Musoma: Raia wawatuhumu TRA kugonga raia wakiwa wanafukuza magendo

Musoma: Raia wawatuhumu TRA kugonga raia wakiwa wanafukuza magendo

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Musoma, Tanzania

Waziri Mwigulu Nchemba apigwa maswali mazito na wananchi mkoani Mara



Wakaazi wa Sirari Rorya wasema wanamtambua vizuri hata mawe na majabali ya (mawe) kote nchini yaandikwa mwigulu rais ktk ya kampeni za urais 2015.

Baada ya sofa hizo waelezea fani na kamatakamata inayofanywa na mamlaka za serikali.

Wananchi waliobeba box 5 thamani yake kwa ujumla shilingi 70,000 wanakamatwa na pia wenye magari wanaosafirisha wafanyabiashara hao wadogo nao wanapigwa fani kwa kubeba mizigo hiyo ya abiria mfano box hizo za sabuni.

Kinachowauma ni kuwa jambo hilo haliwatokei wafanyabiashara wakubwa ....

Source : Bongo5


Kumbukumbu za wananchi wa Sirari wakati Mwigulu Nchemba alipotia nia kugombea urais kuelekea uchaguzi 2015

1663004471869.png

==
Mbele ya Waziri Nchemba Raia mbalimbali wametoa kero zao kwa waziri wa fedha Mwigulu Nchemba ambapo dereva wa taxi amelalamikia kunyimwa leseni na LATRA na kupigwa faini kubwa kila anapokamatwa.

Aidha watu wengine wawili wamelalamikia suala la maafisa wa TRA kuwafukuza raia kwa fuji wakikimbiza magendo hali inayosababisha vifo kwa watu hao.

Raia mwingine amelalamikia fedha za miradi ambazo ni robo ya fedha hizo ndizo hufika kwenye vijiji.

Akijibu kero hizo waziri wa fedha amesema serkali imeyasimia na itayafanyia kazi.
 

MAWAZIRI TANZANIA WAMEANZA KUPIGWA MASWALI MAZITO NA WANANCHI , RAIS AMETULIA MAGOGONI ,DAR ES SALAAM.​

 
AHADI YA MWIGULU KWA WANA MUSOMA, KERO ZAO ATAFIKISHA KWA RAIS

Waziri Mwigulu baada ya kupigwa maswali, atoa majibu na kuahidi kuyafikisha kwa mheshimiwa Rais

Waziri Mwigulu anasema mbali ya maendeleo ya vitu kama barabara na madaraja sasa serikali inajali maendeleo ya watu.

Hivyo ametaka mtu mojamoja anaye jishughulisha na kazi zake za kujiari katika kipindi hiki cha sasa lazima aheshimiwe sana maana serikali haiwezi kutoa ajira kwa wote serikalini.

Mwigulu Nchemba anasema wanaojiajiri kwa namna hiyo wanatuletea maendeleo ya watu na pia usalama wa taifa kwa vile wanajiajiri na kutoa ajira kwa wengine hivyo nchi inapata amani na utulivu.

Anaongezea katika hotuba hiyo kuwa serikali ina majukumu makubwa sana hivyo kuna ulazima wa kugusana gusana kwa tozo na kodi ili miradi mikubwa ikamilike na mapya vile yaanzishwe.

Miradi hiyo mikubwa waziri Mwigulu anayobainisha gharama zake kwa uchanguzi ni
  • Trilioni 6 shilingi za kiTanzania bwawa la Mwalimu Nyerere kule Stiegler's Gorge Rufiji
  • Reli SGR MPYA trilioni 23 hadi mtandao mzima Dar Kigoma, Mwanza na nchi jirani kukamilika,
  • Deni la mikopo ya kimataifa Tshs. trilioni 11 za mikopo lazima kulipwa kila mwaka
  • pia mishahara ya serikalini kwa mwaka ni Tshs. trilioni 9 na bado kuna miradi ya elimu bure ambayo ni bilioni 33 n.k ambayo siyo mikubwa.
Source : Bongo5
 
Hii Tanzania yetu haihitaji maswali magumu tena kwa hawa viongozi, wameshazoea kutoa majibu mepesi maisha yanaendelea, naona sasa inahitaji vitendo vigumu kwao tuone kama wataendelea kutoa majibu mepesi.
 
Back
Top Bottom