Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Muswada wa Marekebisho Sheria-2020: Unajua watu hawataweza kudai haki kwa niaba ya Wanyonge? Viongozi wa juu Serikalini hawatashtakiwa moja kwa moja!

Rais Magufuri ndiye Musa anaetupeleka nchi ya ahadi. Usijali
 
CCM Ni chama kijamaa na rais magufuri ni mwana ccm anaeishi kijamaa ndio tofauti na marais waliopita. Waliokuwa wana ccm waliokuwakiishi kibepari, mwenye akili atanielewa
 
Hili ni jambo la kuogofya sana linaelekea kutokea nchini, serikali imepeeleka mswada bungeni ili kumuongezea kinga rais na viongozi wengine wa bunge na mahakama kinga dhidi ya kushatakiwa moja kwa moja kwa kukiuka katiba ya nchi.

Huu ni mswada wa ajabu na wa kuogofya sana, mtu aliyeapa kuilinda na kuitetea katiba ya nchi inakuwaje leo anatafuta uhuru wa kuivunja katiba hiyohiyo?

Inakuaje marais wengine wote waliotangulia hawakuona kikwazo chochote kwenye kufuata katiba lakini huyu wa sasa kwake yeye katiba imekua kero kwake?

Ni nini hatma ya nchi yetu ikiwa tutaruhusu ujinga wa namna hii kuendelea kutokea? Unajua hata Adolf Hitler aliingia madarakani kwa njia halali kabisa, lakini taratibu akaanza kujiongezea mamlaka na kuwanyamazisha wote aliowaona kuwa kikwazo. Mwisho wake sote tunajua kilichotokea. Binadamu wote ni corrupt kwa viwango tofauti tofauti, hauwezi kumpa binadamu mwezako mamlaka yasiyo na mipaka, mwisho wake ni mbaya tu.

Wito wangu kwa wote mlioapa kuilinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania, wakati wenu ni sasa kufanya hivyo, the republic as we know it is under attack.
Huyu ni jizi,jambazi na kora! Anataka kuficha madhambi!
 
Sisi ni mabwege, ndo maana tunazungushwa kama pia na tunakubali bila kuchukua hatua stahiki, tunaishia kunung'unika kwenye mitandao! Halafu kuna wale mabwege zaidi, wanashangilia ujinga huu! Ila hakuna marefu yasiyo na ncha!
 
06 JUNE 2020
Utawala wa Sheria

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020, mtaalamu wa sheria afafanua


Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020 Mei 29, 2020, Bunge la Tanzania limekaribisha wadaua na wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada Na. 3 unaorekebisha sheria mbalimbali ikwemo Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu, 1994 (BRADEA) na Sheria ya Uongozi wa Mahakama namba 4 ya 2011. Moja ya mambo yanayopendekezwa katika mswada huo wenye lengo la kubadili sheria 13 ni pamoja na kuongezwa kinga ya kisheria kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, na Jaji Mkuu kutokushitakiwa moja kwa moja na badala yake mashitaka kuelekezwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Mapendekezo hayo pia yanapekwenda kuwapa kinga wafanyakazi wa mahakama, ambapo kinga hiyo ikitumika vibaya itapelekea uvunjifu mkubwa wa haki. Tazama uchambuzi huu kisha toa mano yako.

Source : HAKI TV
 
Nimejiuliza maswali mengi juu ya Sheria mpya Inayoenda kutungwa na watawala wetu sipati Majibu.Sheria ya kutoshitakiwa kwa Makosa waliyotenda wakiwa madarakani. Inamaana hawa waliapa kwenda kufanya Makosa?
Je,Kuna Makosa wamepanga kwenda kuyatenda kwa makusudi,kwahiyo wameona wajiandalie kinga kabisa?

Au wamepanga kuwafanyia kibaya gani watanzania mpaka wakaona bora watunge kabisa Sheria ya kwenda kuwalinda?

Au ndo Yale aliyosema Mwl Nyerere kuwa katiba imetoa madaraka makubwa sana kwa Rais kiasi kwamba akija Rais mwingine anaweza kuitawala nchi kidikteta?

Maswali ni mengi sana kuliko majibu,Lakini ninachoona ni kwamba kuna uwezekano wameandaa mazingira ya kuidhurumu nchi na ndo maana wakaona wajihami kwa Sheria hizi za ajabu ajabu.
MUNGU ATUHURUMIE.
 
Sio sawa, kuna tatizo gani mashtaka ya wanyonge yakifunguliwa na mtu au taasisi inayopigania wapate haki yao?

Vitu kama hivi vinakatisha tamaa wale wanaopigania haki.

