Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Wapinzani wengine sio hawa wapiga kelele
wapinzani wakishika ikulu hii haina nguvu yoyote..... hawa wastaafu wataswekwa Segerea 5 years wakati upelelezi ukiendelea.
 
Chadema wapo bungeni wapunge

Hilo watapinga, ila walio wengi watapitisha maana iwapo rais na jaji mkuu wanalindwa hata wakifanya makosa, basi na hao wengi wanaopatikana kwa kuvunja sheria, watafaidika na hiyo kinga ya hao viongozi.
 
Ondoa hii takataka yako. Hii kinga ya kutoshitakiwa ni ya nini kama wao wanafanya mema!? Ni wazi wana maovu mengi ambayo wanaogopa siku wakiwa hawana madaraka watalazimika kuyajibu. Bado wanadaiwa Roho ya yule msichana Akwilina aliyeuawa kutokana na matendo yao ya udhalimu. Bado trilioni 1.5 haijulikani wamepeleka wapi!? Au imefichwa Rwanda!? Haya watalazimika kuyajibu.
Sio kwa ajiri yao tu uwe unaona mbali
 
C kiaz tu bal n kiaz pori
Sasa wewe una tofauti gani na kiazi?
Hujui maamuzi ya Spika kama kiongozi wa bunge yanaathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Rais kama kiongozi wa nchi yanaathiri maisha yako na familia yako?
Hujui maamuzi ya Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali yanaweza kiathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Jaji Mkuu yanaweza kuathiri maisha yako?
Wewe ni nani sasa kama siyo Kiazi?
 
Peleka maoni mkuu muda unao wa kutosha tu. Hii ni Serikali sikivu sana tena unatumia mtandao tu, simple as that au wewe ulitaka wafanyaje?
Amtume lema bado ni mbunge
 
Bashite na Doto nao wapewe immunity...vyama vikuukuu Afrika vinaondolewa madarakani na mgombea anayetokea Ulaya...Gambia,Burundi,Rwanda ,DR Congo nk Sasa Maccm mjipange 4 October
Hii itamsaidia mdee siku akiwa rais
 
Sio kwa ajiri yao tu uwe unaona mbali

Ni kwa ajili ya nani? Sheria kwa ajili ya kutoshitakiwa ina nia gani kama sio kwa ajili ya kulinda uovu? Hapo sheria zinatungwa ili kulinda watenda maovu.
 
Bado ni bure pia, Kinga ya kutoshtakiwa sio ulinzi wa kutolipwa matendo yako,ni busara tu za atakaekuwepo.Katiba ni makaratasi tu na sio musaafu isibadilishwe
Huwezi ukaumiza wenzako ukategemea katiba ikulinde.
Salama yao pekee ni kufia madarakani Kama m7 na PK.
Mwambieni mbowe agombee atakuta kinga
 
Wewe umeethirika na lipi
Hujaathiriwa na hizo nguvu ndio maana unatoa haya maoni. Watu wameumizwa kwa ajili ya ulevi wa madaraka. Halafu kila sheria ya nchi inayotungwa ni lazima imguse kila mtanzania binafsi?
 
Ok ,Noted
Acheni hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,
Sisi wengine tunavichwa wewe mwenzetu umebeba boga kichwani.
 
Back
Top Bottom