MUONGOZO: Mambo ya kuzingatia unaponunua gari lililotumika ndani ya Tanzania



Imetulia mkuu
 
Umefufua thread mkuu!

Mkuu RRONDO huwa napenda sana thread zenye heshima na staha kama hii uliyoianzisha haina watu wenye jazba na upungufu wa ustaarabu.kifupi imejaa shule tosha hasa kwa sisi washabiki wa magari maana si kila mara utakuwa na nguvu ya kuagiza gari kutoka ng'ambo, na wakati mwingine unaweza kuvutiwa na gari lolote lile ambalo tayari linammiliki wake hapa bongo....sasa hatua gani salama uzifuate ili kuepuka ngeu na matatizo yanayoweza kuzuilika...humu tayari tushazipata shule bila ada..na mkuu Mshana jr hope mambo yake yakisimama kuna kitu atatueleza yapi yalimkuta.
Big up Brother RRONDO kwa good thinking.
 
ukiwa unakaa mkoani ndio raha zaidi kwani unavyosafiri nayo ndivyo hata unavyoipima uwezo wake barabarani..na uimara wa injini..magari ya kutoka Japan binafsi nimeyafurahia sana,naonaga kama vile gari mpya kabisa halafu wajapan wanakuwekea oil brand we ni kupitia sheli tu kuongeza wese then unachapalapa..siku nitayoendesha ile inasoma dashboard km 0 au 5 na seat zina manailoni kabisa,dah sijui nitainjoi kiasi gani...u feel that u real driving a car,mlio, muungurumo, acceleration - everything..dah
 
Huh uz safi. Ni saw a pia ukitaka

1. Kununua kiwanja
2. Kununua Laptop
3. Hata kuoa 'kupata jiko'

lazma ufate mengi ya mleta Uzi huu

Wakuu haya huu Uzi sio wa kuupitia juu juu. Inafaa tuurejelee kuusomasoma.

katika kuoa niliacha kuoa bint mmoja ni mzur na anamvuto wa ajabu. Utafiti mdogo tu umenisaidia.

Nilikwepa matatizo ktk ununuji wa kiwanja naamini nilijiepusha na sheeyda
 
Gari zote uwa zinasehemu ya kuchomeka kifaa (OBDE) kujua code gani kama gari ina check engine or service engine soon inawaka.

Mtu anapouza gari anahakikisha warning za engine hazionyeshi. Kutoonyesha taa hakumaniishi gari haina tatitzo ni vile tu computer (PCM) inafidia penye tatizo.

Sasa sisi tunaonunua magari used engine mara nyingi tunaicheck ikiwa inawaka na kutumia code scanner kwa kuangalia LIVE DATA. parameter muhimu ni STFT1 na LTFT1 kwa gari za cylinder 4 na zenye 6 au 8 zinakuwa na mara mbili yani STFT2 and LTFT2. Kirefu chake ni SHORT TERM FUEL TRIM na LONG TERM FUEL TRIM.

Vipimo lazima viwe kati ya -5 mpaka 5 ingawa zinaweza kwena mpaka -10 na 10. Kama STFT1 iko kwenye limit yake lakini LTFT1 ni kubwa iko nje basi injini imeachia sehemu ya kuingiza hewa intake manifold, gari inaenda lakini mwanzoni italalamika kidogo.

Itakuwa vizuri ukichukua hiyo gari uipeleke garage waiweke kwenye computer au mtu mwenye code scaner ndogo tu ya elfu 70 utuwekee live data parameters tukwambie tatizo lipo au hamna gari haitakusumbua mbeleni.

ANGALIZO: mwenye gari anaweza kutoa betry au kufuta code kama engine warning light ilikuwa inaweza muda kidogo ununue. Kwa scanner za kawaida haziwezi kuona kama code ilifutwa scanner za bei zinaona ila ukiingia frame freeze itakupa idadi ya warnings kwa muda mchache uliopita baada ya kuclear au unaweza kuendesha maili 80 isipoonyesha warning zisiporudi basi fuata maelezo ya mwanzo ili usije nunue kitu baada ya wiki misfire zinaanza.
 
mkuu huduma hii naweza kuipata wapi hususani kwa Dar es Salaam, wilaya ya Temeke
 
Katika mambo yote uliyoandika la kweli na la maana ni kutoangalia namba.
Kuhusu udalali nakutafuta gari kwa rafiki au unaefanyanae kazi ni kazi bure.
Sikuhizi kila myu ni dalali kila mahali hadi ikulu

Ni kweli kabisa siku hizi hata ndugu yako wa damu akikutafutia kitu lazima aweke udalali apate cha juu nothing goes for nothing
 

Utaratibu mzuri mnaandikishiana kwanza mkataba wa mauziano alafu mnunuzi akisha deposit hela bank mwenye gari anakabidhi gari na kuhakikisha mzigo umeingia bank pamoja na slip na mnunuzi anachukua gari,mkataba wake na copy ya deposit slip hapo kila upande utakuwa salama ,done deal
 
Safi sana hii itawasaidia wadau wasipigwe na wenye uchu wa fedha

mkuu Chloroquine hio dawa siisahau! nilikuwa sipendi kabisa sindano sasa nikikamatwa na malaria sina namna ila kunywa hio dawa....ni chungu balaa sasa kasheshe malaria ikianza kuisha unaanza kuchomwachomwa sehemu mbali mbali mwilini randomly unawza kusikia umechomwa unyayoni halafu ghafla unachomwa mgongoni mara kwenye korodani! yaani ni tabu tupu!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu RRONDO hiyo dawa ni nzuri sana ile kuchoma choma haikuwa issue mgonjwa alikuwa anapewa mast cell stabilizer kama piriton au cetirizine mambo poa na maleria inaisha kabisa hapa Tanzania kila mwenye kutaka kuingiza dawa atatoa sababu ya kuiondoa sokoni dawa iliyopo. Mfano Uganda walikuwa wanatumia chloroquine ila kutokana na matumizi holela ya watu kumeza dawa bila kupima ikajenga resistance wakaiweka bench kwa muda then wakaweka mkakati kuwa dawa zote za maleria ni prescription only medicine yaani ili upate lazima upime na uwe na cheti cha daktari wakairudisha chloroquine sasa mambo poa sana.
 

chloroquine bado ipo hapa tz?? watu wanatumia?
 
Hizo dawa hazipo kwenye essential drug list ya Tanzania hivyo watu wanazipata nchi jirani hasa Uganda kwa kuwa wao bado wanatumia. ukizihitaji zinapatikana kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…