Hivi kama mswada unapitishwa bungeni ili bunge likaitungie sheria; tunaweza kutegemea matokeo yenye usalama kwa watanzania wote kweli? Kama iliweza kutokea, bunge lenyewe kutunga sheria kama hii;
1. Afisa mtendaji wa mtaa kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi na kozi ya muda usiopungua miaka miwili....
2. Dereva wa serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na kozi ya udereva wa muda usiopungua miaka miwili...
3. Mhudumu wa ofisi ya serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne pamoja na kozi ya waswala yanayofanana na uhudumu wa muda usipungua miaka miwili....
4. Mfungua geti la serikali kuwa lazima awe na elimu ya kidato cha nne na kozi ya uaskari wa muda usiopungua miaka miwili...
Lakini eti mbunge, anayesimamia serikali na watendaji wake; wakiwepo hao madereva, walinzi, nk. mwenye dhamana ya kujadili, kuhoji na kuidhinisha bajeti ya serikali, mwenye kutunga sheria zote nchini, nk ajue kusoma na kuandika kiswahili au kiingereza.....!
Kweli inaingia akilini? Sasa inakuwaje muswada wa kuandikwa kwa katiba mpya upelekwe kwa mtu mwenye ujasiri wa kudhubutu kutunga na kupitisha sheria kama hizo hapo juu? Tena aliyeapa kuilinda, kuitetea na kuitunza katiba iliopo....! Ataelezaje mapungufu ya katiba aliyoapa kuilinda, kuitetea na kuitunza? Binafsi ningependekeza muswada huu uletwe huku kwa wananchi, na kama nao wana kiu ya kuchangia basi wataipata hukuhuku uraiani....!