Dah! Siku za Dar es salaam stand up haziwezi kurudi tena, huwa kuna nafasi moja Tu huwa inatokea, Chid yule anafanya show moja ya Kilimanjaro award then T.I Kama msanii mkubwa toka Marekani anaalikwa kwenye utoaji tuzo ule, wakati unafanya show ya nguvu kwa ngoma zako kali Naitwa nani! Babe ft Ray C, T.I ananukuliwa akiwauliza wenyeji wake alokaa nao.... "Huyu Ni nani?"...anaambiwa huyo Ni mwana Hip Hop anayekimbiza bongo, Na baadaye unashinda tuzo, T.I mwenyewe anakupatia tuzo, Na uhakika uliambiwa jinsi T.I alivyouliza kuhusu wewe, Leo kina Diamond wakipata nafasi Kama hizo wanazitumia hapo hapo, Ni vipi ungefanya ngoma Na T.I wakati ule, bila shaka ungekua mbali, all in all madawa yamekupoteza, sidhani Kama utapata msaada kwenye muziki wako tena, Sana Sana makosa yako wacha yatumike Kama funzo kwa vijana wengine, Na wenyewe wasipojifunza kwako! Wacha yawakute Tu, hatuna namna....sorry Chid Benz, fulsa huwa Ni Mara moja Tu!