Musoma: CCM yaizawadia Shule kengele ya Kisasa

Nadhani kuna haja ya kuifungua akili yetu kiasi.
Najua kuna shule zina changamoto ya kukosa kengele, na kwa hatua ya maisha tuliyonayo bado rim za magari zitaendelea kutumika hata miaka na miaka (hilo siyo tatizo).

Hata kama ingekuwa mwalimu wa shule husika ameomba asaidiwe kupata kengele, kuna mantiki gani kwa hiki kilichofanyika?

Ikishindikana sana tuazime hata akili za Anthony Mtaka halafu hizi zingine tupeleke workshop hadi zikae sawa.
 
Kwahio Rim ya Canter ndio kengele ya kisasa 🤣🤣🤣?!

Siku ikiletwa ile ya umeme itaitwaje sasa?
 
Wametisha sana.Waandikiwe barua ya shukrani kwa uzalendo,ubunifu,kutojikweza,huruma,moyo wa kugawana mema ya nchi na huba kubwa walioonesha kwa uongozi wa shule,walimu wote na jumuiya ya wanafunzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…