Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya Usalama wa Taifa, umewapa 'Kinga ya Jinai' Maafisa Usalama
Hutaki marekebisho ya sheria hii? Mbona marekebisho hayo ni muhimu kwa usalama wa nchi yetu!
Kutokana na Hali mbaya kabisa iliyopo hivi sasa hapa Tanzania ya Watu kutekwa na kupotezwa au kuuawa, Je, bado unaamini kwamba Sheria hiyo Ina UMUHIMU kwa usalama wa nchi hii?

Je, unayaona matokeo mabaya yanayoendelea kutokana na Sheria hii??
 
Idara ya usalama wa taifa ni kama vile hawana maelezo mazuri ya kazi zao. Tusishangae kila siku kuna drama na Raisi anawabadilisha wakurugenzi kila siku. Kwa wenzetu walio endelea usalama wa taifa kuna imegawanywa kwenye makundi mawili tu walinzi wa viongozi wa juu na mambo ya nje ya nchi. Usalama wa taifa wa Tanzania wenyewe unajishughulisha na shughuli za Polisi na hata siasa. Mfano Usalama wa taifa hautakiwi kwenda kwa mtuhumiwa hii ni kazi ya polisi pekee, usalama hautakiwi kushinda bandarini na hata airport hiyo ingetakiwa kuwa vitengo maalumu vya Polisi na tayari vipo.

Tatizo la sasa kwasababu kazi zake hazijaelezwa vizuri na viongozi kama Magufuli waliopita waliwatumia vibaya sasa Usalama wa Taifa umekuwa Mafia ya vigogo wachache. Usalama wa taifa unahusishwa na utekaji, wizi kwenye maduka vya fedha, wizi wa kura na utishaji wa wafanyabiashara. Usalama wa taifa unatakiwa kujishughulisha na shughuli za kimataifa zaidi na ndiyo maana kwenye balozi zetu kuna watu wa usalama wa taifa kutusaidia kwenye biashara za nchi, ulinzi na itelejensia na sio kujishughulisha na mambo ya nje.

Sasa imefika wakati usalama wa taifa wenyewe ndiyo wanajipa kazi ambazo sio zao

Ushauri wangu ni kwamba Raisi na viongozi walindwe na kitengo cha usalama cha jeshi na usalama wa taifa usijisuhulishe na mambo ya ndani kuepusha hii sitofahamu tuliyo nayo. Tutawalaumu Polisi kumbe huko ndani hawa usalama wa taifa hawashikiki na hawana madaraka kuwaambia chochote. Lawama zinaenda kwa Polisi badala ya hiki kikundi cha sirisiri ambacho kimejipa kazi za Polisi. Vigogo wa usalama wanataka Raisi Samia aogope hali ya nchi kiasi kwamba wenyewe pekee ndiyo wawe tegemezi kuanzia chama kushinda kuwatisha wapinzani wa kisiasa....

Usalama wa taifa tunavyo ongea hivi sasa wana sikiliza simu za wapinzani wa Mama ndani ya CCM na viongozi wengine wote sasa je hii ni kazi yao au wamejipa kazi ya kujipendekeza!
 
Back
Top Bottom