Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,075
- 11,682
Sasa panahitajika mtu wa kuongea nao kinaga ubaga na anaeweza kupeleka ujumbe kwa watawala zipi ni non negotiable. Na huyo ni mtu ambae anaweza kuwasoma vizuri.Lakini Fundi, mbona tayari hao Wamagharibi washaainisha nini ambacho kitawaridhisha….
NaamBaadhi ya hayo mambo ni kumuachia Tundu Lissu na wafungwa wengine wa kisiasa.
Ni nani ataamua kuwa huo uchunguzi ni huru? Nani mwisho wa uwajibikaji ni wapi?Uchunguzi ulio huru wa hayo mauaji ukifuatia na uwajibikaji.
Hili ni rahisi kutekelezwa. Lakini wao wenyewe wanajua ubora wa hiyo mifumo inatokana na willingness wa taasisi husika kuhakikisha kuwa zinatekelezwa. Hao hao wakina Cruz ukiwauliza nani alishinda kati ya Biden na Trump, wanapata kigugumizi.Mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi ambayo yataweka mazingira yaliyo sawa kwa washiriki wa uchaguzi.
Katiba mpya bila taasisi ambazo ziko tayari kuitetea ni kujidanganya. Hata hii tuliyonayo ingetekelezwa inavyopaswa ingeleta matokeo tofauti na watu wangewajibishwa.Katiba mpya. Na kadhalika.
BadoUmeusoma huo muswada wa akina Ted Cruz?
Hilo hata mimi sikielewi. Lakini inaonekana huo ni mstari mwekundu kwao.Jamaa wameainisha mambo ambayo ni rahisi sana.
Mfano, Lissu siyo mhaini. Wamemfunga zaidi ya mwaka sasa.
That is so unnecessary. Kumuachia kuna ugumu gani, kwa mfano?
Hilo nalo silijui.Humphrey Polepole wamemteka na wanajua kabisa kilichomkuta, lakini they’re playing dumb.
Nakubaliana na wewe kuwa haya mambo sio magumu kuyatekeleza. Labda bado kuna watu wanaamini kuwa Trump hawezi kufanya kweli.
Amandla...