Kwa mwenye akili na kama ungekuwa nawe unazo basi ungeuliza kwanini hilo pendekezo lako linanawashindeni kulitimiza.
 



isipokuwa pana jambo sisi wa kawaida hatulijuwi.
 



Harakati za kudai haki mnazibatiza kuwa ni kuvunja Muungano. Kwa hilo ni hiari yenu lakini haki si mafuta tu na taratibu tutafanya hivyo kwa vitu vyengine . Hizi lugha za kututisha na Muungano ni hollow, hollow hollow. tunataka haki ndani ya Muungano na mnapohisi kuwa haki hiyo mtaitowa kwa kuvunja Muungano you can do this instant bila ya kungoja kesho na mambo mnayotutisha eti kuuwana na kufa njaa haya yapo hadi sasa. Hili la kuuwana tunafanyiwa na wenzetu kwa kutuletea majeshi kufanya hayo mauwaji na suala la njaa linafanywa na nyie wenzetu kwa kutubana hata kwa rasilimali zetu.
 

Hata mimi nilifundishwa shule kuwa bazazi huwa anaelewa ukweli wa jambo lakini akajizunguusha.
 

Bottom line ni kuwa WAZANZIBARI WANAJADILI KILICHO NDANI YA ZANZIBAR> SIFIKIRI TUNAHITAJI KUWA MAPROFESA KUNGAMUA HILO>
 
sisi kina nani? u mean CCM bara ndo wanataka muungano zaidi? as far as am concerned wananchi wa kawaida hatuna mshawasha wowote na muungano.

Tulio wengi humu ndio sie wananchi wa kawaida na wenngi wetu si CCM lakini tunaotukanana na kukebeheana humu ndani ni sie
 


kwani almasi na dhahbu zenu mnazitia kwenye vikapu? Si mnagawa tu? Tuachieni nasi iwe zamu yetu kugawa. Towa boriti kwenye jicho lako ndio utaweza kutowa kibanzi kwa mwenzako.
 

Inashangaza kuwaambia wenzako wanaongelea wasichokijuwa na wakati kama kufanya hivyo ni ujinga basi wewe umeupita.
Umesahau kuwa huyo JK angekuwa ameshamaliza muda wake zamani kama si hiyo Zanzibar? Umesahau kuwa huyo Jk asingekuwa madarakani hivi sasa kama si Zanzibar kumwangusha Salim. Ni tabu kujifanya unajuwa bali ni raha kukubali kuwa hujui jambo.
 

Inashangaza kuwaambia wenzako wanaongelea wasichokijuwa na wakati kama kufanya hivyo ni ujinga basi wewe umeupita.
Umesahau kuwa huyo JK angekuwa ameshamaliza muda wake zamani kama si hiyo Zanzibar? Umesahau kuwa huyo Jk asingekuwa madarakani hivi sasa kama si Zanzibar kumwangusha Salim. Ni tabu kujifanya unajuwa bali ni raha kukubali kuwa hujui jambo.
 




usiandikie mamate........
 
wazanzibar wanataka tuwaache na matuta hewa..watakoma baada ya kuvunja muungano...pemba nao wakajitenga na mafuta yao....alafu nao mwisho wa siku wakashindwa kuyapata...

watanganyika msijali ...mafuta tanganyika yameshapatikana kwa wingi.........

Kama ilivyokuwa kwa Almasi , dhahabu, gesi na madini mengine mafuta yenu hayatawasaidia Wazanzibari kwani sasa ukiondowa hayo mafuta si mnayo madini na mnatumia wenyewe?
 
zanzibar pia hakuna upinzani ...kuna mgawanyiko..pemba ..CUF,unguja ..CCM...

huwezi kuiita hiyo kuwa ni hali huru ya kisiasa.....ningeita hivyo kama pemba ccm na cuf wangegawana nusu..na unguja vile vile..lakini sasa hatuchekani...


Buisara ingetumika kujadili kitu unachokijuwa kuliko kusikia masikioni tu.
 

