Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Hakuna anayechukia Znz au maendeleo yake, watu wanachukia unafiki wa wznz! mfano wameanza harakati za kuvunja muungano kitambo tu, lakini kwa unafiki hawatamki, wanafanya mambo uani uani tu!

Harakati zipi hizo ? Maana isiwe unalinganisha kampeni za mabadiliko ya Katiba ,kura ya maoni na mambo mingine ambayo huwa yanazungumzwa juu ya meza ,hivi unafahamu kama kuna wakuu wanashughulikia ziitwazo kero za Muungano kwa zaidi ya robo karne na hakuna linalofikiwa hata moja ? Hakuna jambo linalofanywa uwani yote yapo na hutokea watu wakajibizana (wakubwa) ,kumbuka Pinda alipokurupuka na kusema Zanzibar sio nchi. Wazalendo wengi hawakuipendelea kauli ile na kumuona ni mtu aliejaa dharau ,ingawa baadae alijutia na mambo kupozwa na Kikwete kiaina.

Wazanzibari wanajaribu kujipanga katika mambo yao bila ya kuisumbua katiba ya Muungano na pale palipoonyesha mgongano wametaka parekebishwe sasa ikiwa panaweza kurekebishwa inakuwaje mnakuja na maneno yasio na mpangilio kwamba wazenji wanataka kuvunja Muungano ,Hivi watauvunjaje Muungano wakati Tanganyika haipo ?
 
Harakati zipi hizo ?
Wazanzibari wanajaribu kujipanga katika mambo yao bila ya kuisumbua katiba ya Muungano na pale palipoonyesha mgongano wametaka parekebishwe sasa ikiwa panaweza kurekebishwa inakuwaje mnakuja na maneno yasio na mpangilio kwamba wazenji wanataka kuvunja Muungano ,Hivi watauvunjaje Muungano wakati Tanganyika haipo ?

Tuna wimbo wa taifa, wakaenda uani na kurudisha wa zanzibar kinyemela! Bendera ya taifa, wakadai sarafu,chama cha mpira,katiba yao n.k.
Kama hakuna Tanganyika znz iliungana na nai? soma sentensi zako zinajichanganya na sijui kama umegundua hilo.
Swali kwako Mwiba.
Je unapenda muungano au ungependelea muungano uvunjike?? Tafadhali nijibu
 
Actually sisi kama watanzania hasa wenye uelewa tuna sababu ya kusimama na kuitetea serikari yetu ya muungano.Kilichotufikisha hapa ni mfumo wa chama tawala ambao wengi wetu tunahisi tukibadilika hatuwezi kusonga mbele.Watanzania octoba hiyo,kumbukeni ni ujinga kukumbatia JIWE:
 
Ndugu wana JF ,napenda kuwauliza ,hili suala ambalo linaonekana kuchangiwa na kutetewa na watu wa aina kwa aina, hivi ni nani anaepaswa kuitetea uwepo wa serikali ya Tanganyika ,Zanzibar na Hii serikali ya Muungano ?

Karibuni vyama vyote vya upinzani vinasema ikiwa vitashinda basi vitahakikisha kuwa zinakuwepo serikali tatu ,kwa maana kuu kuwa serikali ya Tanganyika ,serikali ya Zanzibar na serikali ya Muungano ,zinakuwepo kikamilifu.

Hapa ukumbini nimeona waZanzibari wanapojaribu kujadili mambo au wanapoweka wazi mambo ya Serikali yao ,kunatokea watu hufanya nongwa na kukasirika vibaya sana kama vile kumesemwa tusi au maneno yasiyostahili kusemwa,kwa ufupi wengine mnaonekana kama kuchanganyikiwa na mnapoteza muelekeo.

Ajabu kwamba nyie msiekuwa na serikali mnakuwa wakali sana kwa kuonyesha kuitetea serikali ya Muungano serikali ambayo hata WaZanzibari inawahusu ,tena wao inawahusu zaidi kuliko nyie wengine ambao serikali yenu, nikimaanisha ya Tanganyika haipo,mlipaswa kukaa kimya ,WaZanzibar wanapanga na kurekebisha yale ambayo wanaona yanafaida kufanyiwa hivyo na wanafanya hivyo kwani wananyo haki kamili ya kufanya hayo.

Haionekani kama mnachangia au kuonyesha kuwa mnajali yale ambayo WaZanzibari wanayafanyia ukarabati zaidi ya kuonyesha kuwa mnachukia au hamupendi kuona maendeleo yao.
Mkuu unachoshindwa kuelewa ni kwamba wabara wengi wanazungumza kwa sababu wao hawana serikali yao na hakuna mtu anayefikiria kwamba hata wao bara wanataka sana kuwa na hicho kidogo mlichokuwa nacho nyie.

