Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Kama kweli aliamini hivyo mbona alikuwa mbele kupiga na kufagilia nyungu...!!
 
Ule haukuwa utafiti kuwa Tanzania hakuna korona, isipokuwa ulikuwa utafiti kuwa korona hata kwenye mapapai inaonekana. (Labda mchato alitaka kuiaminisha dunia kuwa corona is a Hoax)
Mkuu, leta basi matokeo ya utafiti kwamba Tanzania kuna korona
 
Waziri wa afya, Katibu MKUU WA wizara ya afya, mganga Mkuu wa serikali, wote ni jirani zako . Waulize hayo maswali. Ila chato wanawalaumu sana.
 
hujamuelewa msukuma-anahosema kwa nini prof A anatoa jib tofauti na prof b
 
Mkuu, leta basi matokeo ya utafiti kwamba Tanzania kuna korona
Utafiti mwepesii kabisa ambao hata mtoto anaukubali ni kuona vifo sababu ya korona. Sasa nikuulize wewe, Tanzania hakuna mtu hata mmoja aliyekufa na korona?
 
Acha uongo kwahyo yale mapapai ni ww uliyafanyia utafiti?
Haukua utafiti wa kujua kama kuna korona.

Alikua amefanya vile ili kujua kama majibu wanayotoa maabara ni halisi siyo ya kupikwa.
 
Huyu muheshimiwa Msukuma yaani kila anapotoa hoja haachi kabisa kuwadhihaki wana taaluma sijui kana kwamba walimkosea nini au wao ndio walikuwa namemzuia asisome?

Hakuna Professor hata mmoja aliyesema hakuna korona na wala hakuna Daktari yoyote aliyesema hayo kwanza hakukuwa na platform ya kufanya hivyo.

Ushauri tuu kwa Msukuma basi huna budi kupeleka watoto shule
 
amuulize Dr Ndungulile kilichompata
 
Maprofesa sampuli ya Muongo, na yule Wa kafu aliyetengua barua unaweza kutegemea nini kutoka kwao? Wanaangalia upepo ubwabwa unatokea wapi? Huko huko wanapiga pambio!! Hata hao maprofesa wa tiba upepo ulishabadilika!! SAA hii wanavalia kininja ni mwendo wa kufunika pua na midomo kama hawana akili nzuri! Wabongo kwa unafiki!! Ikitokea ( najua haiwezekani) JPM akafufuka na kurudi kwenye kiti chake na mama kurudi kwenye kiti chake cha awali, hao wanaosemà less government watapiga pambio za more government!! Na barakoa hutakaa uione imetorokea wapi!! halafu watu ni wàle wàle!! Wabongo kwa unafiki!!
 
Hahahaaaa...... Msukuma ni la 7 lakini anaongoza kwa kujenga hoja mwanana bungeni!
Musukuma kajenga hoja nzuri sana ila kuna watu watampinga lakini ukweli uko palepale-maprofesa ao hao walisema hakuna corona Tanzania lakini pia wakaenda mbali kwa kusema hata vifaa vya kupimia vinanganya ndio maana mbuzi, fenesi na mapapai yalipatikana na korona hivyo huo ni uzushi mtupu ila leo wamebadili gia angani wanasema korona ipo na chanjo inahitajika.
Kwa hili namuunga mkono Musukuma.
 
Wataalam wetu hawana jipya zaidi ya copy and paste.Msukuma yupo sawa waje na chanjo ya kitanzania na siyo kutusomea vitu walivyoandikiwa.
 
WANAFIKI wanataka kujitoa sasa kwenye legacy.😂😂
Huyo msukuma ni mpumbavu sana, kama aliamini kua Corona haipo wakati wa Mwendawazimu mwenzie, imekuaje nayale MANYUNGU aliokua anajifukiza.
MaCCM ni hovyo kabisa
 
Usiseme "sisi", sema wewe, usiwapangie wengine
 
Uzuri maprofesa wote waliofanya utafiti ni makada wa ccm
 
Msukuma ana ugomvi mkubwa sana na wasomi sijui kwanini.

Na anageuza habari! Hao maprofesa wakati wa JPM ni lini walifanya utafiti wakagundua Tanzania hakuna korona? Hakukuwa utafiti wowote isipokuwa kulikuwa na matamko kuwa Tanzania hakuna korona
Usimlaani sana, anayo sababu. Kuna kitu kinaitwa REDET pale UD, Mlimani, Chuo kikuu. Kilianzishwa na huyo anayejiita Profesa Mkandara. Kila leo REDET ikawa ni kusema uongo tu! Leo hii bado anaaminika hadi kupewa kuzungumzia mambo ya kitaifa. Aibu tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…