Anyway, tusubiri tuone nini kitafuata
 
Yaani hili suala ni kaburi kwa utawala wa Sharia. Magufuli mpumbavu sana. Ni nini kapanga kufanya ?Hadi anapeleka mswada wa kipumbavu namna hii bungeni ?
Haya ni maoni yako Victoire ninayemfahamu au mtu mwingine? Tafadhali futa neno '....mbavu'.

Vv
 
Kinachonishangaza zaidi

Serikali ya awamu ya Tano

1. Imejaza maprofesa na madaktari kila kona
.....sheria Kabudi (mwalimu UDSM)
..... Tulia Phd (Jaji Mahakama kuu)
.....Mwakyembe Phd (mwalimu UDSM)

Naomba tuwaorodheshe, hawa wataalamu wetu wa sheria maprofesa na madokta

Je hili linalofanyika wanamchango gani?
Waliokotwa jalalani, walikuwa wanakula takataka sasa wanakula mapochopocho, hawaoni, wamevimbiwa.

Vv
 
Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa
By
Mtanzania Digital
-
March 17, 2019

maxresdefault-2-1024x515.jpg

Awaasa wenye siasa za malengo, tamaa Ikulu

NA AZIZA MASOUD-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaonyesha kuwa Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kutokana na kile kinachoitwa ‘kinga ya urais’ kuwa na mipaka yake.

Jaji Samatta ambaye amepata kuwa Jaji Mkuu kwa takribani miaka saba kabla hajastaafu mwaka 2007 alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwasilisha mada ya ‘Uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa katika vyombo vya dola pamoja na utekelezaji wa sheria na utoaji wa haki’ katika kipengele cha wajibu wa Ofisi Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) na Takukuru kwa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini.

Akiwasilisha mada hiyo katika mkutano wa uwajibikaji ulioandaliwa na taasisi isioyo ya serikali ya Wajibu, Jaji Samatta ambaye amekuwa akisifika kwa misimamo na kusimamia haki alirejea Ibara 46(3) ya Katiba akisema kinga aliyopewa Rais katika ibara hiyo haihusu vitendo Rais alivyovifanya akiwa Rais lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais.

“Ni ukweli kuwa chini ya Katiba ya nchi hii Rais Mstaafu anaweza kufunguliwa mashtaka Mahakamani na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).Ni muhimu sana ukweli huu ukaeleweka.

“Ni sahihi kabisa kusema kuwa chini ya Ibara 46(3) ya sheria mama hiyo rais aliyeacha madaraka ana kinga dhidi ya mashtaka, hata hivyo kinga hiyo ina mipaka. Inahusu tu “jambo …..alilofanya……kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa katiba…..”kinga hii haihusu vitendo alivyofanya Rais akiwa Rais,lakini inahusu vitendo alivyofanya kama Rais,”alisema Samatta.

Alisema kuna tofauti kubwa na iliyo wazi kati ya maneno ya ‘akiwa’ na ‘kama’,kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba aliyekuwa rais hana kinga dhidi ya mashtaka kuhusu jambo lolote ambalo hakufanya kama Rais.

“Kuhusu jambo la aina hiyo Mkurugenzi wa mashtaka ana mamlaka ya kumfungulia mashtaka na mahakama zina mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi hiyo kama ilivyo kwa kesi za jinai zinazoweza kufunguliwa dhidi ya watu wengine nchini.

“Kwa mfano kama alipokuwa madarakani Rais aliamua siku moja kuendesha gari yeye mwenyewe na akamgonga mtu na kusababisha kifo chake kutoakana na uzembe mkubwa kinga chini ya Ibara 46(3) ya Katiba haitamwokoa kutokana kwenye mashtaka ya kitendo hicho,vitendo vya ufisadi navyo vitakosa kinga hiyo,”.

Katika hilo hilo, Jaji Samatta alikwenda mbali na hata kuwaasa wale aliowaita wenye siasa za malengo au tamaa ya kuwa mpangaji Ikulu akiwataka watambue fika kwa faida ya nchi,ukweli huo.

Alisema watawala pia wanapaswa kuzingatia kuwa safari yao ya kuelekea huko na wakati wote watakapoongoza nchi kwenye jumba hilo kwamba ukweli ni kuwa Rais aliye madarakani hana mamlaka ya kutoa msamaha kwa mhalifu yeyote kabla hajapatikana na hatia mbele ya mahakama isipokuwa tu kama ibara ya 45(1) ya Katiba itabadilishwa kumpa mamlaka hayo.

Alisema hakuna shaka yeyote kuwa ofisi ya DPP ni moja ya ofisi kuu muhimu ndani ya dola hivyo jinsi Katiba inavyoelekeza ndivyo inavyopaswa kuwa katika nchi yenye kufuata utawala wa sheria.