Post yako yako naikubali na ina viashiria vilivyo sahihi lakini umesahau kuwa hata hao viongozi wa CCM Visiwani wameshachoka na kubanwa sana na Muungano kwa vile watu wanaowaongoza wanazidi kudidimia kihali kila siku.
Si kweli kuwa mwananchi wa kawaida haupendi muungano lakini Muungano unamsukuma mwanannchi kwenye kona na hivyo juu ya udhaifu wake atapigana na Muungano.
CCM haiwatoshelezi viongozi wote wa Zanzibar na badala yake vijisenti vinabidi vigawiwe miongoni mwao. Unaonaje iwapo donge nono litakuja directly mikononi mwao? Wanafahamu kuwa kwa mfdumo wa sasa unawanyima fursa ya kutekeleza njia za kupata kipato kikubwa. Hivyo ndani ya hiyo unayofikiriunkuwa ni kujitafutia umaarufu kuna element ya kutaka kupata uhuru wa kujitafutia kipato kwa ajili ya Zanzibar directly kwani wanajuwa kuwa kipato hicho kitawapa fungu kubwa zaidi kama ilivyo kwa wenzao wa Bara.
Kelele unazozifikiri kuwa za kujigamba zinaweza zikawa ni harakati za kweli za kuondokana na hali ya sasa hivi iliyozingirwa na kunyimwa fursa na njia zile zile zinazotumiwa na wenzao Bara kujipatia kipato cha Zanzibar ambapo wao watakuwa na mgao mkubwa.
 
kama hamuamini wazanzibari wamechoka kutawaliwa na Muungano here is the litmus paper, just wapeni fursa wafanye uchaguzi huru wa viongozi wanaowataka, naaapa kwa dini jina la Mungu mmoja, kitu CCM kitakuwa history zanzibar.
 
kama hamuamini wazanzibari wamechoka kutawaliwa na Muungano here is the litmus paper, just wapeni fursa wafanye uchaguzi huru wa viongozi wanaowataka, naaapa kwa dini jina la Mungu mmoja, kitu CCM kitakuwa history zanzibar.

Hapo umawakanyaga kwenye donda ndugu 😀 watapita wakilalamika njia nzima.
 


Pakacha, uhali gani gani? Kwa hadidu rejea hizo hizo unazotaka wewe hebu fikiria kwa Zanzibar ukiondowa huu umri wetu nani hakufanya makosa katika hali hii tuliyomo sasa ya Muungano? Karume Mkubwa ndiye alieiuza nchi kwa kuhofia kuondoshwa madarakani. Watu kama Seif Bakari waliwauwa wenzao kwa kupinga muungano huu na baadae wao wenyewe walipotanabahi na kuidai haki wakafungwa. Aboud Jumbe aliiuwa ASP na kuipeleka Zanzibar Tanganyika na alipotanabahi akataka kujitowa kwenye muungano nae akaangamizwa.Wazanzibari wenyewe walishangiria kuuliwa ASP baada ya kuona inawabana Kidemokrasia na wakiwaonea choyo Watanganyika, sasa kweli imedhihirii wanaitaka ASP irejee, Seif Sharifu na kundi lake walimsaliti Aboud Jumbe nao walipotanabahi wakapigwa na chini. Marehemu Dr Ali Juma aliwasaliti Wazanzibari kwa nafasi ya Umakamo wa Rais na mungu amempenda hakuwahi kuvuna usaliti wake. Salmini aliwatia uhaini wenzake kwa kudai hadhi na haki ya Zanzibar nae aliishia kivyake. Na hata Karume Mdogo (Amani) alipopewa madaraka akaipeleka Zanzibar Tanganyika na sasa anarudi kiguu nyuma.
SASA nieleze kati ya Wazanzibari ukiondowa Generation hii mpya nani hana mkono wake katika kuifisadi Zanzibar kwa kisingizio cha Muungano na nani mwenye haki na asie na haki katika kuitetea nchi yake? Pakacha mrengu wako pengine ndio waliokosa sifa za kutetea haki za Zanzibar kwa hili la mafuta kwani ni nyie mnaofadhiliwa na hao mnaowaambia kuwa waachane na mafuta yenu. Nina hofu kuwa mrengu wako hamko serious na hili jambo kwani ni nyie mnaowapa uwezo wa kuwa na sauti kwa kitu kisicho chao. Kauli yako ya kubaguwa wapiganaji wa haki hiyo inathibitisha kuwa mnafanya kiini macho kwa Wazanzibari wenzenu. Kinyume cha hayo hebu wachieni Wazanzibari waamue kwa haki katika uchaguzi unaofuata na muweke nguvu ya pamoja katika kudai haki yenu.
 
