Museveni anaeonekana kuifahamu sana Tanzania, hii sio hatari kwa usalama?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?
 
Binafsi mi nimekuwa na mashaka haya kuhusu mifumo yetu ya ulinzi! Mikoa iliyopo mipakan kuna watu weng mno toka nchi jiran wanafanya kazi hasa vibarua,biashara as if ni watz! Unaweza ukafika holili , jipe ,tarakea au toloha ukakuta duka la raia wa kenya na mamlaka zipo kimya tu! Ukija huku kwimba wapo waganda,wakenya na wanyarandwa kibao wananunua na kuuza mpunga as if ni wasukuma! Sasa huwez jua majasusi wapo wangap humo kwenye hayo makundi! Sio ajabu ukakuta kagame ana taarifa zote za gesi ya mtwara, chuma cha liganga nk! Si alituma kikosi kupambana na ugaid msumbiji!?
 
Wamarekani waliposhinda Iraq maana yake waliijua Iraq na makabila yake?
 
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?
We hujui kuwa kasoma UDSM, na kukulia Moshi?
 
Binafsi mi nimekuwa na mashaka haya kuhusu mifumo yetu ya ulinzi! Mikoa iliyopo mipakan kuna watu weng mno toka nchi jiran wanafanya kazi hasa vibarua,biashara as if ni watz! Unaweza ukafika holili , jipe ,tarakea au toloha ukakuta duka la raia wa kenya na mamlaka zipo kimya tu! Ukija huku kwimba wapo waganda,wakenya na wanyarandwa kibao wananunua na kuuza mpunga as if ni wasukuma! Sasa huwez jua majasusi wapo wangap humo kwenye hayo makundi! Sio ajabu ukakuta kagame ana taarifa zote za gesi ya mtwara, chuma cha liganga nk! Si alituma kikosi kupambana na ugaid msumbiji!?
Yoweri Museveni ameishi Tanzania,amesoma hapa, amefundisha Tanzania.
Museveni Tanzania ni kama nyumbani.

Kuhusu raia wa mataifa jirani kuzagaa wakijitafutia rizki ni kawaida.
Hata watanzania wamejaa tele kwenye miji ya nchi jirani.
Watanzania wametapakaa kwenye miji ya mipakani ya nchi za Msumbiji, Malawi, Zambia, Congo na Burundi.
Watanzania wanamiliki biashara mbalimbali kwenye miji na vijiji vya nchi jirani zetu
 
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?
Kwanini sasa muingie kwenye mivutano na Museveni? Maccm bana huwa mnakuwa na akili za kijinga kijinga tu

Ndo mjifunze sasa kuwa na Marais wenye exposure siyo kuwa na lirais linapajua kijijini kwao tu hadi linatamani kijiji kiwe nchi inayojitegemea (Chato zii)
 
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?
Kasoma UDSM
Kafundisha UDSM
Harakati za mapinduzi ya Uganda mipango yote alikuwa anafanyia mapori ya Tanzania kwa msaada wa askari wa Tanzania akina Apson/mstaafu.
Nyerere alikuwa kichwa sana.
1. Kabila mkubwa
2. Museveni
3. Kagame
4. Mandela alifichwa Mazimbu Morogoro
Kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki na kusini tulikuwa kama coordinator wa michakato ya ukombozi
 
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?
Wewe hujui Tanzania ndio wamemuweka pale?
 
Binafsi mi nimekuwa na mashaka haya kuhusu mifumo yetu ya ulinzi! Mikoa iliyopo mipakan kuna watu weng mno toka nchi jiran wanafanya kazi hasa vibarua,biashara as if ni watz! Unaweza ukafika holili , jipe ,tarakea au toloha ukakuta duka la raia wa kenya na mamlaka zipo kimya tu! Ukija huku kwimba wapo waganda,wakenya na wanyarandwa kibao wananunua na kuuza mpunga as if ni wasukuma! Sasa huwez jua majasusi wapo wangap humo kwenye hayo makundi! Sio ajabu ukakuta kagame ana taarifa zote za gesi ya mtwara, chuma cha liganga nk! Si alituma kikosi kupambana na ugaid msumbiji!?
M7 na Kagame plus Kabila wa Kongo, both baba na mtoto wote hao ni vijana wetu, Kabila Jr kasomeshwa kwa kodi zetu kuanzia msingi, secondary hadi Jeshi, baba yake alikua anaishi Sinza na Kabila kakulia Sinza, secondary kasoma Sumbawanga huko, same same na hao wengine including M7 anae zungumziwa hapa. Kwa taarifa yako, M7 ndio mwanzilishi wa wazo la kumpa Nyerere UTAKATIFu ule wa Roman Catholic, anamuonaga Nyerere kama baba yake kabisa. So sio ajabu
 
Nimekuwa namsikiliza rais wa Uganda mara kwa mara akitoa hotuba zake hasa akiwa hapa nchini, kwa kweli huyu mheshimiwa kijiografia anaijua vizuri sana Tanzania.

Unakuta anaelezea maeneo ya ndani ya nchi yetu yaani vijiji na mpaka makabila ya maeneo husika tamaduni zao, lugha zao nk.
Sasa ikiwa mtu kama huyu tukaingia kwenye mivutano naye haiwezi kuwa hatari kwetu kutokana na kwamba anajua vingi sana vya kwetu!?

Pk ndiye wa kuogopwa
 
M7 na Kagame plus Kabila wa Kongo, both baba na mtoto wote hao ni vijana wetu, Kabila Jr kasomeshwa kwa kodi zetu kuanzia msingi, secondary hadi Jeshi, baba yake alikua anaishi Sinza na Kabila kakulia Sinza, secondary kasoma Sumbawanga huko, same same na hao wengine including M7 anae zungumziwa hapa. Kwa taarifa yako, M7 ndio mwanzilishi wa wazo la kumpa Nyerere UTAKATIFu ule wa Roman Catholic, anamuonaga Nyerere kama baba yake kabisa. So sio ajabu
Kabila kasoma Sangu - Mbeya sio sumbawanga. Nyumba wanazo kibao tu, kunduchi , Tegeta nk.

All in all, sio tatizo kwa foreigner kuijua TZ maana wengi wameishia hapa no sawa na mtanzania aliyeko nchi za watu nae anayajua ya huko hakuna sehemu wanasema asipite mtu asiye raia.

Ishu kubwa ni government top secret kufika kwao, na hizi zitafika sio kwa kusema wasije TZ Bali ni kuhakikisha haifanyiki espionage.

Bahati mbaya wengi wamepata nafasi serikalini hivyo hapo ndio kun shida, unakumbuka Kuna Kanali alikuwa jeshini kitengo Cha IT akatimka kwao Rwanda na Kagame akampa nafasi serikalini nadhani alikuwa Waziri au Naibu? Hii ndio hatari kubwa Ila ya museveni kuvijua vijiji hata mie navijua vijiji vya Uganda na maeneo take mengi.
 
Back
Top Bottom