Mzee Mwanakijiji umenikuna! Hawa Wazanzibari wanaota ndoto za mchana za utajiri, sasa wameipata. Ooh Mafuta ya Zanzibar ni ya Zanzibar; mara Ooh zama za kutishana zimeisha, Ooh mafuta ya Zanzibar hayaendi bara mpaka dhahabu ya Mwanza igawiwe Zanzibar! Hawa wala tende wana matatizo kweli kweli! Wanasema hayo huku bara tukilipia starehe zao zote kwa fedha itokanayo na pamba, mpunga, chai n.k. Zama za kuwabeba Wazanzibari zimekwisha - tuwaachie Zanzibar yao ndogo kama wilaya ya Pangani lakini yenye Rais, Waziri Kiongozi, Naibu WK, mawaziri na manaibu wao 40, wakurugenzi na makatibu wakuu zaidi ya 100, viongozi wa siasa zaidi ya 5,000! Kisiwa cha viongozi! Kalagha bhao!
Kwa mwenye akili na kama ungekuwa nawe unazo basi ungeuliza kwanini hilo pendekezo lako linanawashindeni kulitimiza.