Nakupongeza swahib kwa bandiko lina mengi ya kutukumbusha na kuwaeleza wachangaaji wengine wasiyoijua kadhia ya Zanzibar. Sawa na tuwaachie Wazanzibari waamue kwa haki katika uchaguzi ujao- lakini hiyo ni pamoja na kutotutumia opinion leaders (wazee) kuwatisha na kuwashurutisha watu(hasa vijana- new generation) kule Pemba waipigie CUF. na waachwe huru kabisa. Jengine hao viongozi waliowahi kufanya makosa ndio ninasema tuachane nao - tena kwa mirengu yote. Kwani hivi CUF hawana wengine zaidi ya Seif? au hawapewi nafasi tu. Huo mrengu mwengine wanabadilika kila mara au huoni? Wafanyao makosa hawarudi (Dk. Bilali hakurudi!!!!!!)-ingawa makosa hayakuwa yake ya moja kwa moja.
 

PAKACHAjamaa yangu usiwe rahisi hivyo wa kujitia mitegoni. Nini kosa la Dr. Bilali? kufuata mkondo wa demokrasia? Hivyo huoni kuwa unapalilia kile unachowakosoa wenzako? Kwa hatuwa ya mwanzo nani alikuwa chaguo la Wazanzibari kwa mujibu wa katiba yenu? La pili kwanini mlikubali kuteuliwa mtu aliekuwa si ridhaa yenu? La tatu nyinyi ni chama chenye demokrasi kubwa,iweje mumuone Dr Bilali kuwa ni mkosa kwa kufuata taratibu mlizojiwekea? Na kama mmeshampa mtu miaka mitano na akashindwa kuiongoza nchi kwa nini mkazanie abaki tu eti amalize miaka kumi? Hii si sawa na watani wenu CUF wanaomweka mtu huyohuyo kwenye chaguzi zote?
Kuhusu suala la kubadilisha viongozi naona bado hamjafanya hivyo na kinachofanyika ni kuwa mtu akishapewa urais miaka kumi katiba inamzuia kuendelea kinyume cha hivyo mgekuwa mkiendelea na hao hao. Hebu niambie kina Ali Ameir, Mohammed seif khatib na wengine mnawangojea wafe madarakani kwa vile hamna wengine wa kuchukua nafasi zao?
Nakushauri jamaa yangu muache kupanga nani ni mzanzibari zaidi ya mwengine ili mfanikiwe katika harakati za kudai haki zenu.
 
Tatizo la Zanzibar ni kuwa ile jamii yenyewe bado haijajikomboa. Uchaguzi ni kweli hauwi huru -kwa maana ya huru- Wengi wa wapiga kura hawapigi kura kwa mujibu wa ridhaa zao. Hii kwa pande zote wanaoipigia CUF na wanaoipigia CCM. Wapiga kura wanapiga kura kutekeleza misimamo inayowekwa na hao "opinion leaders" (wazee) Na ndiyo maana ya CUF kushinda siku zote Pemba- na CUF hiyo kushindwa kuambulia kitu Kaskazini Unguja na Kusini Unguja. Sasa nafikiri tuwe na system ambayo itafanya wapiga kuira(hasa hao new generation) kuwa huru kweli. Lile suala la nguvu ya Dola si la kweli Bwana. CUF hawana nguvu ya Dola -kwa nini wanashinda Pemba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…