Yaani mwanamke anayekwambia anakupenda hata kama hauna hela, huyo muogope sana.
Kwa kawaida kama kwako kunaungua, basi kwa mwenzio kunateketea.
Kwenye maisha tunahitaji pesa kusavaivu, kama mwanamke wako anakwambia anakupenda hata kama hauna hela, huyo muogope kama ukome.
Wewe hauna hela, ila yeye matatizo yake bora matatizo yako wewe, siku akija kwako ndipo utajua kumbe hukujua vizuri kumhusu.
Mimi mwanamke anayeniambia ananipenda hata kama sina hela, najiweka mbali sana na yeye.
Maana hiyo ni dalili ya kukubali ufukara.
Inatakiwa mwanamke akupende ukiwa na hela,
tofauti na hapo ni matatizo unatengeneza.