Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Ok ,Noted
Achane hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,
Hata kama hainisaidii lakini Kwani hofu ya kushitakiwa hawa ndugu hasa huyo wa kwanza inatoka wapi?
 
Ok ,Noted
Achane hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?...
Ondoa hii takataka yako. Hii kinga ya kutoshitakiwa ni ya nini kama wao wanafanya mema!? Ni wazi wana maovu mengi ambayo wanaogopa siku wakiwa hawana madaraka watalazimika kuyajibu. Bado wanadaiwa Roho ya yule msichana Akwilina aliyeuawa kutokana na matendo yao ya udhalimu. Bado trilioni 1.5 haijulikani wamepeleka wapi!? Au imefichwa Rwanda!? Haya watalazimika kuyajibu.
 
Bashite na Doto nao wapewe immunity...vyama vikuukuu Afrika vinaondolewa madarakani na mgombea anayetokea Ulaya...Gambia,Burundi,Rwanda ,DR Congo nk Sasa Maccm mjipange 4 October
 
Ndio anayetumika kupitisha sheria kandamizi. Kimsingi anayetaka ulinzi hapo ni rais zaidi. Ila amewachomeka hao wengine maana huwa anawatumia, na pia ni kupoteza watu maboya ili isionekane ni yeye mwenyewe.
Kwani kwa katiba ya sasa Rais anashtakiwa?
 
Awamu hii wanajua iwe iwavyo lazma wakiondoka madarakani ama ni ccm au upinzani utakaochukua utawala ni lazima washtakiwe.

Dhamira zao zinawasuta kwa matendo waliotenda ndio maana wanatafuta cha kuwafunika.

Hasa hii kitu inaitwa spika imeifanyia vurugu kuu katiba ya nchi kwa hii awamu.
Bado ni bure pia, Kinga ya kutoshtakiwa sio ulinzi wa kutolipwa matendo yako,ni busara tu za atakaekuwepo.Katiba ni makaratasi tu na sio musaafu isibadilishwe.

Huwezi ukaumiza wenzako ukategemea katiba ikulinde. Salama yao pekee ni kufia madarakani Kama m7 na PK.
 
Ok ,Noted
Achane hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,

Hujaathiriwa na hizo nguvu ndio maana unatoa haya maoni. Watu wameumizwa kwa ajili ya ulevi wa madaraka. Halafu kila sheria ya nchi inayotungwa ni lazima imguse kila mtanzania binafsi?
 
Katiba sio msahafu muda wowote unaweza ukaibadili
Kwa makusudi unavunja katiba, sheria, kanuni na taratibu zilizopo, halafu unakimbilia kujiwekea kinga ya kutokushtakiwa huko mbeleni ukitoka madarakani. Ni kwa sababu ya "fear of unknown, right!?" Lkn kumbuka hata hizo kinga huweza kutolewa pale inapopasa, na hata ukashitakiwa wewe peke yako na kwa nafsi yako wala si kwa cheo chako.
 
Sasa wewe una tofauti gani na kiazi?
Hujui maamuzi ya Spika kama kiongozi wa bunge yanaathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Rais kama kiongozi wa nchi yanaathiri maisha yako na familia yako?
Hujui maamuzi ya Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali yanaweza kiathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Jaji Mkuu yanaweza kuathiri maisha yako?
Wewe ni nani sasa kama siyo Kiazi?
Katiba inaweza kubadilishwa muda wowote
 
Ndio anayetumika kupitisha sheria kandamizi. Kimsingi anayetaka ulinzi hapo ni rais zaidi. Ila amewachomeka hao wengine maana huwa anawatumia, na pia ni kupoteza watu maboya ili isionekane ni yeye mwenyewe.
Chadema wapo bungeni wapunge
 
Jamaa hawana uhakika wa kesho yao. Wanajihami. Wanajua kabisa ya kwamba kuna makosa mengi wameyafanya mengine yanavunja katiba sasa wanajiwekea kinga. Kwani nani asiyejua kwamba kumrudisha bungene Mwambe aliyejivua ubunge ni kuvunja katiba? Nani asiyejua kuwakataza wapinzani kufanya shughuli za kisiasa ni kuvunja katiba? Nani asiyejua kuwa kununua ndege bila bajeti yake kuidhinishwa na bunge ni makosa? Nani asiyejua kuwa kuhamia Dodoma hakukupitishwa na bunge? Nani asiyejua kuwa fedha anazogawa Jiwe vichochoroni na barabarani hazijaidhinishwa na bunge? Nani asiyejua kuacha watu wapigwe risasi na kutekwa na kuwa kwenye viroba bila kufanya uchunguzi ni uhalifu? Kuna madudu mengi mno! Wanajihami hao.
Kesho ipi wakati wanadunda sana tu
 
Ok ,Noted
Acheni hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,
Yaan wee ni pimbi mnoo..kwnn hutaki kuumiza kichwa???kwnn wajiwekee sheria za kutokushitakiwa?? Nyie ccm mbona mnakuwa mapimbi kiasi hicho?? Kama ni watenda mema kwnn wanahofu ??? Hii awamu ni ya kishenzi sana ndo maana wanajihami
 
Back
Top Bottom