Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Chanzo: Clouds Digital
Tunahitaji kubadilisha sheria zetu ili mtu awe mbunge anatakiwa awe ana shahada
 
Magu alisema kutokana na waliyoyasema matokeo ya utafiti uliofanywa na wachunguzi/maprofesa/doctors na wanausalama aliowatuma
Si kweli alisema yeye mwenyewe alipeleka sample maabara ya taifa na ndio matokeo yakaonesha zile sample ambazo zilikuwa za mapapai na oil chafu zina Corona, na kule maabara ya Taifa wanaopima hizo sample wala sio hao Maprofesa....ni mkurugenzi tu wa maabara ndio alikuwa na PhD...
 
Form seven ni Shida, yaani yeye anadhani kipindi cha utawala ULE yale maamuzi ya kupinga na Kuficha kuwa Corona haikuwepo yanaweza ku-hold water kwa kiongozi wa sasa mwenye Maono (uongozi sikivu). Hivi ni kweli huyo form Seven hajui hasara ya kupoteza wapendwa wetu kwa Maamuzi ya ajabu ajabu. Mimi Ilikuja kunizidishia machungu na niliuchukia utawala ule zaidi tena Zaidi pale tu Dada yangu Daktari alipofariki kwa corona and was the only Dr in our family. Baba alikuwa anatuambia alimsomesha kwa gharama kubwa. Tumwombe tu huyo form seven hasiturudishe matesoni,kwani maamuzi ya uongozi wa sasa kuhusu Corona (task force ya kumshauri SSH kuhusu Corona) ni sahihi na yaheshimiwe. Anachojifanya hajui ni kuwa, Watawala uliopita Ulikuwa unaogopwa, ulikuwa utawala wa YES BOSS or ONE MAN SHOW kila alichokisema mtawala ndicho wasaidizi wake walikitenda na kutuaminisha kuwa tuko sahihi ili mradi tu Maisha na familia zao vilineemeka na utawala ule.
Acha kuwa zumbukuku, msukuma pamoja na std seven yake lkn bado ana hoja ya msingi kabisaa! Huwezi kuweka taaluma matakoni kwa sababu ya wanasiasa..hivi magufuli angewafanya nn madaktari wote wangebaki na msimamo wa kisayansi!?? Mbona professor wa chuo kikuu huria aliyeandika waraka alibaki kuusimamia ingawa serikali iliupinga!?? Huwezi kuwa msomi huku husimamii ulichosoma!!
 
Mbona na yeye msukuma hakusema ukweli?
 
Acha kuwa zumbukuku, msukuma pamoja na std seven yake lkn bado ana hoja ya msingi kabisaa! Huwezi kuweka taaluma matakoni kwa sababu ya wanasiasa..hivi magufuli angewafanya nn madaktari wote wangebaki na msimamo wa kisayansi!?? Mbona professor wa chuo kikuu huria alyeandika waraka alibaki kuusimamia ingawa serikali iliupinga!?? Huwezi kuwa msomi huku husimamii ulichosoma!!
I don't exactly your position. Unasifia ujinga tulioachana nao kwa Msaada wa Mungu au Unabisha tu Kwa sababu shule yako ni ndogo.
 
Form seven ni Shida, yaani yeye anadhani kipindi cha utawala ULE yale maamuzi ya kupinga na Kuficha kuwa Corona haikuwepo yanaweza ku-hold water kwa kiongozi wa sasa mwenye Maono (uongozi sikivu).

Hivi ni kweli huyo form Seven hajui hasara ya kupoteza wapendwa wetu kwa Maamuzi ya ajabu ajabu. Mimi Ilikuja kunizidishia machungu na niliuchukia utawala ule zaidi tena Zaidi pale tu Dada yangu Daktari alipofariki kwa corona and was the only Dr in our family. Baba alikuwa anatuambia alimsomesha kwa gharama kubwa.

Tumwombe tu huyo form seven hasiturudishe matesoni,kwani maamuzi ya uongozi wa sasa kuhusu Corona (task force ya kumshauri SSH kuhusu Corona) ni sahihi na yaheshimiwe.

Anachojifanya hajui ni kuwa, Watawala uliopita Ulikuwa unaogopwa, ulikuwa utawala wa YES BOSS or ONE MAN SHOW kila alichokisema mtawala ndicho wasaidizi wake walikitenda na kutuaminisha kuwa tuko sahihi ili mradi tu Maisha na familia zao vilineemeka na utawala ule.
Pole sana kwa kufiwa na mwanafamilia. Mwanafamilia mmoja anapotoweka na zaidi ya maelfu usiowafahamu.

Mungu awajalie nguvu za kuishi na hayo machungu.
 
I don't exactly your position. Unasifia ujinga tulioachana nao kwa Msaada wa Mungu au Unabisha tu Kwa sababu shule yako ni ndogo.
Wewe shule ulienda kusomea Ujinga! Wapi ulipoona nimesifia?? Jibu hoja ya huyo darasa la 7, hoja yake ipo wazi ilikuwaje wakati huo wasomi watuambie kitu kingine na leo tena waseme vinginevyo!??
 
Msukuma ana ugomvi mkubwa sana na wasomi sijui kwanini.

Na anageuza habari! Hao maprofesa wakati wa JPM ni lini walifanya utafiti wakagundua Tanzania hakuna korona? Hakukuwa utafiti wowote isipokuwa kulikuwa na matamko kuwa Tanzania hakuna korona
Nadhani ana inferiority kwa sababu ya kuksa elimu. Anajua alichokikosa, na kwa sababu hawezi kukipata, anajitahidi kujipa moyo kuwa siyo kitu muhimu.
 
Ni kauli za walioshindwa kuendelea kusoma. Msomi ni msomi tu, mfumo wa kumfanya mwanasiasa awe juu ya mwanataaluma ndio unaowafanya walazimishwe kutoka nje ya weledi wao
Kwa hilo uko sahihi! Mbunge Musukuma analipwa milioni 11 na marupurupu mengine. Profesa unamlipa milioni 6 bila marupurupu mengine. Hapo Musukuma anajikuta akijiona ni mtu muhimu kuliko kila Profesa.
 
Wewe shule ulienda kusomea Ujinga! Wapi ulipoona nimesifia?? Jibu hoja ya huyo darasa la 7, hoja yake ipo wazi ilikuwaje wakati huo wasomi watuambie kitu kingine na leo tena waseme vinginevyo!??
let us urge objectively, the issue is no body was ready to loss his job simply b'se the knew exactly what their boss wanted by the time being. Usijifanye amnazo or bongolala a.k.a Form seven ukashindwa kujua nchi ilikuwa inaenda kama gari bovu.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Chanzo: Clouds Digital
Hahahah
 
Back
Top Bottom