Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Muonekano mpya wa Chidi Benz baada ya kutumia unga

Duh mimi si mpenzi wa bongo music hata kidogo lakini nimeumia sana kuona hiyo picha kwani mwaka Jana Chid Benz alifanya show Kakola Kahama akiwa na mwili wenye afya kabisa!! Sasa masikitiko yangu ni watu hapa jamii forum wanavyomtukuna maskini wa mungu anayeomba msaada hata wa kimawazo tu kwa Watanzania na wasamaria wema. Duh Watanzania roho mbaya hadi wengine wamegusia kuwa alikuwa anamtukana Lowassa!!! Mimi mwenyewe nilikuwa team lowassa na hadi leo namkubali mzee lkn chuki za kwenye siasa siwezi kuzileta kwa mtu anayehitaji msaada. Duh Tanzania nchi niliyoaminishwa ina watu wenye mioyo mizuri lkn kwa sasa hawana tofauti na Mazombi ya Shein Zanzibar. Chid Benzi nakuombea kwa mungu kuanzia leo katika kipindi hiki cha Kwaresma taweka sala maalumu kwa ajili yako. Nakupenda kama kaka na kama mwana mpotevu ambaye umekumbuka makosa yako na kurudi kuomba msamaha kwa Watanzania wakusaidie ila bahati mbaya wengi washakuwa kama kundi la ISIS kwa mioyo ya kishetani. Mungu aliyekuumba hatakuacha uteseke na hakuna lisilowezekana ukimtumaini mungu atakuponya.
Mkuu huyu ni unga ndiyo umemfanya hvy sasa unataka aombewe ili iweje?teja hiyo ndiyo malipo yake acha apotee tu!
 
Binadamu bwana

Ukiwa na mafanikio makubwa watakuonea wivu, wataponda sana mara unajiona sana, limbukeni, freemason, huna lolote etc.

Ukifeli kimaisha na hali mbaya ambapo unahitaji msaada hawakusaidii ila unabaki kuwa kicheko na topic kubwa mitandaoni

Ukifa ndio wanajifanya ooooh marehemu hata jana tumewasiliana nilikuwa ninampango wa kumrudisha kwenye game, michango kibao kusherekea mazishi, machozi ya kinafki, rip za kumwaga mitandaoni na nyimbo zako kupigwa 24hrs hiyo wiki
 
Mnaohusisha tatizo lake na HIV mnakosea sana,
Tatizo hamjawahi muona m bwia unga anakuaje, anakula nini, anaishije,
Unga ni mbaya sana kuliko hata huo ugonjwa mnaousema,

Mnamkumbuka Kelvin wa HOME ALONE?
Nenda kamuangalie alivyo.

Mwngn anauliza mbona Ray C kanenepa, seriously!!
Ray c alikuaje kabla hajaanza kupata matibabu?

Sisi vijana tukiamua tunaweza fanya jambo la kuwakwamua vijana wenzetu juu ya matumizi haya ya madawa,
Kuliko kuwabeza na kuwadharau.

Naamini kwa kua wameshindwa kudhibitiwa hao wauzaji wakubwa,
Tunaweza kuwadhibiti hawa watumiaji, wakikataa kutumia basi hao wauzaji watashindwa kuuza.

Huo ni mtazamo wangu tu mdogo.
 
Aliwahi kukiri Carlos santana kwenye wimbo wake "Black magic woman" alielezea kwa masikitiko the way madawa yalivyomwingiza kwenye njia mbaya ya maisha isio na mwelekeo alilalamika saana kwenye nyimbo ile.. inasikitisha saana.

Its a must listen song kwa wote addicted and non-addicted.
 
Jamaa aliijua saana sanaa ya muziki maana alitumia lugha ya picha kuyazungumzia madawa ya kulevya kama mwanamke mzuri ambae ndie huyo Black magic woman ambae jamaa anampenda na ameshindwa kabisa kumuacha sababu kamroga jamaa.

Ila kama unavyojua warahibu wengi wa madawa ya kulevya wengi huwa hawataki kukubali kwamba madawa yameathiri maisha yao, that's why hata Santana alitoa wimbo huu ya 80's na watu wakajua ni ishu ya mapenzi kumbe malalamiko juu ya kushindwa kuchomoka kwenye urahibu wa madawa ya kulevya.

#saynotodrugs.
 
Huu sio unga peke yake...nina wasiwasi na kale kaugonjwa kame muingia..Luna mateja wengi tunawajua hawajakongoroka kama huyo jamaa
 
kwasasa chidi benz hamkuti dogo janja kwa afya,asaidiwe na nani badala ya kujisaidia mwenyewe kwanza kuacha upuuzi.
niliwahi kuwa mvutaji mzuri wa sigara,nikapata kansa ya mapafu nikatibiwa nikapona.daktari siku ananiaga alisisitiza kunywa pombe moshi achana nao.mpaka leo niko poa kwani kweli sijagusa.
Nilikua namkubali sana chid kwa rap zake kwakweli angeendelea angefika mbali sana.nafkiri Nay kidogo anafuatia lakini kwa Chid yuleeee Nay bado sana.
Nay ni msanii wa rap?... Me najua anaimba MIPASHO.
 
Hii hapa mistari ya wimbo wa Carlos Santana akilalamika juu ya Black magic woman ambae alimsawiri kama mwanamke mrembo aliemroga Santana kizungu na anaempenda na hawezi kumwacha kamwe! kumbe maana yake ilikuwa ni madawa ya kulevya yamemkamata na hawezi kuyaacha kirahisi.

Moral of the story....madawa ukiyaanza na ukawa mrahibu kamwe!! huwezi kuyaacha kirahisi.
 

Attachments

  • 1458450172866.jpg
    1458450172866.jpg
    38.3 KB · Views: 62
Back
Top Bottom