“Ofisi ya DPP ikiyumba na utawala huo utatereka vibaya, hilo likitokea hakuna mwananchi ambaye hataathirika kwa namna moja au nyingine, moja ya malengo ya sheria ni kumpa DPP uhuru katika kutumia mamkala yake na kuhakikisha hakuna woga, uonevu au upendeleo katika kuamua mshukiwa ashtakiwe au mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya mtu huyo yafutwe au laa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema utenganisho huo wa mamlaka hayo pia unalenga kuzuia siasa kuingilia au kutumika katika masuala hayo nyeti na kitaalamu.

Alisisitiza kuwa ofisi ya DPP haipo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mshukiwa lazima ashitakiwe au mshitakiwa lazima aonekane na hatia.

Alisema DPP na maafisa walio chini yake ni watumishi wa nchi ambao wajibu wao ni kulinda maslahi ya umma yakiwemo yale yanayohitaji mtu asiye onyeshwa na ushahidi kuhusika na utendaji wa kosa la jinai hashtakiwi na mshitakiwa ambaye ushahidi dhidi yake hauthibitishi kwamba alitenda kosa hatiwi hatiani.

Alisema kutumia njia za uonevu na udanganyifu hakuwezi kuyafanya mapambano dhidi ya uhalifu likiwemo kosa la rushwa yafanikiwe kinyume chake hatua hizo zitafanya mapambano dhidi ya uhalifu kutofanikiwa na chuki dhidi ya watawala kujengeka.

“Mwananchi aliyeshitakiwa na kosa la rushwa na inaonekana na mahakama kuwa haijathibitishwa kutenda kosa hilo ana haki ya kuachiliwa ,kama mshitakiwa aliyeshitakiwa na kosa lingine lolote na ushahidi dhidi yake unaposhindwa kulazimisha atiwe hatiani.

“Wakati mwingine siku hizi ninaposikiliza taarifa ya habari kupitia vituo vya televisheni napata picha kuwa baadhi ya viongozi wa serikali wanateka mamlaka ya ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, bila shaka yoyote hatua hizo ni kinyume cha Katiba na zinaweza kusababisha viongozi wakahukumiwa kama watafunguliwa kesi za madai mahakamani na kuwalipa wanaonewa,”alisema Jaji Samatta.

Alisema hatua hizo za watawala zinaweza kusababisha kuharibika kwa kesi ambazo vinginevyo zingeweza kuthibitisha hatia za washtakiwa, uovu huo unaweza kutokea hata kwenye kesi za rushwa na mapambano dhidi ya uovu huo lazima yafanyike kisheria na si vinginevyo.

Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkurugenzi wa taasisi ya Wajibu ambaye ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh alisema a alisema lengo la taasisi hiyo ni kuongeza ushirikishwa wa wananchi katika suala zima la uwajibikaji.

Alisema aliamua kumualika Jaji Samatta kwakuwa ni mmoja kati ya viongozi waadilifu ambao wanaongea na kutenda vitu ambavyo wanaviamini na kwamba ni miongoni mwa watu wanaochukia rushwa kutoka moyoni.

Alisema mkutano wa jana ambao ni wa tatu baada ya kufanyika mikutano mingine mwishoni mwa mwaka jana katika Chuo Kikuu Dodoma pamoja na Chuo Kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro ni muendelezo wa kutoa elimu kuhusu uwajibikaji kwa wanafunzi wa elimu ya juu.

Mwisho

Source : Jaji Samatta: Rais Mstaafu anaweza kushitakiwa | Mtanzania
 
Wazalendo sio wengi siku zote.

Shibe mwana malevya, njaa mwana malegeza.

By

Mtoto wa mjini.
 
Ndicho kitakacho fuata, amewaumiza wengi sasa mwisho wa siku atataka kufia ofisini ili kujilinda.
Lazima tulipinge hili sisi kama wananchi.
Utapinga vipi? Mahakamani mmmh! Bungeni mmmh! Barabarani kuna polisi na vifaa vyao! JF na mtandao mingine ya kijamii kuna Bia Yao & Company! Kwenye sanduku la kura mmmh! Niambie utapitia wapi?
 
Hivi mtu ambaye hashtakiwi popote huwa anaapa ili iweje?
Kwa nionavyo mimi anaapa ili kuwapa ujiko viongozi wa dini. Hivyo akiapa viongozi wa dini wanaendelea kumsujudia na kumwambia ni chaguo la Mungu.
 
Ipo siku hii nchi itatawaliwa na mlundi stuvurugeeee alafu katiba iwe inamlinda hakuna kumshitaki popote sheria tumetunga wenyewe.
 
Back
Top Bottom