Muungano: Maalim Seif aipa tume ya jaji Warioba masharti

Mimi nawashangaa mnaong'ang'ania Muungano. Tuwaunge mkono Wazanzibari waende zao haraka sana. Tudai na sisi Tanganyika yetu badala ya kukimbizana na kivuli cha Wazanzibari. Kwa hili nawaunga mkono Waliberali 100%
 
Nadhani hakuna mtu anayeweza kupinga muungano kwa maana ya neno na nia ya tendo lenyewe. lakini mtu anaweza kupinga Muungano wa tanganyika na Zanzibarau au muungano mwingine kwa mantiki ya muudo na faida zake kwa kila upande. Ikiwa kama hilo la kuukataa muungano litatokea Watanganyika tuwaachie wazanzibari waamue sisi tukae kimya na uamuzi wowote watakaoamua kama ni kuuvunja au kuendelea nao tuukubali nasi tutabaki salama kama alivokwisha sema mwalimu.
 
Kuna kitu Zanzibar hawakielewi, ila woga wao wa kujitegemea unawafanya kuendelea kung'ang'ania vitu.
Ni hivi, sisi hatutaki aina yoyote na muungano nao, hivyo waituambie habari za Muungani, sisi hatutaki kabisa kuwepo na muungano, na maadam wao wameamua kujitoa na kubeba hilo bango la kujitoa, basi wajitoe jumla badala ya kuleta aina za miungano mezani.
Wanang'ang'ania nini kuwa na sisi, mpaka wanaa kutuletea aina za miungano....wanaogopa ku-stand alone? basi waache kelele.
 
Bahati mbaya upande wetu Tanganyika hakuna hata kiongozi mmoja anaweza kujitokeza wazi na kuyasema kama Mtanganyika nao wanaitaji nini katika huu muungano huu kama uendelee huwe wa aina gani na kama uvunjwe kila nchi ibaki na kwake.
Hapa Seif anatetea nchi yake iwe kamili mimi binafsi naungana naye amekuwa muwazi zaidi tatizo kwetu Tanganyika kwa nini viongozi wetu wanawalazimisha watu wa nchi ingine kuungana, viongozi wetu wana maslahi gani ni huu muungano mbona hawasema wapo kimya tu huku wakitumia nguvu nyingi kuulinda.
 

Mkuu wote waliochangia hakuna hata mmoja aliyetoa matusi,wamejitahidi kutoa maoni yao,nashangaa unamshambulia mtoa hoja badala ya kushambulia hoja.
 
Yupo sahihi Mliberali wawaachie Zenji yao mana sioni umuhimu wa Muungano huu ambao wabara hawanufaiki nao na wavisiwani wanadai hivyo hivyo sasa anaenufaika na Muungano ni nani? Kweli akili kumkichwa.
 

Hadidu rejea za warioba ni marufuku kuuvunja.
 
Huyu yakhe atupshe mkapa yupo wap akamtandke kwa ffu naskia yeye na karume ni uamsho
 
Kukata mzizi wa fitina hapa ni kura ya maoni iitishwe, wazanzibar wote wapewe fursa ya kutoa maoni yao iwapo wanakubaliana na muungano au la. Kikwazo ni kwamba ccm inaliogopa hili kwa kuwa ina uhakika wazanzibar hawautaki muungano na watapiga kura ya kuukataa. Badala yake wanaamua kuwatawala kimabavu tu.
 
Nguruvi3,

..wa-Znz wameweka ya kwao mezani.

..na sisi wa-Tanganyika tuweke ya kwetu mezani.

..suala la ardhi, Maalim Seif amelielezea ktk taarifa waliyotoa baada ya kongamano lao.

..kwa upande wangu madai ya kina Maalim yanabeba 90% ya matamanio yangu.

..naunga mkono msimamo wa Maalim Seif na wenzake.

cc: Barubaru, THE BIG SHOW, takashi, GHIBUU, Nonda
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nakuomba nikusumbue kupata majina ya hiyo tume ya maridhiano na hadidu za rejea kwa tume ya katiba. Nilikuwa 'offline' kwa wiki moja hivi.
 
Nadhani wangekuwa sasa kusema Muungano wa Jamhuri za TanZania, kwani hapo (bolded) pana tofauti ya tafsiri.
 


Mimi Pia namuunga mkono Maalim Seif kwa asilimia mia moja,

Ila nachokiona mimi kama Mtanganyika ni kwamba kama tumeamua kuuvunja basi tusiwe selective katika namna ya uvunjaji,Maalim Seif asiwe selective,

Kwa mtazamo Wangu mimi Mkuu JokaKuu ni kwamba kila upande uchukue 50 zake kivyake vyake,

Maadam Zanzibar wanaona wamebanwa na huu muungano basi waamue kwa amani kuondoka na sisi tuwaache kwa amani waondoke,lakini sisi tusitake chochote kutoka kwao,na wao wasitake chochote kutoka kwetu,,

Yaani tuuvunje muungano katika kila nyanja,tuifanye zanzibar kamavile tunavoichukulia nchi nyingine mfano kenya,uganda n.k,,maingiliano ambayo yapo na ya kihistoria tutajua namna ya kuyapangilia ili tuendelee na maisha yetu kama kawaida...
 
Last edited by a moderator:
..wa-Znz wameweka ya kwao mezani.

..na sisi wa-Tanganyika tuweke ya kwetu mezani.
Nina wasiwasi kuwa Watanganyika (with all respect to them) bado hawajawa na ujasiri wa kuanzisha makongamano na kuweka ya kwao mezani, sanasana wataishia kwenye "meza za mitandao".

Mpaka leo bado kuna Watanganyika (no offense) wanaotegemea Warioba na tume yake kuleta mabadiliko ya Muungano!
...si rahisi kama unavyofikiria JokaKuu
 
Mtu akiondoa vihasira kwa sababu yoyote ile, kwa mbaaali, hichi kipengele (2.Kubadili jina la muungano kutoka Jamhuri ya watu wa Tanzania na kuwa muungano wa Jamhuri za Tanzania) kina mantiki: Kinakuwa kama kinaomba federalism, na federalism haina tatizo as such. Tatizo linalokuja ni kwamba Maalim kachanganya vitu kwenye madai. Huwezi kuomba federalism halaf ukaomba na uraia wa pekee, na uwakilishi wa kimataifa wa pekee. Hii ni kama kuchanganya chumvi na sukali kwenye chakula hicho hicho; so confused! Polisi, bendera, baraza la mitihani la pekee, hivi vinaelezeka kujitenga ndani ya federal states. Lakini si uraia na uwakilishi wa kimataifa.



 
Mimi ni Mtanganyika na ninasubiri kwa hamu hiyo siku Tanganyika yetu itakaporejea. Kwa mantiki hiyo, ninamuunga mkono Maalim na Wazenj wote na Walibelari wote kudai Zanzibar huru. jamani tuwaunge mkono maana siku Zanzibar itakapopata uhuru wake, moja kwa moja na Tanganyika itakuwa imerejesha uhuru wake. Ushauri wa bure kwa akina Maalim na Walibelari: vunja ndoa na CCM, unga mkono harakati za ukombozi wa pili wa Tanzania zinazoendeshwa chini ya uongozi wa CDM na M4C yake mtakuwa mmejihakikishia uhuru wenu. Muungano kama ulivyo leo hii ni mradi wa CCM kuendelea kuhodhi utawala. As long as mnaendelea na ndoa ya CUF + CCM (sijui kama ni ya jinsia moja au tofauti), basi hizo ngonjera zitabakia hapo hapo Kibanda maiti!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…