Musoma: Padri wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bunda apandishwa Kortini kwa kuongoza Genge la Uhalifu

Mapadri wamecharuka na madili, dili za hela, dili za albino.....wataanza na udalali

Hawa ndio mapadri ambao kanisa limewatengeneza miaka ya hivi karibuni. Wengine ni very corrupt. Hawaogopi kuliabisha kanisa. Kitendo kama hiki ni cha kidhalimu na hakikubaliki. Majimbo karibu yote kuna vituko vya mapadre wake.

Inashangaza sana na inaaccha maswali, hawa mapadri waliandaliwaje mpaka wakawa Mapadri? Haina maana kuwa na mapadri wengi halafu hawana lolote la kuchangia zaidi ya kuongeza uvunjifu wa maadili. Kuna walimu wa aina gani kwenye shule za maandalizi ya mapadre?

Kusema kweli wanatukwaza sana. Ingekuwa vema kila jimbo lianze kuangalia upya mienendo ya mapadri wake wote. Kuanzia seminary mpaka kupewa daraja takatifu. Bora wawe wachache ila wema kuliko kuwa wengi halafu corrupt, ili kuondoa hizi aibu ambazo sasa zimeanza kutokea ndani kabisa ya kanisa.

Na mapadre ambao wamefungiwa kwa hila na uonevu, sababu ya kusimama imara kwenye kazi ya wito wao, warudishwe mara moja.

Tuache kujidanganya tumesimama wakati tunaanguka. Na kanisa sio mali binafsi ya maaskofu ambao wanalea au kuchochea kupata mapadre wasiostahiki kuwa mapadre.
 
Luca shida yako ni kutofahamika kama weye chawa wa duniani au motoni,anaye kuelewa atusaidie kukujua tasafali.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…