Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amesema haina haja ya kuweka wahudumu wanaotoa huduma za ndani ya treni ya Mwendokasi (SGR) ili kuepuka shirika kupata hasara kwakuwa ndio kwanza mradi huo umeaanza hivyo haina haja ya kuweka gharama kubwa za uendeshaji.
"Hakuna haja ya kuwa na wahudumu wanaopita kuuliza abiria kama wanakunywa chai au kahawa. Treni inapaswa kuwa na behewa rasmi la chakula, kama ilivyo kwenye huduma za kimataifa, ambapo abiria ana uhuru wa kwenda kununua chakula au kinywaji bila kusubiri kuulizwa."
Mbunge Musukuma ameyasema hayo leo Februari 03, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu na Nishati na Madini