Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Muswada wa Rais, Spika, Waziri Mkuu kutoshitakiwa unapangiwa siku mbili Juni 5&6 tena kwa hati ya dharura

Ukija uongozi mwingine, ni kutunga sheria itakayoruhusu mtu kushtakiwa kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani hata kabla ya sheria.

Sadam Hussein aliweka kinga zote lakini bunge jipya lilifuta yote. Akashtakiwa na akanyongwa. Viongozi wahitahidi kutimiza wajibu bila ya kuvunja sheria, wasipoteze muda wa kutunga sheria za kuzuia kushtakiwa.

Kiongozi akifanya uhalifu atashtakiwa tu, awe hai au amekufa. Kama atakuwa amekufa, itatangazwa ili wazao wake wajue kuwa mzazi wao alikuwa mhalifu.,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe una tofauti gani na kiazi?
Hujui maamuzi ya Spika kama kiongozi wa bunge yanaathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Rais kama kiongozi wa nchi yanaathiri maisha yako na familia yako?
Hujui maamuzi ya Waziri mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali yanaweza kiathiri maisha yako?
Hujui maamuzi ya Jaji Mkuu yanaweza kuathiri maisha yako?
Wewe ni nani sasa kama siyo Kiazi?
Tena kiazi jeshi
 
Sio kila mtu alikuwa muuza unga .pigana kivyako
Watz wasipofanya maamuzi magumu October hakuna tena nafasi ya kuyafanya tena ni mwendo wa mateso na kuumizwa zaidi ya walivoumizwa.Jiulize kwann Ikulu dodoma Hali ipo ya awali,pili vipi bashite akiwa ndie spika ajae tatu wawe na Kinga ya kutoshtakiwa unategemea huku tumetengwa na jumuia za kimataifa nn kitafata.Si wasiojulikana watamaliza watu, umasikini ukitamalaki huku idadi ya wakimbizi ikiongezeka.
Chondechonde dalili za mvua ni mawingu nafasi pekee ya kubadili upepo ni October.
Hata watumishi wanao nufaika Sasa vipi kesho wakianza kukopwa mishahara nn kinashindikana Kama wastaafu malipo yao tu ni tatizo vipi mishahara kuja kukopwa mbeleni huko?
 
Kiongozi ukifanya uhalifu utastakiwa tu Kinga sio kichaka cha kufichia uhalifu wako, kumbuka system mpya na Mambo mapya,ameshatkiwa Saddam,Bashiru, Mubarak wakiwa na Kinga.Salama pekee ya dikteta yeyeto ni kufia madarakani,akiwa nje ya madaraka ni lzm wammgawane aliowatendea mabaya
 
Ok ,Noted
Acheni hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,
Ficha ujinga wako.
 
Ok ,Noted
Acheni hofu ambazo hazina msingi kabisa

Maisha ya Rais,Spika,Waziri mkuu au Jaji mkuu wewe yanaathiri vipi maisha ya kwako binafsi au ya familia yako?

Je wewe binafsi ukiwapeleka hao mahakamani ni faida gani unapata ?au ni hasara gani unapata?

Tuache ushabiki wa kivyama,Sheria kama hizi hata siku moja hazikuongezei pesa mfukoni kwa wananchi wa huko nanjilinji au Singida

Je watanzania wangapi wanasoma hizo sheria kuhusu Rais kushtakiwa au kuachwa

Kila mtu apambane na hali yake,
Maswali na hoja za kipuuzi kweli kweli,na haijawahi kutokea.

Yaani hujui maamuzi ya rais,waziri mkuu ama spika yana athari gani katika maisha ya watu?

Wasiojulikana wanapotoa uhai wa watu wewe hujui kuna madhara gani kwa watu?
Serikali inapokosa kuajiri watu,kuongeza watumishi,kutoongeza mishahara kwa watumishi huoni tatizo lolote kwako?
Wabunge wanaopigiwa risasi hadharani na hawakutakiwa na serikali,wala tukio kuchunguzwa na serikali ilitoa kulinda na kuitetea katiba,hakuna shida?

Spika anapokosa kufuata katiba na sheria za nchi ili kulisimamia na kuliendesha bunge,wewe unaona poa kabisa?
Kwa hoja zako hizi naona kuna tatizo mahali,maana mlolongo ni mwingi.
 
Jamaa hawana uhakika wa kesho yao. Wanajihami. Wanajua kabisa ya kwamba kuna makosa mengi wameyafanya mengine yanavunja katiba sasa wanajiwekea kinga. Kwani nani asiyejua kwamba kumrudisha bungene Mwambe aliyejivua ubunge ni kuvunja katiba? Nani asiyejua kuwakataza wapinzani kufanya shughuli za kisiasa ni kuvunja katiba? Nani asiyejua kuwa kununua ndege bila bajeti yake kuidhinishwa na bunge ni makosa? Nani asiyejua kuwa kuhamia Dodoma hakukupitishwa na bunge? Nani asiyejua kuwa fedha anazogawa Jiwe vichochoroni na barabarani hazijaidhinishwa na bunge? Nani asiyejua kuacha watu wapigwe risasi na kutekwa na kuwa kwenye viroba bila kufanya uchunguzi ni uhalifu? Kuna madudu mengi mno! Wanajihami hao.
Naomba kuuliza swali, kwani rais mwingine akiingia madarakani haiwezekani kutengua sheria zinazowekwa kulinda wahalifu?

Kama inawezekana kwanini tuna wasiwasi?
 
Back
Top Bottom