Mimi kuelezea siwezi kwa kweli ndio maana nahofia nisije nikaelezea nikaharibu ladha halafu ukafikiri ni mbaya kisa usimulizi wangu mbovu[emoji38][emoji38]
Huyo demu kwenye cover page anaitwa Wednesday na amehamishwa na wazazi wake kutoka shule aliyokuwa anasoma kwenda Nevermore. Nevermore ni shule ya outcasts, wanafunzi wake ni kama watu wa kawaida tu ila wana abilities mbalimbali ambazo binadamu wa kawaida hawana, wengine wana uwezo wa kujibadilisha na kuwa viumbe hatari.
Kwenye maeneo ya jirani ya Nevermore kuna mauaji yanafanyika na watu wanashindwa kujua ni nani anayefanya hivi huku Mayor wa Jericho town na askari mkuu wa mji huo wanafikiri kuwa ni dubu ndio anafanya haya mauaji. Lakini ukitafakari kwa kina inaonekana kiumbe kinachofanya mauaji haya ni kiumbe chenye akili kwa sababu kinaua na kuchukua baadhi ya viungo vya mwili kama vidole gumba, moyo n.k
Wednesday ni binti jasiri, anafuata njia zake, hajali hisia za watu, ni mkaidi hakati tamaa, genius jeuri na ni mchunguzi pia. Kwa mara ya kwanza kabisa Wednesday alipata kuona kiumbe hiki kikiua mtu mbele ya macho yake. Ndipo Wednesday akaanza kukifuatilia. Wednesday anapata psychic visions zinazomsaidia kuona past na future na zilikuwa zinampa mwangaza sana kwenye uchunguzi wake. Baadaye kabisa Wednesday anakuja kugundua kuwa huyo Monster ni mwanafunzi mmojawapo kutoka Nevermore school. Anajiuliza maswali mengi huyu monster [emoji88][emoji88] ni nani, na kwa nini akiua anachukua viungo, anashirikiana na nani hapo shuleni na mambo mengine kibao.
Hivyo Wednesday anaamua kupeleleza hili suala kiundani zaidi huku akiwahisi baadhi ya watu kuhusika.
Wednesday 2022 ni miongoni mwa series zilizotazamwa zaidi Netflix kwa sasa
View attachment 2501420