MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Hii filamu imetengenezwa kutoka kwenye vitabu vya Phillip Pullman, His Dark Materials ambavyo vilipigwa marufuku kwasababu vilikuwa vinakashifu dini ya Ukristo. Kinachonifurahisha kuhusu hii filamu/tamthilia ni maudhui yake tu: Ukifuatilia kwa undani Pullman anasifia kile ambacho kilitokea barani Ulaya miaka ya 1776-1848, (Age of Enlightenment) ambapo wasomi walianza kupambana na nguvu ya Kanisa Katoliki pamoja na wafalme wa Ulaya.
Kikibwa zaidi hii tamthilia inasifia kabisa matendo ya The Illuminati (The Enlightened Intellectuals), ambao walikula kiapo kupambana na Kanisa Pamoja na Mungu wao. Humu ndani The Illuminati wanawakilishwa na mwanasayansi Lord Asriel ambaye anashirikiana na malaika walioanguka (The Fallen Angels), kupambana na Kanisa Katoliki (The Magesterium) likimuwakilisha mungu wao (The Authority).
Hii filamu/tamthilia imetengenezwa kikawaida, lakini kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa kinachoendelea duniani utagundua kabisa ujumbe mbaya ambao hii filamu inausambaza. Mle ndani kumejaa mambo ya ajabu sana ya kiimani na kisiasa, ambayo yamekuwa yakiendelea. Ukiangalia vizuri kuna Secret Societies kibao mle ndani na alama zake,.....
Pullman (The Author) himself confessed that the aim of the books and series is to undermine christian beliefs and send a message to the Catholic Church. It's just intense, perverted and rebellious,......
Kama una roho nyepesi usiangalie kabisa wala usisome vitabu vyake,.......