Wanawake ni mtaji wa ccm ili isife kwa kukosa maspika na mawaziri wa kuipigia kampeni inawekeza kwa wanawake kiujumla huu ni upuzi na ujinga uliomithilika tunataka kutawaliwa na watu wenye uwezo bila kujali jinsia na sio kuingiza pumba kwa visingizio vya jinsia tumeliwa kwenye uspika na kama watu hawajifunzi waendelee kukumbatia pumba za kina warioba za wabunge wawiliwawili
Sasa si ndio tunataka kuwasaidia mtoke vizuri; najua tukianza kudai serikali moja Zanzibar hawatokubali.. tukidai serikali tatu bado tutakuwa tunajaribu kuwaappease Zanzibar...
Tatizo wewe Mwanakijiji una akili sana lakini ujue jamaa wanapanua mianya ya ufisadi na uwingi wa maofisi ili kuajiri watoto wao, mashemeji na wajomba. Hivi nchi imeliwa mpaka imetoboka sasa ndio tuwe na mafastjet watatu tukione cha moto bora tuunde majimbo, Zanzibar iwe jimbo, bara pawepo majimbo kwa idadi ya jimbo moja sawa na idadi ya wazanzibari kisha tuwe na Raisi mmoja. Hakua haja kuongeza urasimu mpya na ubwerere wa matumizi hebu watupe mfano marais watatu au wanne wanatawala nchi gani duniani kama sio watu waliochanganyikiwa hawa.Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?
Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!
Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.
Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.
Na maneno mengine mengi....
In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
Sijui kwa nini bado tuna "flip flop" na suala la Muungano. Wote tunajua kuwa huu Muungano ni kikwazo kikubwa sana katika ku-design a good, an effective and a responsible governing system.
Kama siyo huu muungano wala tusingekuwa na system, au kujaribu hata kupendekeza system, ya utawala isiyoeleweka, even kufikia extent ya kupendekeza kuwa na ceremonial president.
Watanzania wapewe haki ya kujiamualia through a referendum. Waulizwe kama bado wanapenda kuendelea kuwepo kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kama hawapendi, basi na Muungano uvunjwe, kila mtu achukue times zake. Kama bado wanapenda Muungano uwepo, basi waulizwe wanapendelea Muungano wa aina gani.
Personally, kuendelea kupendekeza kuwepo Muungano wa serikali tatu, tena with a ceremonial president, ni kukwepa ku-address the core problems za Muungano wa sasa na kuendelea kuendeleza kiini macho cha Muungano.
Najaribu kufikiria idea ya kuwa na ceremonial president kwenye nchi ambayo viongozi wake waliochaguliwa kuwa accountable kwa wananchi, lakini wanafanya kazi zao in a ceremonial way. Sasa itakuwaje kama wakipewa full title ya kuwa ceremonial leaders?
Kwa nchi kama Tanzania, we need a responsible and accountable President, not a ceremonial president. Hatutaki kuwa na Rais ambaye kazi yake itakuwa ni kutembea na mikasi mfukoni kwa ajili kukata utepe kama anavyofanya Makamu wa Rais.
Kama vipi na tusiwe na rais wa aina hiyo kabisa. We aren't that rich to pay for someone simply for doing nothing.
kibanda maiti
Kwa Mtazamo wangu naona Tume imekurupuka katika mambo mawili.
1 Ni suala la muungano na serikali zake, Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusu Muungano hasa kwa upande wa pili (Zanzibar) kwa maoni yangu hapa nadhani lingekuwepo pendekezo la kupiga kura kuhusu muungano kama wanautaka au la na kama wanaunataka ni wa aina gani?
KUHUSU SERIKALI TATU.
Kama alivyosema ndugu Mwanakijiji kuhusu mzigo wa serikali tatu, napata shida kidogo kujua ni kwa namna gani serikali hizo mbili zitakuwa zinachangia katika serikali ya Shirikisho, kwa muono wangu naona kama kutakuwa kuna upande mmoja utakuwa unaelemewa (unanyonywa na upande mwingine) na hapa unaweza kuwa upande wowote ule either Tz bara au Tz Zanzibar, So kwa misingi hiyo tukisema tuwe na serikali moja ka anavyosema Ndugu Mwanakijiji ni jambo jema ambalo linapunguza matumiz makubwa katika shughuli za utawala na kupeleka gharama hizo katika matumimizi ya maendeleo, LAKINI tuwe wa kweli Je ni kweli Wazanzibari watakubali serikali yao "kufa" ili kufanikisha kuwa na serikali moja? Hasa ukizingatia kwamba kila kukicha wanapigania kupata mamlaka kamili? Tusubiri tuone.