Isipokuwa kutokana na makubaliano ya Muungano wameshindwa kuweka madai yao wazi kwani mara ya mwisho walipojaribu hivyo kiliwatokea puani..Lakini leo inawashangaza sana Wabara kuona nyie mkiendelea kudai na kutimiziwa mahitaji yenu na huyu baba yetu CCM mwenye wake wawili (Mkapaism) ooops!.

Aidha nyie muwe watoto wa kambo mlozaliwa na na tumbo la mke wa pili haina maana kwa udoigo wenu basi baba ndio mifedha yoote aliepeke kweny hali sisi huku tumeachwa katika kibanda cha makuti.. Kwa maana kwamba ukubwa wa kiwanja chetu haina maana tunamiliki utajiri wa baba, fedha inatoka ndani kwena kwa mke huyu wa pili..
 
Haya mambo matatu na mengine mengi yaliyopo na yatakayokuja yanahatarisha mchakato wa uchaguzi mkuu. Tukianza na afya ya mkuu, sote tunajua ni kiasi gani hofu na sintofahamu pale ambapo la kutokea laweza kutokea. Kiukweli rais ni mgonjwa na mwenendo unaonyesha. Rais si mchangamfu tena kama awali na kampeni zake zimekosa mashiko. Lolote laweza kutokea. Suala la muungano ni ishu nyingine. Leo kiuwazi kabisa zanzibar imeanza mchakato wa kujiengua toka 'makucha' ya bara. Zbar leo wana makamu wao wa rais. Kitendo cha wagombea wenza wa vyama vyote bara kutoka nchi nyingine (zbar) kinabatilisha moja kwa moja mchakato wa uchaguzi mkuu. Bado kidogo cuf na ccm zbar watafanya maajabu ya kutengeneza chama kipya na kuachana na bara. Itakuwa kama ASP na TANU walipoungana na kuunda ccm. Haya yataleta mtikisiko kwenye uchaguzi huu. Suala la tatu ni pale ccm itakapoamua kukataa ukweli kuwa upinzani umechukua nchi. Wao wanasema ccm is here to stay. Ccm itatawala milele na nguvu zote zitatumika kuhakikisha hili linatekelezeka. Hapo ndio mwanzo wa vuta nikuvute. Ni wakati huo pia tutawakumbuka watabiri wetu. Haya yataweza kutokea endapo watanzania watatumia haki zao kikatiba, utashi wao na kuamini katika kile wanachotaka. Lakini akili zetu zikibakia kama za jana basi na mambo yote yatakuwa kama jana. Sina sababu ya msingi ya kusema naitakia tz uchaguzi mwema bali naitakia mabadiliko (mapinduzi) mema na ya staha. (sijapanga vizuri kwa kuwa nimetumia mobile. Hope nimeeleweka lakini).
 
Masuala yako ni mazuri na mazito yote yana umuhimu mkubwa yanahitaji uchambuzi wa kina, ungeyatenganisha kila moja likajadiliwa kivyake nafikiri lingekuwa jambo la busara, ni maoni yangu tu.
 
Masuala yako ni mazuri na mazito yote yana umuhimu mkubwa yanahitaji uchambuzi wa kina, ungeyatenganisha kila moja likajadiliwa kivyake nafikiri lingekuwa jambo la busara, ni maoni yangu tu.
ni kweli, chief na ndio maana nikaweka hiyo comment ya mwisho. Lakini cha msingi mada inaeleweka
 
kwaheri muungano zanzibar jamani ndo mnatuacha duh zenji jamani zenji

No! zenj wanafagilia Muungano, Lakini wataka Muungano wa kweli sio huu UKOLONI mliwagusa pabaya Kuwaambia mafuta ya Muungano lakini madini ya Tanganyika, zanzibar si nchi ni sehemu ya Tanzania, ah mbona hii Tanzania nikama ile Tanganyika! nembo ya Taifa la Tanganyika ndiyo nembo ya Tanzania. Wakashtuka Dah awa jamma wajanja enh! Kumbe mnatukoloni enhee.
 
Kutokana na uzito wa nafasi mnayogombea katika uchaguzi mkuu mwaka huu, tunaomba kila mmoja wenu ataje hadharani (katika kampeni zenu zinazoendelea) kiasi cha mali alizonazo bila kusahau kiasi cha fedha mlizonazo kwenye akaunti zenu ikiwa hapa nchini au nje ya nchi.

