Vijana tusiwatenganishe wazazi wetu! Tuwaheshimu na kuwathamini huku tukiwajali kwa chochote kidogo tukipatacho:
View attachment 2710529
Nawasihi kama haujawahi kuiona ewe kijana ambae mbeleni ni mzee tafadhali itafute hii ni zawadi na fundisho kubwa mno kwetu.
View attachment 2710531
Fundisho kwetu:
1.KAMWE SIKU ZOTE USIACHE KUTENDA WEMA, wema ni akiba.
2. Tunaishi na wazazi ila daima hatuoni thamani yao
Kuna Yatima wanalia kwa hiyo nafasi ya upendeleo tuliyopewa kuishi na wazazi ambao sisi hatuoni thamani yao.
3. Ewe mzazi siku zote walee watoto wako katika malezi mema coz nao siku moja watakuwa wazazi.
4. Ewe kijana wewe kuwa na huo umri wako, elimu yako, na kila kitu chako basi tambua ni wazazi wako walijinyima ili tu wewe ufanikiwe kuvipata hivyo ulivyo navyo.
Thamini na kutambua mchango wao katika elimu yako. Kazi nzuri na kipato visikufanye uwadharau wazazi wako na kuwaona ni wajinga.
5. Ewe kijana ishi na mumeo / mkeo kwa akili na usipokuwa makini basi atakupoteza kwa kuongozwa na tamaa.
Mke ni nguzo ya mafanikio kwa mumewe.
Mkiishi kwa upendo daima mtafanikiwa kwa lolote mlipangalo.
Mke au mume usiwe sababu ya migogoro katika familia za wengine.
Huyo mume unaemuona hivyo usidhani ameshushwa kutoka Mbinguni bali ni Juhudi na upendo wa wazazi wake.
Tumia akili kuishi na familia yako plus wazazi wako coz bado wana nafasi kubwa katika maisha yako.
6. Mti ili uwe na matunda kule Juu, tambua mizizi yake inapata virutubisho huku chini.
Wazazi ni mizizi yetu daima.
Hii movie imeniliza sana
duh huyu mzee anajua.
itafute hata subtitle ya English tu.
Hautajuta