Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Duh mimi si mpenzi wa bongo music hata kidogo lakini nimeumia sana kuona hiyo picha kwani mwaka Jana Chid Benz alifanya show Kakola Kahama akiwa na mwili wenye afya kabisa!! Sasa masikitiko yangu ni watu hapa jamii forum wanavyomtukuna maskini wa mungu anayeomba msaada hata wa kimawazo tu kwa Watanzania na wasamaria wema. Duh Watanzania roho mbaya hadi wengine wamegusia kuwa alikuwa anamtukana Lowassa!!! Mimi mwenyewe nilikuwa team lowassa na hadi leo namkubali mzee lkn chuki za kwenye siasa siwezi kuzileta kwa mtu anayehitaji msaada. Duh Tanzania nchi niliyoaminishwa ina watu wenye mioyo mizuri lkn kwa sasa hawana tofauti na Mazombi ya Shein Zanzibar. Chid Benzi nakuombea kwa mungu kuanzia leo katika kipindi hiki cha Kwaresma taweka sala maalumu kwa ajili yako. Nakupenda kama kaka na kama mwana mpotevu ambaye umekumbuka makosa yako na kurudi kuomba msamaha kwa Watanzania wakusaidie ila bahati mbaya wengi washakuwa kama kundi la ISIS kwa mioyo ya kishetani. Mungu aliyekuumba hatakuacha uteseke na hakuna lisilowezekana ukimtumaini mungu atakuponya.
Ni kweli mkuu kwenye maisha huwa kuna SECOND CHANCE.
 
Dah! Siku za Dar es salaam stand up haziwezi kurudi tena, huwa kuna nafasi moja Tu huwa inatokea, Chid yule anafanya show moja ya Kilimanjaro award then T.I Kama msanii mkubwa toka Marekani anaalikwa kwenye utoaji tuzo ule, wakati unafanya show ya nguvu kwa ngoma zako kali Naitwa nani! Babe ft Ray C, T.I ananukuliwa akiwauliza wenyeji wake alokaa nao.... "Huyu Ni nani?"...anaambiwa huyo Ni mwana Hip Hop anayekimbiza bongo, Na baadaye unashinda tuzo, T.I mwenyewe anakupatia tuzo, Na uhakika uliambiwa jinsi T.I alivyouliza kuhusu wewe, Leo kina Diamond wakipata nafasi Kama hizo wanazitumia hapo hapo, Ni vipi ungefanya ngoma Na T.I wakati ule, bila shaka ungekua mbali, all in all madawa yamekupoteza, sidhani Kama utapata msaada kwenye muziki wako tena, Sana Sana makosa yako wacha yatumike Kama funzo kwa vijana wengine, Na wenyewe wasipojifunza kwako! Wacha yawakute Tu, hatuna namna....sorry Chid Benz, fulsa huwa Ni Mara moja Tu!
Hiyo ni kweli kabisa mwangalie hata king kiba[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Dah wauza unga wanazidi kumaliza vijana.Chid amekua kama Amba rose!apelekwe rehab jamani.
 
Huwa napendaga kusema hivi na ntarudia kusema
Usimcheke au kumdharau mtu yoyote aliyekuwa ni muathirika wa utumiaji wa madawa!
Mtu yoyote unaweza kujikuta umeingiaa ktk mkumboo huko....wa kuitumia madawa
Ikitokea nafasi ya kumsaidia mtumiaji we msaidie....
Safi sana mkuu, ndiyo maneno ya utu uzima. Sio kuonekana we mjanja wakati mwenzako ana shida.
 
haya sasa FISIEM mkumbukeni msanii wenu maana mwanzo nilimkubal saaana ila kipind cha kampeni alitoa nyimbo ambayo alimtukana sana LOWASA tena matus ya nguoni na akatutus na UKAWA KIUKWELI NILICHUKIA SANA TOKA SIKU HYO HAD LEO SIMFAGILII TENA NAFKIR KIAS FULAN ILE LAANA ALIYOJIPALIA YA KUMTUKANA KIONGOZ WANGU NAYO IMECHANGIA
We nae fala kweli. wakat wa kampeni alikuwa tayar na hali hiyo. laana gani sasa? kwanza LEMA kasema ni heshima kubwa kwa Mungu kumtukana FISADI.
 
We are the authors of our own destiny and King Kong wrote a lot
 
Simlaumu Chid, nailaumu Nchi yetu kushindwa kuzuia madawa haya mipakani kwetu.

Baadhi ya watu wanaofanya biashara hiyo pia wanatuharibia nguvu kazi ya taifa
 
Unga ni noma wengine wanasema eti ukila vizuri haukudhuru, mara ooh Kuna first class sijui. Jiulize je Maradona, Whitney Houston, Brenda Fassie walikuwa wanakula dagaa na tembele?
 
Mola anusuru kizazi chetu! Akina Ray C wanaweza kumsaidia Mwenzao kama walivyosaidiwa wao. Tujaribu kuvaa Ubinadamu fanya Chid ni sehemu ya Familia yako
 
Kama sikosei alimpigia kampeni Mr Magu.Akale alikopeleka Mboga.
 
Back
Top Bottom