Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Katiba: Download na pitia uone kilichomo na usambaze

Huu ni ujinga eti tume inaundwa na rais af haita jumuisha watu kutoka vyama vya siasa,wabunge wala watu wa usalama. Hizi ni njama za ****** wanataka kuleta katiba ambayo haibani chama tawala, tusikubali mpaka tuone tume huru itakayoundwa na bunge. Na wabunge wa cdm wawe makini coz hawa wabunge wa ccm wanaweza kutumia wingi wao kuunda tume ya ajabu. Inabidi wapiganaji wetu wawe makini sana tusiingizwe choo cha kike.
 
Msaada hauna shida yeyote iliyo wazi, marekebisho yanaweza kufanyika bila kuathiri upatikanaji wa katiba mpya Tanzania..
 
Sina uhakika na vijana wa Tz, wengi hawajishirikishi kujua namna nchi yao inavyoibiwa. nachojua kama wangejua
walau hata kidogo ujinga anaofanya kikwete ungekwama. Nahisi Jk anatuona sisi mafara.
 
Ndugu zangu kama munakaa chini munategemea CCM watafanya mabadiliko ya katiba na ikaeleweka, hapo mumenoa, kwasababu JAJI MKUU CCM sijui WAZIRI MAMBO YA KATIBA CCM, takataka gani sijui CCM, sasa nyinyi mutaishia kutoa maoni na kwa taarifa yenu katiba itabaki vilevile, hawa CCM ni Mambumbumbu sana na hawafikirii mbele, bali wanafikiria hapa walipo sasa
 
kwa mfano kusema kuhoji tume ya iliyoundwa na rais ni kosa la jinai amabayo azabu yake ni jela miaka mbili au failni ya mil. 5 au vote pamoja haina tofauti kabisa na ile sharia ya kiarabu ya kuadhibu kwa kupigwa mawe hadi kufa ukienda kinyume na uislamu.

kwa ndoto niliyooteshwa leo ni kwuwa huu mswaada kama wakristo wataukubali upite, basi watakuwa wahanga wa sharia kali za kiislamu na watapata mateso makubwa kutoka kwa hawa waislamu wa pwani.

na huu muswaada ukipita tu, basi tzazania haitakwepa kitanzaia cha kujiunga na OIC na kmakhakama za Kadhi ambazo huwa ni kero kubwa kwa jamii ya wakristo duniania kokote.

nawakilisha.

wewe ni mdini mbona tanzania imejiunga na vatican.ongea siasa na usiguse mamb yb dini
 
bunge la Tanzania lina wawakilishi wa rais na vyama vyao sio wawakilishi wa wananchi ndio maana katiba haiwahusu,Mawaziri ndio usiseme kama miungu watu kama wao wataishi milele kwa vyeo vyao hivyo mambo ya kitaifa yanaendeshwa kihuni maana viongozi wote wakola.
 
wewe MKWEGA udini wenu na rais wenu kama unaakili nzuri angalia vyeo mnavyopeana nyinyi kwa nyinyi,idara zote kuanzia wakuu wa mikoa,wilaya.wakurungezi ktk mashirika ya umma,marpc,majaji,mawaziri wizara zote mhimu,yote sumu ya rais wenu kikombe hicho hakitamuepuka hata milele na jamaa yake ndio kachaparaba mbele za haki utabili kwisha
 
Hivi kama mswada unapitishwa bungeni ili bunge likaitungie sheria; tunaweza kutegemea matokeo yenye usalama kwa watanzania wote kweli? Kama iliweza kutokea, bunge lenyewe kutunga sheria kama hii;
1. Afisa mtendaji wa mtaa kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi na kozi ya muda usiopungua miaka miwili....
2. Dereva wa serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na kozi ya udereva wa muda usiopungua miaka miwili...
3. Mhudumu wa ofisi ya serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na kozi ya waswala yanayofanana na uhudumu wa muda usipungua miaka miwili....
4. Mfungua geti la serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne na kozi ya uaskari wa muda usiopungua miaka miwili...

Lakini eti mbunge, anayesimamia serikali na watendaji wake; wakiwepo hao madereva, walinzi, nk. mwenye dhamana ya kujadili, kuhoji na kuidhinisha bajeti ya serikali, mwenye kutunga sheria zote nchini, nk ajue kusoma na kuandika kiswahili au kiingereza.....!

