Muonekano mpya wa Beyonce wazua tafrani, bado ana vigezo vya kujiita "black woman" ?

Muonekano mpya wa Beyonce wazua tafrani, bado ana vigezo vya kujiita "black woman" ?

Nakaa Afrika ndugu yangu.
Sojahamisha mada wewe ndiye una uwezo mdogo wa kuelewa.

Marekani mtu kuwa "Mtu Mweusi" haina uhusiano na rangi ya ngozi.

Unaweza kuona mtu anaonekana mweupe kama mzungu lakini ni mtu mweusi.

Nimekuwekea mpaka picha hapo ya mtu anayeonekana mweupe lakini ni mweusi.

Huelewi wapi?

Hiyo dhana nzima ya race ni ya kutungwa kuungwaungwa na watu tu.

Ndiyo maana kila sehemu watu wanajipangia wenyewe nani mtu mweusi na nani si mtu mweusi, Waaarabu Marekani wanabadilishwa mara wawekwe kwenye watu weupe mara watolewe.

Unaelewa hilo?

Unakaa nchi gani mkuu?
 
Si umekataa kuhusu race, wr unaelezea kuhusu marekan na sio Afrika na mi nilikueleza kuhusu Afrika.

Nipo Tanzania.
Naam.

Haya mambo mengine ukikaa nchi isiyo na diversity ya watu mbalimbali si rahisi kuyasikia na kuyaelewa vizuri.

Mfano Tanzania ni nchi ambayo haina diversity kubwa ya watu, watu wengi ni Wabantu.

Maongezi ya race, ethnicity, colour, hayafanyiki sana kama nchi za South Africa, Brazil au Marekani, nchi ambazo wame deal na matatizo haya kwa muda mrefu sana.

Ndiyo maana nilianza kueleza habari kwamba Marekani kuwa mtu mweusi si rangi ya ngozi, au nilisema suala zima la race ni hadithi ya kuungwaungwa na watu tu, inakuwa vigumu kuelewana.

Huishi katika nchi yenye matatizo haya kwa sana, na hivyo, hukutani nayo sana, hujayasoma sana na kuyaelewa.
 
Naam.

Haya mambo mengine ukikaa nchi isiyo na diversity ya watu mbalimbali si rahisi kuyasikia na kuyaelewa vizuri.

Mfano Tanzania ni nchi ambayo haina diversity kubwa ya watu, watu wengi ni Wabantu.

Maongezi ya race, ethnicity, colour, hayafanyiki sana kama nchi za South Africa, Brazil au Marekani, nchi ambazo wame deal na matatizo haya kwa muda mrefu sana.

Ndiyo maana nilianza kueleza habari kwamba Marekani kuwa mtu mweusi si rangi ya ngozi, au nikisema suala zima la race ni hadithi ya kuungwaungwa na watu tu, inakuwa vigumu kuelewana.

Huishi katika nchi yenye matatizo haya kwa sana, na hivyo, hukutani nayo sana, hujayasoma sana na kuyaelewa.
Ulo sahihi mzee.
 
Taharuki hii ilianza baada ya binti mzungu anayeitwa Sweeney kuwekwa kwenye tangazo la American Eagle. Tangazo hilo limefanya vizuri sana kibiashara, lakini kwa upande mwingine, lilizua kilio kikali.

Marekani imegawanyika pande mbili chama cha Republicans, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Rais Trump, na chama cha Democrats, ambacho viongozi wake wa zamani ni pamoja na Obama na Biden (Kamala Harris alishindwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu).

Wafuasi wengi wa chama cha Democrats, hasa wale wa mrengo mkali, huwa na mtazamo kwamba karibu kila jambo la kijamii linapaswa kutazamwa kupitia rangi ya ngozi ya mtu. hata kazi wanatoa kwa kigezo cha rangi ya ngozi hata kama hawana sifa kamili.

Katika muktadha huo, waliona mafanikio ya tangazo hilo kama kuendeleza hadithi za eugenics, wazo la kwamba uzuri au ubora unahusishwa na sifa za mtu kuwa mzungu (kama ngozi nyeupe, macho ya kizungu, nywele za kizungu ).

View attachment 3435347

Ndani ya muda mchache kampuni ya nguo za Levis ikajibu kwa kumtumia black woman maarufu kwenye jamii ya wamarekani weusi, chaguo lilikuwa ni Beyonce lakini picha za tangazo zimezua gumzo, hana tofauti sana na mzungu, kajichubua ama kuweka make up awe mweupe kama mzungu, Nywele kazitia dawa na kuzistyle ziwe kama za mzungu,

Tangazo limebuma, hawaoni uzuri wa asili wa black woman, watu wanahoji ule uAfrika wake kwanini usingebaki kama alivyo, kwanini awe kama mzungu ?


View attachment 3435192

Hizi ni picha za Beyonce zikionesha ngozi yake ya asili

View attachment 3435196

View attachment 3435391
Beyonce ni light-skinned. Haina maana kwamba sio mtu mweusi.
 
Back
Top Bottom