Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Uchaguzi 2020 Musoma: Tundu Lissu alala Butiama nyumbani kwa Mwalimu Nyerere

Jamaa anapuyanga tu huko, ona anachohutubia
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

Nawapenda sana watani zangu Wagogo, naamini kabisa mtanipa kura, tena inawezekana Lusinde akanitafutia Kasichana kazuri ka Kigogo au mnasemaje Wagogo?, si mtanipa?, zege halilali, RC Dodoma mwagize Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma huu mwezi wa tisa ndani ya miezi miwili Barabara ya Mlowa kwenda Mvumi itangazwe tenda kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami ili Wagonjwa wanaougua hapa wawe wanapelekwa Mvumi, tunataka Jimbo hili ambalo lipo karibu na Makao Makuu ya Nchi tulibadilshe liwe lenye kunusanusa makao Makuu”
Jpm akiwa Mtera leo
Huko ni kupuyanga?
 
Lazima atawasumbua tu hao akina nyerere haishi visasi

Hakuna watoto ambao hawajali kama wa Nyerere wao maisha yao ya kawaida ...useme ukiwatesa watakosa kula Pizza ...
Wakati wa Kikwete Makongoro alishughulikiwa sana hadi akakosa ujumbe wa NEC na MWENYEKITI CCM MARA kwa kuwabana mtandao kwenye vikao vya chama , ni mjumbe pekee wa NEC ambaye alikuwa anasimama kumwambia Kikwete ,Lowassa na Rostam ukweli bila kuwaogopa wala kupepesa jicho.
Hata sasa kwenye kamati kuu mjumbe pekee mwenye uwezo wa kumuambia Magufuli ukweli bila kuonyesha kumuogopa au kuogopa atamfukuza ni Makongoro ....hadi kuna siku Magu aliwauliza wasaidizi wake , "...huyu anajiamini na nini ?"
Ujuwe hana shukrani Makongoro na Bulembo ndio watu pekee 2015 walimpigia kampeni nchi nzima wakati ule mgumu . ....safari hii kwa obsession za kina Bashiru na Pole wakawaondoa
 
Mwalimu Nyerere alipinga ubaguzi sana. Lissu ni Mtanzania kama Watanzania wengine
 
Hakuna watoto ambao hawajali kama wa Nyerere wao maisha yao ya kawaida ...useme ukiwatesa watakosa kula Pizza ...
Wakati wa Kikwete Makongoro alishughulikiwa sana hadi akakosa ujumbe wa NEC na MWENYEKITI CCM MARA kwa kuwabana mtandao kwenye vikao vya chama , ni mjumbe pekee wa NEC ambaye alikuwa anasimama kumwambia Kikwete ,Lowassa na Rostam ukweli bila kuwaogopa wala kupepesa jicho.
Hata sasa kwenye kamati kuu mjumbe pekee mwenye uwezo wa kumuambia Magufuli ukweli bila kuonyesha kumuogopa au kuogopa atamfukuza ni Makongoro ....hadi kuna siku Magu aliwauliza wasaidizi wake , "...huyu anajiamini na nini ?"
Ujuwe hana shukrani Makongoro na Bulembo ndio watu pekee 2015 walimpigia kampeni nchi nzima wakati ule mgumu . ....safari hii kwa obsession za kina Bashiru na Pole wakawaondoa
Aisee duuuh

Hata hapo CCM nakongoro yupo tu kimwili kiitikadi yule mpinzani kitambo.

Kumbe jamaa wanawazingua sana akina NYERERE
 
Ukoo wa Nyerere siyo uliopiga kura za maoni acha upotoshaji.

Ukoo wa Nyerere ni mdogo sana pale Zanaki, hata kura zingepigwa kwa koo wasingeshinda acha kupotosha.

Musoma hakuna tabia za kujipendekeza kwa familia maarufu, hayo mambo yapo huko kwa waswahili wenzenu, Chalinze, Lindi and likes.

JPM alilenga kumdhalilisha Makongoro kwakua anatajwa tajwa kuwa Rais. Jiulize nani aligombea urais na MAGU 2015 hajadhalilishwa kisiasa
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?

Mama Maria alisimamishwa atoe neno kwenye mkutano wa kampeni za CCM.

Akasema hana la kusema yeye kawekwa kuongeza idadi ya watu tu
pale.

Kwa watu tunaojua kusikiliza mtu tulielewa.Kwa mama kama yule aliyeiona historia ya nchi nzima tangu inazaliwa kusema vile, ilikuwa kama anaikosesha radhi CCM.
 
Mgombea wa Urais wa CHADEMA amelala Nyumbani kwa Mama Maria Nyerere Mjane wa Baba wa Taifa

Kwa heshima anayopewa Baba wa Taifa ndani ya CCM na nchi kwa Ujumla hii haina madhara kwa familia na Chama?

