PreGE2025 Musukuma: Wakuu wa Wilaya wanaotaka ubunge, Bungeni hakuna hela

PreGE2025 Musukuma: Wakuu wa Wilaya wanaotaka ubunge, Bungeni hakuna hela

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kuna siku mwaka 2012 nilikuwa nimerudi Tanzania likizo. Nikawa natembea kuona mji. Natoka zangu Zanzibar nimeshuka bandarini Forodhani Dar. Nikamwambia dereva aliyekuja kunipokea arudi na mizigo yangu nyumbani, mimi nitakuja mwenyewe.

Nilikuwa nataka kuuona na kuukagua mji wangu mwenyewe nikiwa peke yangu, huku nikitembea kwa miguu, baada ya kukaa ughaibuni kwa miaka 10 mfululizo bila kurudi likizo.

Nikatembea hapo mjini kutoka Forodhani nikakatisha mitaa nikienda maskani Upanga. Nikajikuta nipo Lumumba. Nikasema hapa nikipata sehemu ya kupata juisi na chakula itakuwa vizuri sana.

Naam, kama nilikuwa nimeomba dua iliyojibiwa vile, mkabala na ofisi ya CCM nikaona kuna mgahawa mkubwa. Nikaingia nipate chakula.

Sasa nimekaa pale Lumumba kwenye mgahawa nimeagiza chakula na juisi, meza na nyuma yangu walikuwa wamekaa watu wawili, kwa mazungumzo yao ilionekana wale ni wabunge wa CCM. Mmoja wao alikuwa analalamika kuwa ubunge hauna maslahi kama alivyofikiri. Kifupi alisema katumia pesa nyingi za biashara zake kujitosa kwenye kampeni za ubunge, lakini haoni atakavyozirudisha. Akasema , kwa msingi huo, hategemei kugombea ubunge tena kwenye uchaguzi uliofuata. Mwenzake naye alionekana kukubaliana naye na kulalamika kuwa ubunge hauna faida.

Niliwashangaa sana kusikia wameenda kwenye ubunge kutafuta pesa.

Nilipata maswali mengi sana kuhusu maadili ya hawa wabunge, haja ya kuwa na sheria za Campaign Financing zenye kutekelezwa na zenye meno, haja ya kupunguza mishahara na marupurupu ya wabunge ili watu wasitake kuwa wabunge kupata pesa bali kutumikia watu, na matatizo mengine mengi yanayoendana na haya.

Ni miaka 13 imepita sasa, lakini naona matatizo yale bado yapo pale pale.
Kuna ukweli flani kwa wale wanaoingia Bungeni kutafuta pesa. Kutegemea mshahara wa na posho ya Ubunge kutajirika ni ngumu kwa Nchi masikini kama yetu. Kila mchango, tuzo za mashindano jimboni, kutatua changamoto ndogondogo za Wananchi/wanachama zote zinakuhusu!

Nafikiri wapo wanaoingia kwa ajili ya connection za biashara, Uwaziri nk
 
"Umesema kuhusu wakuu wa mikoa, wakurugenzi, Makatibu Wakuu. Nimeona watu wengi wameacha kazi hadi Makatibu wakuu. Nataka kuwaambia na sema uwazi. Ubunge sio kama watu wanavyotafakari. Watu wanasema ukiwa Mbunge kuna hela za bure utapata. "Itakuwa tajiri mshahara ni mkubwa. Sijaona hizo hela, bungeni, zaidi nimeona kuna umaskini tu.

Zaidi umakuja na moyo wa kuwasaidia watu. Kwa sababu zile hela mgawanyiko wake ni mkubwa sana. "Sio zako. Unaweza ukawa unalipwa mshahara mkubwa Mil. 3. Unakutana na matatizo. Nina watu kama Sita wananisubiri wamefiwa wanataka msaada kusafirisha. Bado tunafungua shule. Yaani zile hela zote zinaisha kwenye matumizi. Hata familia huwezi kuwapa hela. "Hata ukiwa na pesa Ukija bungeni.

Unaweza kumaliza miaka mitano na ukatumia fedha zako. Na wengine wanafirisika. Ndio maana unaona watu wengi wameacha. Ukija na mawazo Ukisema bungeni kuna hela. "Ndio maana siamini kama bungeni kuna hela na nyinyi wenyewe mtanisaidia na Watanzania kwa sababu sisi sio wabunge peke yetu"- Joseph Kasheku 'Musukuma', Mbunge wa Geita.
View attachment 3385779
Chanzo:Clouds Tv
Mwenyewe anakuambia akiwa jimboni mwake kuwa bunge ni kwa ajili ya vialaza tu, aliwahi kunukuliwa akihoji kuwa mtu kama umesoma unakwenda bungeni kufanya nini, kule ni kwa ajili yetu sisi Standard 7 failures, ni sehemu yetu ya kucheza, kuruka serekasi na kufurahisha wananchi, huku tukijirusha na wabunge wanawake wa kuteuliwa. Uzuri huyu dogo anasemaga ukweli bila kuficha.
 
Kuna ukweli flani kwa wale wanaoingia Bungeni kutafuta pesa. Kutegemea mshahara wa na posho ya Ubunge kutajirika ni ngumu kwa Nchi masikini kama yetu. Kila mchango, tuzo za mashindano jimboni, kutatua changamoto ndogondogo za Wananchi/wanachama zote zinakuhusu!

Nafikiri wapo wanaoingia kwa ajili ya connection za biashara, Uwaziri nk
Wacha ujinga, Tanzania si nchi masikini.
 
Kijamaa kijanja sana hiki anadanganya umma live eti bungeni hamna hela yeye miaka yote hii anatafuta nini?Musukuma hwbu acha ubinafsi acha watu wapambanie makombe
 
Back
Top Bottom