2. KUHUSU BUNGE
kiuhalisia binafsi napinga kuwa na wabunge wawili kila jimbo (Mwanamke na Mwanaume) na hii ni kwasababu haya ni matumizi mabaya ya fedha za walipakodi, hii ni demokrasia ambayo hata kwa mabwana wakubwa ambao walituletea sisi mfumo wa demokrasia na haki sawa kwa wote haupo. Kwa mtazamo wangu Viti maalumu vifutwe na huu utaratibu wa wabunge wawili kila jimbo ufutwe na abaki mmoja kama ni mwanaume au mwanamke wote wapambane na atakayeupata ubunge ndo huyo tuachane na huu mfumo majimbo yenyewe yapo zaidi ya 200 so ukizidisha mara 2 ni wabunge zaidi ya 400 hii kwa kweli hapana hapa warioba anataka kuwatafutia watu ulaji.
Ni Mtizamo wangu kama Mtanzania.
SERIKALI YA TANGANYIKA NA YA ZANZIBAR
101.(1) Kutakuwa na Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar ambazo zitakuwa na mamlaka katika Tanganyika na Zanzibar juu ya mambo yote yasiyo ya Shirikisho kwa mujibu wa Katiba hii;
(2) Serikali ya Tanganyika na ya Zanzibar zitaundwa na kutatekeleza madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii na Katiba ya Tanganyika na Zanzibar;
(3) Kiongozi Mkuu wa wa Serikali ya Tanganyika na pia Kiongozi Mkuu wa Serikali ya Zanzibar ataitwa Gavana wa Tanganyika na Gavana wa Zanzibar;
(4) Kutakuwa na kiapo rasmi cha Gavana wa Tanganyika na cha Gavana wa Zanzibar kitakachosimamiwa na Jaji Mkuu wa Tanganyika na Jaji Mkuu wa Zanzibar ambapo viongozi wote wawili wataapa kuitii, kuilinda na kuitetea Katiba hii, kiapo cha utii mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Shirikisho la Tanzania, na kiapo kingine chochote kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar.
102. (1) Magavana wa Tanganyika na Zanzibar watachaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Tanganyika na Katiba ya Zanzibar;
[h=5]Sema hapana Serikali "Tatu", Sema ndiyo "Serikali moja". Nchi moja, Taifa Moja, Watu wamoja - nje ya hapo Hapana!!! Tumeshatengeneza ulaji na ukiritimba wa kutosha kwenye serikali mbili halafu tunataka kuongeza serikali ya tatu? Mizigo miwili midogo imetushinda (tunahangaika nayo) halafu magenius wetu wanataka kutupa mizigo mitatu mikubwa!? Kwanini tusiamue kutengeneza mzigo mmoja tu tukaubeba!?[/h]Pamoja na jaribio dhaifu la Tume ya Warioba kupendekeza kuikataa majimbo, pendekezo lao la Katiba Mpya kimsingi linatengeneza majimbo yale yale (States) ambapo kutakuwa na majimbo mawili - Tanganyika na Zanzibar! Kwa sababu kama nchi mbili zimeungana na kuunda 'Shirikisho" basi zile zilizoungana haziwezi kuendelea kuwa nchi tena; zinahamisha hakimiya (sovereignty) yake kwenda kwenye federal government isipokuwa kama kilichoundwa (Shirikisho) siyo nchi!
Kwa kuanzisha mfumo wa Majimbo - Jimbo la Tanganyika litakuwa na nguvu kubwa sana kuliko jimbo la Zanzibar. Lakini kama wakiamua kufanya hali ya sawa katika kuendesha serikali ya Jamhuri ya Muungano Zanzibar itaonewa kwani ikitakiwa kuchangia nusu ya gharama za kuiendesha serikali ya Muungano italalamika mno na sidhani kama Wazanzibari watatakiwa kukubali mfumo huo.
Kwa sababu hiyo njia ya kuimarisha "Muungano" kama lengo ndio hilo basi ni kuingia Serikali Moja ya Kitaifa na Nchi Moja - siyo serikali tatu za kitaifa. Chini ya serikali hiyo moja ya kitaifa (federal government) kutakuwa na serikali za Majimbo (States) ambapo Zanzibar itabakia kama ilivyo (Visiwa vya Mafia, Bagamoyo, Pangani vinaweza kuongezwa huko... I know.. I know.. au ikagawanywa Unguja ikawa kivyake na Pemba kivyake!.) halafu Tanganyika igawanywe kwa States saba hivi ambazo zitaunda 'Regional Governments). Chini ya Regional Governments kutakuwa na "Local Governments" za Miji, Majiji, Vijiji na mifumo mingine ya kujitegemea.
Na maneno mengine mengi....
In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
!
In short.. Tusikubali serikali tatu za nchi; bali serikali moja, nchi moja, taifa moja na watu wamoja.. Mapendekezo ya Tume ya Warioba kuwabebesha Watanzania mizigo hii ni ya kupingwa, kukataliwa na kupuuzwa.
Kitu cha kijinga zaidi ni uwepo wa mawaziri zaidi ya kumi wakishughulikia mambo saba. Mambo saba wizara 15? Haiwezekani.
Mbona rasimu haijasema pesa za kuendesha hizo serikali zitachangiwa katika mfumo gani ?