Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Musukuma: Maprofesa wanatuchanganya; wakati wa Magufuli walisema hakuna Corona na wakati huu wa Samia wanasema tuchanjwe

Anawaonea maana mpaka mawaziri walifikia hatua ya kuogopa kuvaa barakoa kwa sababu ya hofu ya dikteta hayati maiti
 
Anawaonea maana mpaka mawaziri walifikia hatua ya kuogopa kuvaa barakoa kwa sababu ya hofu ya dikteta hayati maiti
Nilicheka na kuchoka walipotangaza "mwamba kadancha" ghafla bin vuu nikamwona "profesa maja..." katinga barakoa... matumbo haya...
 
Form seven ni Shida, yaani yeye anadhani kipindi cha utawala ULE yale maamuzi ya kupinga na Kuficha kuwa Corona haikuwepo yanaweza ku-hold water kwa kiongozi wa sasa mwenye Maono (uongozi sikivu).

Hivi ni kweli huyo form Seven hajui hasara ya kupoteza wapendwa wetu kwa Maamuzi ya ajabu ajabu. Mimi Ilikuja kunizidishia machungu na niliuchukia utawala ule zaidi tena Zaidi pale tu Dada yangu Daktari alipofariki kwa corona and was the only Dr in our family. Baba alikuwa anatuambia alimsomesha kwa gharama kubwa.

Tumwombe tu huyo form seven hasiturudishe matesoni,kwani maamuzi ya uongozi wa sasa kuhusu Corona (task force ya kumshauri SSH kuhusu Corona) ni sahihi na yaheshimiwe.

Anachojifanya hajui ni kuwa, Watawala uliopita Ulikuwa unaogopwa, ulikuwa utawala wa YES BOSS or ONE MAN SHOW kila alichokisema mtawala ndicho wasaidizi wake walikitenda na kutuaminisha kuwa tuko sahihi ili mradi tu Maisha na familia zao vilineemeka na utawala ule.
Hivi dada yako (dakitari), kweli hakujua kuhusu corona?! Ndiyo hayo hayo yanayo mshangaza Mh. Msukuma. Au dada yako alikuwa anahonga na kupewa maksi tu! Hivyo siyo kweli kwamba baba alimsomesha kwa gharama kubwa! Matokeo yake - ukipewa degree bila kufahamu kitu darasani, kitakacho kuua hutakijua!
 
Kama Maprofessa walisema hakuna corona, ile.nyungu uliyopigq huku unajirikodi ilikuwa.ya nini?
 
Msukuma anapotosha,vile vipimo walivyopimia Mapapai havikuonyesha kuwa Tanzania hakuna corona bali vilionyesha kuwa ni vipimo vyenye kasoro
 
Hata JPM siku zake za mwisho alisema tufuate maelekezo ya wataalamu ila wajiridhishe kwanza wasipokee kila kinachotoka nje ila hajawahi kusema wazi kwamba hakuna corona ila yeye aliamini zaidi njia za maombi na kujivukiza sasa kama ilikuwa au anaamini hakuna corona ziele kauli zake alikuwa anaamanisha nini. Alikiiri corona ila tusiogope Mungu yupo watu waombe siku 3 aliwahi kukiri mtoto wake aliumwa corona haya aliyasema mwenyewe. Ila yeye alikuwa na njia zake za kupambana na Mama ana maoni yake lakini hakuwahi kusema hakuna corona, na video kibao zipo.
 
Dah Msukuma ana aleji na maporofesa............ mapprofesa Maprosoo
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Chanzo: Clouds Digital
Maprofesa wetu wamekuwa wanasiasa, wanaangalia wapi mkubwa kalalia. Angalia makarablasha watakyobeba kuonyesha usomi wao,inabidi wabebe na mkomkoteni kuja kuwakilisha hayo makarabrasha yao ili kuonyesha kwamba kweli yale wanayowakilisha ni ya kweli kumbe ni mbwembwe tu kama za msemaji wa simba.
 
Mbunge wa Geita vijijini mh Joseph Kasheku aka Msukuma amesema maprofesa wa Tanzania wanafeli sana na hii inasikitisha ndio maana aliwaripua bungeni.

Msukuma amesema kwa mfano tafiti za Corona zilizofanywa na maprofesa wakati wa hayati Magufuli wakitumia mapapai mbuzi, sungura, mafenesi na oil ilionyesha Tanzania hakuna Corona lakini alipoingia Rais Samia maprofesa walewale wameshauri tuanze kuchomwa " masindano" na kuvaa mabarakoa.

Msukuma anajiuliza hawa maprofesa wetu wamesoma kweli?

Msukuma amemshauri Rais Samia kutumia wanasayansi wa nje kama anaona hawa wa kwetu wamejaa longo longo.

Chanzo: Clouds Digital
Hamuna labda hiyo ilikuwa " Speaking Error"
Mbona " Typing Error" ipo inakubalika?
 
Chanjo ya corona ni ufisadi tu. wakowapi wanaoumwa korona Tanzania? Kama korona inawafuta wavaa barakoa hao wa high profile ambao wakati Hayati yupo walikuwa hawavai na wala hawakufa, basi wachanjwe wao.

Yawezekana virusi vinaambatana na mawazo ya kiutawala utawala na ndiyo maana hata chanjo inagusa hadi DNA na RNA ili pengine iwaondolee hisia za utawala ili corona wasiwafuate.

Sisi tusio viongozi hatuna korona na hatuvai mabakkoa na hiyo korona haijatufuata, watuache.

Si rahisi kuelewa mpangi huu ni ufisadi wa aina gani.
Mku sema tu hujaenda kupima, lakini ukipima tu utakutwa nayo!!!!!!
 
Anawaonea maana mpaka mawaziri walifikia hatua ya kuogopa kuvaa barakoa kwa sababu ya hofu ya dikteta hayati maiti
Hilo sio kweli kwa sababu hata sasa hao mawaziri hawavai barakoa au wewe unawaona bungeni na barakoa?
 
Back
Top Bottom