Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baada ya kusikia watu wengi 'wakiumizwa' na 'kupigwa' wakiwa kwenye harakati za kutafuta usafiri uliotumika nchini, nimeona sio mbaya nikitoa ushauri ni jinsi gani unaweza kuepuka majanga kwenye zoezi hilo.
Naandika kama mnunuzi au muuzaji wa aina hio ya magari, kwahio siegemei upande wowote na ninachokiandika hapa sio sheria naweza kuwa sahihi au nisiwe sahihi ila ni imani yangu lipo litakalosaidia baadhi ya watu.
Njia muhimu za kufuata ili kupata gari unalotaka ni kama ifuatavyo:
1.Fanya utafiti mdogo juu ya gari unayoitaka: Uliza ujue gari unayoitaka inauzwa kiasi gani[makadirio]. Ukiweza kujua bei ya showroom au ukiagiza mwenyewe Japan halafu linganisha na bei utakayopewa hapa. Hili ni muhimu kwa sababu nimeshuhudia watu wananunua magari yaliyotumika Tanzania kwa bei ambayo ukiagiza mwenyewe unalipata kutoka japan au ukiongeza kidogo tu unapata la showroom.
2.Usiwe na haraka: Usiwe na haraka kabisa kwenye kutafuta gari. Utaletewa kila aina ya gari na usipokuwa makini utanunua gari bovu. Angalia taratibu angalau magari matano tofauti kwenye chaguo lako ndipo uamue, madalali watakusumbua ili mradi tu wapate cha juu.
3.Epuka madalali: Kama unaweza epuka madalali. Tafuta gari kwa kuuliza watu ulio karibu nao, ndugu jamaa na marafiki au unaofanya nao kazi au biashara. Hii ni nzuri chochote kikitokea una pa kuanzia. Madalali wengi hawajali maslahi yako wala ya muuzaji cha muhimu kwao ni cha juu tu. Gari ya 4m dalali atakuuzia 5-6m.
4.Tafuta Fundi: Ukilipenda gari lolote tafuta fundi akusaidie kulikagua,hata kama una idea na magari kuna vitu hutaviona ila fundi atakusaidia. Kuwa makini kuna mafundi huwa wanabonyezwa wakufiche hitilafu halafu baadae wanarudi kupewa chao ukishauziwa kanyaboya.
5.Epuka gari iliopigwa rangi: Epuka gari iliopigwa rangi siku chache kabla ya kuwekwa sokoni, wazoefu wanajua gari za aina hio ndio umuhimu wa fundi unapokuja. Gari inaweza kuwa imegongwa hivyo imenyooshwa na wanakuzuga kwa rangi inayong'aa. Siku hizi rangi hata 200,000 unapiga gari nzima ila ukinunua hilo baada ya mwezi rangi inababuka yote.
6.Epuka gari iliooshwa engine:Ukikagua gari ukiona imeoshwa engine ogopa sana. Mara nyingi gari zinaoshwa engine kuficha 'leakage',yaani oil na vitu vingine vinavyovuja kutoka sehemu mbalimbali za engine.
7.Jaribu gari wewe mwenyewe: Ni muhimu kuendesha na kuijaribu gari wewe mwenyewe hata ukienda na fundi. Ipitishe njia mbovu usikie jinsi ilivyo chini,chochote kinachogonga kuwa makini,usisikilize ukiambiwa ni tatizo dogo, kwanini hakurekebisha. Ingawa yapo matatizo madogomadogo ila kuwa makini.
8.Usiangalie Namba: Usibabaishwe na namba, eti hii C,D etc. Kuna gari namba A ziko vizuri kuliko namba C. Muhimu ni hali ya gari husika kwa muda huo.
9.Nenda TRA kujiridhisha: Ni muhimu kujua ukweli na status ya gari na mwenye gari. Jiridhishe anaekuuzia ndio mwenye gari. Akuonyeshe nyaraka zote halisi hata za kodi aliolipia.
10.Mwisho kabisa ukilipenda gari fanyeni makabidhiano kwa kuandikishana kwa mwanasheria. Ukiweza lipia benki na ubaki na risiti kama ushahidi wa malipo kupitia akaunti yake. Epuka kubeba cash kumpelekea muuzaji mahali alipo.
