Musukuma: SGR inawahudumu kama Ndege, tutapata hasara waondolewe

Musukuma: SGR inawahudumu kama Ndege, tutapata hasara waondolewe

Mawazo ya kijima!

Anataka SGR iwe kama "gogo" la kigoma!
Hata usafi wa vyoo usiwepo!

What a disgrace!
 
Yuko sawa. Sema kuna wachangiaji humu wanakurupuka kama Kasongo. Amesema liwepo behewa la chakula anayehitaji aende akale siyo awepo mtu wa kupita kuuliza watu kama wanataka kula. Misuse of public funds.
Labda ndiye huyo muhudumu wa behewa la chakula hakuona watu wakienda kula akaona achangamshe miguu
 
Mawazo ya kijima!

Anataka SGR iwe kama "gogo" la kigoma!
Hata usafi wa vyoo usiwepo!

What a disgrace!
Wewe ndiye una mawazo ya kijima. Umewahi walau kusafiri nje ya Tanzania? Sehemu nyingi sana wameshaondoa zile huduma za kutumia watu na wameweka self service. Treni zinakuwa na automatic machines na unanunua chochote unachotaka. Kwa sababu sisi bado tuko nyuma, ingekuwa vizuri wakaweka mabehewa ambayo watu wanakwenda kununua wenyewe. Kitu kama usafi wa vyoo watu wawili wanatosha kufanya shughuli au wanaocheki tiketi. Bila kubana matumizi treni zitakufa.
 
So ana discourage ajira hapo then haoni shida Wala nini
Hao watakaoajiriwa hawataweza kulipa kodi itakayozidi faida za SGR, Serikali inajali pesa zaidi kuliko life standard za hao watakaoajiriwa
 
"Hakuna haja ya kuwa na wahudumu wanaopita kuuliza abiria kama wanakunywa chai au kahawa. Treni inapaswa kuwa na behewa rasmi la chakula, kama ilivyo kwenye huduma za kimataifa, ambapo abiria ana uhuru wa kwenda kununua chakula au kinywaji bila kusubiri kuulizwa."
Huyu anataka kuturudisha kwenye zama za kusafiri na ugali kwenye bag la nguo
 
Kama ni kweli anachokisema Musukuma,ninashauri Kadogosa afukuzwe kazi,na sio kusimamishwa kazi ,Wala kuhamishiwa pengine
 
Mawazo ya kijima!

Anataka SGR iwe kama "gogo" la kigoma!
Hata usafi wa vyoo usiwepo!

What a disgrace!
Uliwahi kwenda China ukapanda SGR kutoka Beijing kwenda Gouzhuoh zaidi ya Kms 3000?
Kinachofanyika Tanzania SGR ni uhujumu uchumi na musukuma Yuko dawa 100%
 
Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amesema haina haja ya kuweka wahudumu wanaotoa huduma za ndani ya treni ya Mwendokasi (SGR) ili kuepuka shirika kupata hasara kwakuwa ndio kwanza mradi huo umeaanza hivyo haina haja ya kuweka gharama kubwa za uendeshaji.

"Hakuna haja ya kuwa na wahudumu wanaopita kuuliza abiria kama wanakunywa chai au kahawa. Treni inapaswa kuwa na behewa rasmi la chakula, kama ilivyo kwenye huduma za kimataifa, ambapo abiria ana uhuru wa kwenda kununua chakula au kinywaji bila kusubiri kuulizwa."

Mbunge Musukuma ameyasema hayo leo Februari 03, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu na Nishati na Madini

Hao ni chakula cha viongozi na nafasi zao hazitangazwi bali huwafikia walipo. Ushamba na ulimbukeni ndio ulifanya waajiriwe, alfajiri anasafiri na sanduku lake la magurudumu toka Dar. anakwenda Dodoma mchana anarudi Dar na sanduku lake ndani zimo zana za mashosti!
 
Ni kama vile kuwa na mkuu wa mkoa na wawilaya na wakurugezi wakati kazi zote hizo zingemalizwa na mtu mmoja tu.
Ulitaka watu wale wapi? 😹😹
Kwann usiwaseme wabunge ndio mizigo pale bungeni?? Min acha roho mbaya 🤣
 
Back
Top Bottom