Kweli inaingia akilini? Sasa inakuwaje muswada wa kuandikwa kwa katiba mpya upelekwe kwa mtu mwenye ujasiri wa kudhubutu kutunga na kupitisha sheria kama hizo hapo juu? Tena aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuitunza katiba iliopo....! Ataelezaje mapungufu ya katiba aliyoapa kuilinda, kuitetea na kuitunza? Binafsi ningependekeza muswada huu uletwe huku kwa wananchi, na kama nao wana kiu ya kuchangia basi wataipata hukuhuku uraiani....!
 
Huyu co 2 mdini ila hata akili yake haina akili,kwanza co msomi wa kitabu anachokiamini,pili hawez kuoteshwa na mungu na hawezi kua prophets,tatu pia hajui kua wanaooteshwa ndo hawa hawa wanaotuambia 21 may ilikuwa mwisho wa dunia c ni mwehu huyu.soma(k.torat13.5) au torat 17.2-5, KADHI WEWE INAKUHUSU NINI?mambo ye2 waislam wewe yanakugusaje jifunze kuwa na akili we mchungaji ucye 2lia.kwanza unaönekana hata dini yako huijui.OIC NI KWAFAIDA YA WAISLAM NA NCHI YE2 KWA UJUMLA.mbona wewe vatcan ndo wachungaj wa katolik ndo wanauraia pia au hujui?
 
Chakachueni... Chezeni Ngoma ya Katiba muwezavyo.. tambueni hamtakaa hapo milele.. Tumekuja.. TUMEWASILI.. watanzania hawajalala kiasi hicho.. Ni katiba gani, ya nchi gani!! isiyojieleza yenyewe inavyoweza kubadilika au kufikia UKOMO wake..? kiasi kwamba jambo hili limekuwa la kupikwa kila kukicha na watu tunakusanywa.. tunaongea sana.. ingawa mchezo mnaujua ya kwamba mna-by time hadi kufikia next election.. JIULIZENI.. HOW FAR SURE YOU ARE kwamba mtashinda next uchaguzi.. Nionavyo mie.. Hata kama katiba haitabadilika, kushinda uchaguzi 2015 kwa chama kilichopo madarakani leo hii, kwa sampuli ya wananchi hawa waliopigika hadi kwenye mifupa sidhani!!!!!!!... kiasi kwamba hata protocal team zitakazopangwa kuchakachua matokeo zote zitakua na wanachama wenye mashati ya kijani ila ndani ya mioyo yao ni Opositions.
 
Katiba ni sheria mama ya nchi na hivyo inatakiwa ilinde haki za raia wote na rasilimali zao. Katiba haiwezi kuwa document ya kulinda interest za watu wachache ili waendelee kutawala milele na kujiwekea kinga za kutokushitakiwa hata baada ya kuhujumu rasilimali za wengi. Ujanja ujanja wa kuwatowashirikisha wadau muhimu katika mchakato mzima wa kuandikwa katiba mpya ni kutokana na ubinafsi wa wachache ambao wanataka kutumia udhaifu wa katiba kudidimiza haki za raia na kupora raslimali za nchi. Siwezi kuwa mnafiki kwa kuafiki mchakato wenye mlengo huo. Mstakabali wa nchi hii uko mikononi mwetu. Tuungane kwa dhati kupigania katiba shirikishi kwa manufaa ya wananchi wote wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo na si kwa manufaa ya genge la wabinafsi wachache.
 
kweli kazi tunayo,awa watawala wanachezea nguvu ya umma
na iyo siku ikifika shime wanainchi tunawaadabishe wao tu!!
sio turumbane sisi kwa sisi!!tusidangayike na awa mafisadi
 
yaan mm nashindwa hata nitoe vipi shukran zangu kwa mpango huu wa kutufungua macho
 
Katiba ya Mpya ya Tanzania haiwezi kupatikana kirahisi katika Mazingira haya ya Sarakasi gandamizi za Serikali zinazoendelea...!¡.. ni lazima Wananchi tufike mahali tujitoe mhanga na Kufanya Maamuzi Magumu..!¡..
 
tangazo:kutakuwepo na maswali na majibu kuhusu katiba hapa washington dc,kupitia redio ya demokrasia ya " wpfw 89.3.na pia tutalijulisha bunge la marekani wasikilize siku hiyo.kwani wao ndio wanoizinisha kutoa pesa kuja tanzania.sasa ndugu zangu kaane mkao wa kula ,mimi naitwa .ludigo mhagama kutoka wpfw,nitahakikisha kunakuwepo na external pressure kwenye hii issue muhimu .mungu ibariki tanzania.wataanzania tusiwe na woga hii ni issue muhimu sana.shambulia wanaangaika hao.bado kidogo sana tutawamaliza.katiba ndio bomu lao.sasa shikilieni hapo. Tuwasiliane kwenye 202 367 2761.
 
Back
Top Bottom