Musukuma aisifia DP world ya Dubai sakata la bandari. Adai Taifa linacheleweshwa na wajinga wanaotaka kushirikishwa kila kitu

Huamini kama.tumepata Uhuru?
 
Kazi ya serikali ni ipi? Na je serikali ilishindwa kutumiza majukumu yake kinaachofata ni kipi?

Siku zote mnaisifia humu serikali kufanya kazi nzuri, Leo mnakataa kuna sehemu haufanyi vizuri.

Sheria zipo wazi, dola ipo, serikali ipo. Hamjui mfanye nini?
 
Kuna wakati saa mbovu huonesha majira sahihi! Kwa hiyo siyo ajabu bali tunadili hoja iliyo mezani; Je Mama Samia na Mbarawa wana nia njema na bandari zetu? Kwa nini bandari za Zanzibar hazimo? Kwa nini tunaendelea kugawa ardhi yetu kwa Waarabu tu? Je kwa nini Marais kutoka Zanzibar ndiyo wanachangamkia ardhi ya Tanganyika? Maana tuliona Rais Ali Hassan Mwinyi naye kutoka Zanzibar ndiye aliyewauzia Waarabu Ngorongoro alipokuwa Rais wa Tanzania.

Hoja hizi zinahitaji majibu.
 
Sawq
 
Huamini kama.tumepata Uhuru?
Huamini kwamba uhuru hauifuti historia?

Jina Dar es Salaam limetoka wapi? Jisomee:

 
Suala la hawa jamaa kuchukua bandari yetu hii haizuiliki tena, je

ajira zitakuaje..?,

Usalama wa bandari yetu jee..?

Vipi wahamiaji haramu, bidhaa haramu, silaha kupenyezwa kimagendo.?

Taarifa sahihi za mapato yatokanayo na bandari tuyajuaje..?

Tutamonitor vipi exports zitakazokuwa zinafanyika bandarini..?

Mbao, makinikia, pembe za ndovu, pamba na bidhaa zingine muhimu zitaenda ulaya na mataifa mengine bila control yetu

Hiyo kamati ilihoji haya mambo kweli...?

Ni suala la muda CDF akawa ulamaa kutoka UAE na jeshi letu kwenda mikononi mwa watoto wa baniani [emoji848][emoji57][emoji706][emoji706][emoji706]

Wanaanza kidogo kidogo mwisho watataka kulima wenyewe, control ya Mbuga zetu itakua kwao, kila kitu kitakua chao

TANZANIA INAELEKEA KUBAYA,
 
Hizi ni changamoto nzuri za nchi yenye amani. Kumbuka hayo mataifa makubwa yana uhuru una miaka zaidi ya 200 lakini kuna mahali panaboreshwa bado.
 
Haka kajamaa kanafikiri kuwa na mdomo wa kuongea basi umemaliza kila kitu.......hivi kwa elimu ya la saba unaweza vipi ku comprehend mambo mazito ya mstakabali wa nchi yanayohitaji elimu kubwa with high reasoning capacity.

Yaani kutembelea dubai na kuona mashine tu zinafanya kazi badala ya watu hiyo tayari ni justification ya kugawa bandari kwa waarabu!

Kwa sasa nchi ina wasomi wengi sana, hivi haiwezekani mbunge angalau awe na elimu ya shahada ya kwanza ili angalau tuwe na wabunge wanaoweza kutoa hoja kwa weledi.​
 
Huyu alimwingiza Chaka Lowassa kisha akamtosa

Akaja kumuingiza Chaka Magufuli

Mtu aliyekula nyama ya mtu huwa haachi

Kupenda hela za dezo akakusanya wajinga wajinga wenzake akalazimisha kuingia GGM. Eti chama kinataka kutembelea uwekezaji. Akazuiwa getini. RPC mmoja akasema huwezi kuingia bila kibali. Akaanza naye bifu.
Kwa ufupi ni kweli hajasoma na anaungaunga kama yeye mwenyewe anavyosema.
Prof labda Kishimba🤣🤣🤣🤣🤣
 

Yes wanaweka 4T ila Hawa DP inatakiwa waweke 9T kukamilisha GATE 9 ,pesa tunazo kabisa eg Tunatenga 550B kila mwaka kununua magari ambayo matumizi(wese+maintanance) yake ni mara mbili ya gharama za kununulia ,bado kuna pesa zinapotea kwenye semina ,warsha,makongamano ,per diem na vitu vinayotaka kunafana na hivyo ni nyingi sana!
 
JPM alituonyesha tunaweza, lakini hawa ndugu wengine wanaturudisha utumwani...SGR ni trilioni ngapi tushindwe ya bandari...Pesa huwa zipo bank na siyo kwingine...Chamsingi tuondoe hao binadamu ambao tangu enzi wanaendeleza nepotiam kwa nafasi critical ndiyo sababu hawana ubunifu zaidi ya kufisadi mali ya watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…