Haya machache naamini yanaweza kuwa msaada kwa watu wanaonunua magari yaliyotumika nchini,wengine mnaweza kuongezea mawili matatu na kurekebisha nilipokosea.
Umefufua thread mkuu!
mkuu huduma hii naweza kuipata wapi hususani kwa Dar es Salaam, wilaya ya TemekeGari zote uwa zinasehemu ya kuchomeka kifaa (OBDE) kujua code gani kama gari ina check engine or service engine soon inawaka.
Mtu anapouza gari anahakikisha warning za engine hazionyeshi. Kutoonyesha taa hakumaniishi gari haina tatitzo ni vile tu computer (PCM) inafidia penye tatizo.
Sasa sisi tunaonunua magari used engine mara nyingi tunaicheck ikiwa inawaka na kutumia code scanner kwa kuangalia LIVE DATA. parameter muhimu ni STFT1 na LTFT1 kwa gari za cylinder 4 na zenye 6 au 8 zinakuwa na mara mbili yani STFT2 and LTFT2. Kirefu chake ni SHORT TERM FUEL TRIM na LONG TERM FUEL TRIM.
Vipimo lazima viwe kati ya -5 mpaka 5 ingawa zinaweza kwena mpaka -10 na 10. Kama STFT1 iko kwenye limit yake lakini LTFT1 ni kubwa iko nje basi injini imeachia sehemu ya kuingiza hewa intake manifold, gari inaenda lakini mwanzoni italalamika kidogo.
Itakuwa vizuri ukichukua hiyo gari uipeleke garage waiweke kwenye computer au mtu mwenye code scaner ndogo tu ya elfu 70 utuwekee live data parameters tukwambie tatizo lipo au hamna gari haitakusumbua mbeleni.
ANGALIZO: mwenye gari anaweza kutoa betry au kufuta code kama engine warning light ilikuwa inaweza muda kidogo ununue. Kwa scanner za kawaida haziwezi kuona kama code ilifutwa scanner za bei zinaona ila ukiingia frame freeze itakupa idadi ya warnings kwa muda mchache uliopita baada ya kuclear au unaweza kuendesha maili 80 isipoonyesha warning zisiporudi basi fuata maelezo ya mwanzo ili usije nunue kitu baada ya wiki misfire zinaanza.
Karibu tuwasiliane kuhusu kuagiza magari japan, dubai na S.A.
Vilevile ukihitaji gari second hand ya Tanzania hapa
Katika mambo yote uliyoandika la kweli na la maana ni kutoangalia namba.
Kuhusu udalali nakutafuta gari kwa rafiki au unaefanyanae kazi ni kazi bure.
Sikuhizi kila myu ni dalali kila mahali hadi ikulu
Mkuu kweli kubeba hela ni nuksi, ila hata hii ya kumuwekea mtu hela kwenye account kabla hujakabidhiwa mzigo ni shida kuna kituko kilimtokea jamaa yangu wakasumbuana sana na muuzaji. Labla ungetueleza utaratibu mzuri wa kufanya malipo na mkabidhiano ili mwisho wa cku watu wasijeumia.
Safi sana hii itawasaidia wadau wasipigwe na wenye uchu wa fedha
Mkuu RRONDO hiyo dawa ni nzuri sana ile kuchoma choma haikuwa issue mgonjwa alikuwa anapewa mast cell stabilizer kama piriton au cetirizine mambo poa na maleria inaisha kabisa hapa Tanzania kila mwenye kutaka kuingiza dawa atatoa sababu ya kuiondoa sokoni dawa iliyopo. Mfano Uganda walikuwa wanatumia chloroquine ila kutokana na matumizi holela ya watu kumeza dawa bila kupima ikajenga resistance wakaiweka bench kwa muda then wakaweka mkakati kuwa dawa zote za maleria ni prescription only medicine yaani ili upate lazima upime na uwe na cheti cha daktari wakairudisha chloroquine sasa mambo poa sana.