He he he he ! bi Zenj anataka abebwe he he!
 
Binafsi huwa sioni faida za hii ndoa, bora ivunjike tu, kwanza mizigo wanatubebesha, kaeneo kadogo kama mkoa mmoja wa bara, lakini kila kitu kanataka mgawo kama nchi kamili!

Ingekuwa mie talaka tatu ningetoa mara moja!
 
wabara ndio wanaoungangania huu muungano Zanzibar hawautaki

Hata Wabara hatuutaki, wanaong'ang'ania ni Viongozi ambao hawana vision hawataki kusikiliza maoni ya Wananchi na wanaung'ang'ania ili kulinda maslahi yao. Hakuna chochote ambacho Wabara tunafaidika kutokana na Muungano huo.
 
Wanaotakiwa kudai serikali ya Tanganyika ni Watanganyika wenyewe na si Wazanzibar.

Mkuu Madela Wa- Madilu hapa umemaliza. Ni ajabu Wazanzibar kudai bara wawe na Serikali inawahusu nini? Wenyewe tumeridhika na Serikali ya muungano kama nao wanatamani si wavunje SMZ ili tuwe na Serikali moja tu?
 
he! Mbona hivyo wewe.
 
kinachofurahisha kuwa yale makelele tuliyokuwa tukipiga juu ya muundo wa muungano kupitiwa upya sasa yamesikika mpaka viongozi waandamizi wa SMZ wameona kuna umuhimu huo sasa, wameona kuwa kumbe jamaa si wenzetu kama tulivyokuwa tukidhani na wana tumia muungano kupata miradi yao na kudumsha ustawi wa matumbo yao tu, huku wazanzibar wakikauka wakavuuu.eti muungano!
 
kama hawautaki si waondoke sisi tujiunge na visiwa vya Comoro?

Kwani Tanganyika peke yake haiwezi kuwepo bila kuungana na nchi nyingine? Baada ya Zanzibar then Comoro? Why not Kenya and Rwanda kam basi ni lazima?
 
MOJA WAPO YA matatizo makubwa kule Zenj ni uvivu ulio kithiri.
Hawalimi maana wanasema si jadi yao ni ya WATWANA kulima.Kila aliyepo anataka kufanya biashara ya kununu bidhaa nje na kwenda KUUZA BARA.
Ardhi ya Zanzibar na Pemba , hasa Pemba ni nzuri mno kwa kilimo.Katika miaka ya 80 Mzee Kawawa alipo watembelea kule Pemba risala ilisomwa kuwa wanasikitika kuwa ski hizi(siku hizo) wanyamwezi hawaruhusiwi au wamepungua kuingia Zanzibar. Hivyo kilimo kimeathirika.Mzee Kwawa alishangaa sana na kuwa uliza kuwa , hivi nyinyi hamli mpaka mlimiwe.
Hiki ni kielelezo cha utegemezi kwa upande wa bara ambako vile vile kuna umaskini wa kutisha.Sasa ukimtegemea mtu/taifa jingine wakati wewe mwenyewe hujifanyii maendeleo yoyote ndio mwanzao wa kudai talaka kwa ajili ya kukosa matunzo.
Suala la kutenga na Zanzibar linaweza kuwa si suluisho la kudumu kwa matatizo ya Zanzibar maana baada ya matatizo haya ya reja reja bado kunatatizo kubwa sana la tofauti kubwa ya Zanzibar(mainisland) na Pemba.
Mimi nejihakikishia kuwa muungano ukivunjika leo wawili hawa hawaivi chungu kimoja.
 
Taabu kubwa Visiwani ni watu wavivu ktk kazi!!!

Kubwa Visiwani wanalojua ni Kulalamika tu na kuomba msaada!!!
 
watu wanashindwa kuelewa hizi mada wahuruju tu! wazanzibar hawakusema muungano uvunjwe, walichosema na mimi nawaunga mkono kuwa mfumo wa muungano una matatizo na unahitaji kurekebishwa, nyinyi mmeshika uvunjwe, vp? sasa na huyu naye(Lole Gwakisa) eti tatizo wazanzibar hawalimi!? hii inahusiana vipi na matatizo ya muungano? Muungano ndo unafanya hali ya maisha ngumu visiwani hayo unayoita mambo ya kuuza na kununua yote yameuliwa na mfumo huu mbaya wa muungano ndo maana wazanzibar wanapiga kelele urekebishwe siyo uvunjwe,mkitaka uvunjwe hilo ni lenu wenyewe wanzanzibar wapo tayari itakavyo pigwe wao watacheza hawana tena cha kupoteza ispokuwa matatizo yaliyowazonga na shida za maisha zinazoletwa na mfumo mmbovu wa muungano.
 
Taabu kubwa Visiwani ni watu wavivu ktk kazi!!!

Kubwa Visiwani wanalojua ni Kulalamika tu na kuomba msaada!!!
kazi zenyewe zipo? nyinyi mkiletwa huku kuja kupiga kura na chama chenu cha Mafisadi hamrudi makwenu mnahamia kila pahala mnajipachika tu...........aaaaagh.
 
sasa ole wake mtu 2010 mtu aje alete pua yake huku, kupiga kura.........CCM, tapikwa supu anywewe....ya popo bawa yatakuwa madogo.
 

Jana usiku niliona yule waziri Khatibu akitoa maelezo kuhusu mafanikio ya muungano na jinsi walivyotatua kero za muungano katika channel ya TBC1. Ni mzanzibari huyu ambaye anasema kuna mafanikio makubwa katika kuuimarisha muungano. Wenzie wanasema uvunjike. Ni vurugu mechi tu maana wazanzibar hawautaki huu muungano. Nakubaliana na wanaosema ni muungano unaolazimishwa na viongozi wetu kwa maslahi yao. Ndiyo sababu kamwe wananchi hatutaruhusiwa kuamua kama tunauhitaji au vipi, au pia kama uboreshwe vipi?
 
kwani mzenji alipo olewa alipewa haki ya KUACHA?

Akerwe huyo Mume tu, mpaka atowe Talaka! vinginevyo, kelele za mlango .......
 
ENGLAND ,scotlland ,welsh (UNITED KINGDOM)(BRITISH)kila mmoja kati yao wanaenzi chimbuko lake.chakushangaza UNITED REPUBLIC OF TANZANIA (TANZANIA) MZANZIBAR anauenzi chimbuke lake la uzanzibari wake huku MTANGANYIKA hataki kusikia au kuitwa yeye ni mtanganyika.how sad is that ??
 


Rais wa Muungano wa Tanzania ni Jakya Mrisho Kiwete, Rais wa Muungano waEU anaitwa nani?
 

Baraza la Wawakilishi lina CCM wengi kuliko CUF na ukifuatilia huyo Seif alikuwana conciliatory tone kuliko hao CCM.
 

Message sent lakini ni bunge hilohilo Pinda alpata kigugumizi na 6 akatowa vitisho. Sio kweli kuwa hawawezi kusema lakini hawapewi ruhusa.
 


Kama tungekuwa na tabia ya mtu kujiamulia jambo linalomuhusu basi tungekuwa Wastaarabu lakini hili halipo na ndio maana Wazanzibari wnaamuwa kuwalisheni dawa ile ile mnayoitumia nyie YA KUINGILIA MAMBO YASIYOWAHUSU>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…