa sababu yuko complex) itatutaka tufikiri kwamba mungu naye kaumbwa.
Kwa sababu uwezi kusema kwamba ni lazima complexity ndogo iwe imeumbwa, lakini complexity kubwa iweze kutokea bila kumbwa.
Huwezi kusema kiti ni lazima kiwe kimeumbwa, halafu ukasema Jumbo Jet linaweza kutokea tu.
Huwezi kusema binadamu ni lazima awe ameumbwa, halafu mungu hajaumbwa.
Kwa sababu sheria ile ile iliyokufanya uone binadamu ni lazima awe ameumbwa (kwa sababu ni complex) zitakutaka ulazimike kufikiri kwamba mungu naye ni lazima awe ameumbwa, tena haja ya mungu kuumbwa inakuwa kubwa zaidi.
Kwa sababu kama complexity ni lazima iumbwe, complexity kubwa zaidi ni lazima zaidi iwe imeumbwa.
The argument from design falls on its face due io it's logical absurdity.
Kwa sababu mungu atahitaji muumbaji wake, na muumbaji wake atahitaji muumbaji wake, ad infinitum, ad absurdum.