Pale kuna gesti hata wewe Ukitaka unalala, kwa hiyo hakuna tatizo hapo
 
Nadhani familia ya Mwalimu ipo kiupanzani upinzani sana.
Mfano mjukuu wa Nyerere Vicent amewahi kuwa mbunge Musoma kupitia CHADEMA.
Mke wa Madaraka Liticia Nyerere (sasa marehemu )aliwahi kuwa mbunge wa viti maalum Kupitia Chadema.
Makongoro Nyerere aliwahi kuwa nccr mageuzi na akawa mbunge wa Arusha.
Nyerere pia aliwahi kusifia sera za CHADEMA hivo alikufa nusu CCM nusu CDM.
Hayati baba wa Taifa angekuwa hai leo angekuwa bennet na mzalendo mwenzake Tundu Lissu
 
Nyerere alisifia sera za chadema kwakua baadaye aligundua mshauri wake wa uchumi na waziri wa fedha Edwin Mtei alikuwa sahihi kwenye ushauri aliompa wakagombana ...na ni yeye ndiye alimrecomend Mtei kwenda kuwa Mkurugenzi WORLD BANK ....na hata alivyorudi Alimrecomend Mtei kwa Mwinyi akamteuwa kwenye Tume ya MTEI iliyoshauri mfumo wa kodi na kuunda TRA inayosifika leo
Lakini pia Chadema wasisi wake karibu wote walikuwa watumishi wa serikali waandamizi ambao walikuwa hawakubaliani na Ujamaa na ndio maana sera nyingi za sasa za serikali za Uchumi wa Soko ilikuwa copy and paste ya hizo sera za chadema ambazo Nyerere alizisifia na wakti huo chadema kilikuwa chama kidogo sana , vyama vikubwa vilikuwa CCW[ mapalala], NCCR, UMD etc laki aliwaambia CCM chama kitakachokuja kuwasumbua mbeleni sio hivyo bali ni Chadema

Pia kikubwa ni kuwa chadema wasisi wake hawakuwa na umaskini wa kipato ...walikuwa matajiri ,wasomi au wafanyabiashara ..hivyo hapakuwa na tatizo kubwa la kurubuniwa na kuwekewa vipenyo waharibifu kama vyama vingine ambavyo viongozi wake walikuwa hasa na umasikini hasa wa kipato ....pamoja na kuwa na msimamo mkali walishindwa kujizuia pale serikali ya ccm ilipopenyeza pesa
Andiko zuri nimejifunza mengi hapa.
Nadhani bila blaa blaa CHADEMA ni CHADEMA chenye mikakati na sera nzuri kwa Taifa.
Mfano kuna Bavicha queen..Kuna Bawacha,Bavicha na kuna Baraza la wazee .
Sera zao zinajikita ktk misingi ya utu haki na maendeleo.
Ila CCM na vyombo vya dola zinaona CDM n chama kinachokuja kuahiribu maslahi yao.
 
nadhani ndio maana halisi ya Baba wa Taifa .....hata Baba yao aliwakaribisha wote nyumbani kwake na kuna wakati ccm walilalamika yeye kula na wapinzania ,,,...akawajia juu !!

Halafu hata kisiasa ilimshinda nini Magufuli hata kwenda tu Butiama wakati huu wa kampeni kusalimia na kuzuru kaburi na badala yake akachagua kuagiza mama maria aburuzwe kuletwa mkutanoni na hata kupangiwa na kina pole pole aseme nini ????
Magufuli huyu huyu kawauwa kisiasa watu wote aliogombea naye urais ndani ya ccm 2015 ...niambieni mmoja tu aliyebaki ambaye hajamuuwa kisiaasa ......
Mwisho hapa kamchuuza Makongoro aende kugombea ubunge huku akijua uchaguzi ule uliojaa rushwa ......na hata baada ya kushindwa hakutaka kumpitisha kama alivyowapotisha aliowataka kina Kunambi ...lengo lake anataka ahakikishe kuwa ikifika 2025 hakuna mpinzani hata ndani ya chama chake .......huyu hakuwa mtu wa kuondoka 2025 lakini atakuwa ameona watu hawamtaki ..na mwaka huu lazima AIBE SANA KURA na bado hazitatosha atatangazwa kibabe ..na mdogo wake baba mmoja mahera
Mwaka huu magufuli bila kumwaga damu hawezi kutangazwa msindi maana kushindwa ameshashindwa kabla hajaanza
 
Hakuna watoto ambao hawajali kama wa Nyerere wao maisha yao ya kawaida ...useme ukiwatesa watakosa kula Pizza ...
Wakati wa Kikwete Makongoro alishughulikiwa sana hadi akakosa ujumbe wa NEC na MWENYEKITI CCM MARA kwa kuwabana mtandao kwenye vikao vya chama , ni mjumbe pekee wa NEC ambaye alikuwa anasimama kumwambia Kikwete ,Lowassa na Rostam ukweli bila kuwaogopa wala kupepesa jicho.
Hata sasa kwenye kamati kuu mjumbe pekee mwenye uwezo wa kumuambia Magufuli ukweli bila kuonyesha kumuogopa au kuogopa atamfukuza ni Makongoro ....hadi kuna siku Magu aliwauliza wasaidizi wake , "...huyu anajiamini na nini ?"
Ujuwe hana shukrani Makongoro na Bulembo ndio watu pekee 2015 walimpigia kampeni nchi nzima wakati ule mgumu . ....safari hii kwa obsession za kina Bashiru na Pole wakawaondoa
Nimeshangaa sana jinsi Abdalla Bulembo alivyo kimya, kama vile sio yeye aliyekuwa kampeni manager wa Magufuli 2015
 
Nimeshangaa sana jinsi Abdalla Bulembo alivyo kimya, kama vile sio yeye aliyekuwa kampeni manager wa Magufuli 2015
Ccm ina vichwa vingi siyo kama chadema kwamba akiondoka Mbowe chama kina kufa.
 
Back
Top Bottom