Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku Musukuma amesema haina haja ya kuweka wahudumu wanaotoa huduma za ndani ya treni ya Mwendokasi (SGR) ili kuepuka shirika kupata hasara kwakuwa ndio kwanza mradi huo umeaanza hivyo haina haja ya kuweka gharama kubwa za uendeshaji.
"Hakuna haja ya kuwa na wahudumu wanaopita kuuliza abiria kama wanakunywa chai au kahawa. Treni inapaswa kuwa na behewa rasmi la chakula, kama ilivyo kwenye huduma za kimataifa, ambapo abiria ana uhuru wa kwenda kununua chakula au kinywaji bila kusubiri kuulizwa."
Mbunge Musukuma ameyasema hayo leo Februari 03, 2025 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia hoja ya Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu na Nishati na Madini
Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma, ameikosoa mifumo ya huduma katika reli ya kisasa (SGR), akipendekeza kuondolewa kwa wahudumu wa ndani ya treni kwa sababu huduma wanazotoa hazina umuhimu wa msingi. Akizungumza bungeni, Musukuma alieleza kuwa badala ya kuwa na wahudumu wanaopita kuuliza abiria kama wanahitaji chai au vinywaji, SGR inapaswa kuwa na behewa maalum la huduma za chakula na vinywaji, ambako abiria wanaweza kwenda kujipatia wanachohitaji bila usumbufu.
Katika takataka ambazo huwa azieleweki kama zina jisaidia haja gani ni huyu jina la kabila lake ukiondoa erufi za mwanzoni mbili unapata kiungo cha uzazi.
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa gharama zipo kwenye SGR tu na siyo kule walikojaza wabunge wa viti maalum wasio na kazi yoyote au kujaza wakuu wa mikoa. Wilaya na Wakurugenzi hiyo siyo gharama
Aliyeshiba hamjui mwenye njaa gharama zipo kwenye SGR tu na siyo kule walikojaza wabunge wa viti maalum wasio na kazi yoyote au kujaza wakuu wa mikoa. Wilaya na Wakurugenzi hiyo siyo gharama
Yuko sawa. Sema kuna wachangiaji humu wanakurupuka kama Kasongo. Amesema liwepo behewa la chakula anayehitaji aende akale siyo awepo mtu wa kupita kuuliza watu kama wanataka kula. Misuse of public funds.