Mzalendo Uchwara
JF-Expert Member
- Jan 26, 2020
- 4,437
- 13,836
kiukweli hizi nchi zetu za.kiafrika ili uweze kuwashinda mabeberu huna budi kupingana na katiba ya nchi yako kwenye maslahi yao waliyoyachomeka katika hiyo katiba,Hili ni jambo la kuogofya sana linaelekea kutokea nchini, serikali imepeeleka mswada bungeni ili kumuongezea kinga rais na viongozi wengine wa bunge na mahakama kinga dhidi ya kushatakiwa moja kwa moja kwa kukiuka katiba ya nchi.
Huu ni mswada wa ajabu na wa kuogofya sana, mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi inakuwaje leo anatafuta uhuru wa kuivunja katiba hiyohiyo?
Inakuaje marais wengine wote waliotangulia hawakuona kikwazo chochote kwenye kufuata katiba lakini huyu wa sasa kwake yeye katiba imekua kero kwake?
Ni nini hatma ya nchi yetu ikiwa tutaruhusu ujinga wa namna hii kuendelea kutokea? Unajua hata Adolf Hitler aliingia madarakani kwa njia halali kabisa, lakini taratibu akaanza kujiongezea mamlaka na kuwanyamazisha wote aliowaona kuwa kikwazo. Mwisho wake sote tunajua kilichotokea. Binadamu wote ni corrupt kwa viwango tofauti tofauti, hauwezi kumpa binadamu mwezako mamlaka yasiyo na mipaka, mwisho wake ni mbaya tu.
Wito wangu kwa wote mlioapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati wenu ni sasa kufanya hivyo, the republic as we know it is under attack.
Mbona Wananchi hujawataja. Wananchi ndio wanaobariki hayo yote, hawapo serious, ukiwepo wewe na wote wanaopita hapa.Rais wa hovyo.
Baraza la mawaziri la hovyo
Spika wa hovyo
Wabunge wa hovyo
Bunge la hovyo.
Tuko chini ya utawala wa kipumbavu sana huu
Ni wakati sasa wa vyombo vya ulinzi na usalama kuingilia kati na kuwaweka sawa hawa watawala.
Maofisa wote wa jeshi, polisi na hata usalama wa taifa hua wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi.
Wakati ndio huu, tukishindwa kumdhibiti huyu Magufuli atazidi kuitumbukiza nchi kwenye udikteta hatua kwa hatua, tutakuja kuamka ikiwa too late.
Sio kweli, viongozi wa kiafrika wanavunja katiba zao kwa manufaa yao binafsi.kiukweli hizi nchi zetu za.kiafrika ili uweze kuwashinda mabeberu huna budi kupingana na katiba ya nchi yako kwenye maslahi yao waliyoyachomeka katika hiyo katiba,
Ndio hapo sasa, unasema unafanya mambo mema kwa maslahi ya nchi alafu unahaha kujiwekea kinga.Kama tunafanya kwa nia njema na kwa mapenzi ya dhati kwa Tanzania na Watanzania,
Ki ukweli hakuna haja ya kujiwekea kinga yoyote, maamuzi yetu, kazi zetu zitoshe kutukinga na kutusafisha maana tunania njema na tunakubalika pia.
Kinga tuwaachie wanaotaka ubabe na utukufu kama kina Kim wa north korea
Na ndio maana yake, unapokimbilia kujiwekea kinga dhidi ya uhaini inamaana imepanga kufanya uhaini!Magufuli siyo muadilifu na hupenda kuonea na kunyanyasa wasio upande wake.
Hofu hii ndiyo inamfanya ajijengee ngome ya sheria ili akiaacha madaraka asishitakiwe.
Angekuwa msafi asingekuwa na hofu hizi! Anavunja sheria na katiba kwa makusudi ndiyo maana ya yeye kuanza kujiwekea kinga.
Huu mswada ukipitishwa Ccm jiandae kuondoka mapema sana OctoberMulipoambiwa siku akitokea mwandawazimu kuongoza hii inchi anawaweza kujipa umungu mtu mlifikiria Nini? Hii ni rasha rasha tu.
Ndicho kitakacho fuata, amewaumiza wengi sasa mwisho wa siku atataka kufia ofisini ili kujilinda.Na baada ya hapo kitakachofuata ni kumfanya awe mfalme, utawala usio na kikomo.
Unafikiri lengo la kuwakingia kifua hao jamaa wanaohusika na mchakato wa sheria na katiba ni nini?