Tunawatakia mafanikio mema katika kampeni zenu
 
mwaka huu tutashuhudia mengi, kwa kweli kuna haja ya kufungua sanduku la panorama na kuzungumzia kwa uwazi kuhusu huu muungano.


heri tuzungumzeni sasa kuliko wakati mwengine


Zanzibar yaibua kero mpya ya Muungano

Na Mwinyi Sadallah
3rd September 2010
Chapa
Maoni


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imezuia hati idhini (charter) za vyuo vikuu vya Zanzibar kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete, kutokana na mgongano wa kisheria.
Uamuzi huo umesababisha Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (Suza) kutopatiwa hati idhini na Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kama ilivyofanyika kwa baadhi ya vyuo vilivyopo Tanzania Bara.

Sherehe ya kukabidhiwa hati hizo zilifanyika Agosti 18, mwaka huu, Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, alithibitisha kutokea kwa mgongano huo wa kisheria, lakini alisema suala hilo tayari limeanza kutafutiwa ufumbuzi wake.
Waziri Haroun alisema ni kweli Rais Kikwete ametoa hati hizo kwa vyuo vikuu tisa, lakini vyuo vikuu vya Zanzibar havikukabidhiwa hati hizo kwa kuwa Rais wa Zanzibar ndiye anayetakiwa kuzikabidhi kwa vyuo vikuu vya Zanzibar.

Alisema Zanzibar inataka hati hizo zikabidhiwe Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na baadaye kutayarishwe sherehe ya kuzikabidhi kwa vyuo vikuu husika.

Alisema Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar kimeanzishwa kwa sheria namba 8, ya mwaka 1999 na Baraza la Wawakilishi Zanzibar na mkuu wa chuo hicho ni Rais wa Zanzibar.

Waziri Haroun alisema Elimu ya Juu ni suala la Muungano, lakini alisema hati idhini ya vyuo vikuu vya Zanzibar zinatakiwa zitolewe na kukabidhiwa na Rais wa Zanzibar.

"Elimu ya juu ni ya Muungano, lakini sheria haituzuii kuanzisha vyuo vyetu na ndio sababu Zanzibar ikaanzisha Suza,'' alisema.

Inafahamika kwamba Vyuo vikuu Zanzibar ambavyo vinatambuliwa na TCU ni Chuo Kikuu Tunguu na Chuo Kikuu cha Elimu Chukwani.

Hata hivyo, Waziri Haroun alivizuia vyuo vikuu hivyo kupokea hati idhini jambo ambalo inaripotiwa kuwasononesha TCU.

Lakini habari kutoka ndani zimesema kumekuwa na mvutano kati ya Wizara ya Elimu Zanzibar na ile ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya Muungano kuhusu sheria namba 5 ya vyuo vikuu nchini.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Profesa Ali Seif Mshimba, alisema hana uwezo wa kuzungumzia mvutano uliojitokeza kuhusiana na sheria hiyo.

"Nasikitika sana mie siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na suala hilo, mimi siyo mwenye chuo waulize wenye chuo, hasa Waziri husika, " alisema.

Uchunguzi zaidi ya NIPASHE umegundua Chuo Kikuu cha Tunguu ambacho tayari kinatambuliwa kilikuwa kipokee hati idhini yake, lakini ghafla wahusika walitakiwa waondolewe katika orodha ya vyuo vikuu ambavyo vilitakiwa vikabidhiwe hati hizo kutokana na mvutano uliojitokeza.

Vyuo tisa vilivyokabidhiwa hati idhini hizo na Rais Kikwete ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (Duce) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa (Muse).
Vingine ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hebert Kairuki (HKMU), Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Morogoro (MUM), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (Teku), Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi.

Vingine ni Chuo Kikuu cha Sebastian Kolowa (Sekuco), Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba Kilimanjaro (KCMC), Chuo Kikuu cha Matakatifu Augustine Tanzania na vyuo vyake vishiriki, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana kilichopo Dodoma, Chuo Kikuu cha Sokoine pamoja na Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara mjini Moshi.

Mgogoro huo ni mpya katika masuala ya elimu ya juu na hadi sasa haijafahamika ni lini vyuo vikuu vya Zanzibar hati idhini zake zitasainiwa na kukabidhiwa wahusika.

Vyuo vikuu vya Zanzibar ni Suza, Tunguu na Chukwani ambavyo vimekuwa vikipokea wanafunzi kutoka nchi za kigeni tangu kuanzishwa kwake.

Hivi karibuni Baraza la Wawakilishi Zanzibar lilipitisha mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar pamoja na mambo mengine yakiitambua Zanzibar kuwa nchi, kumuongezea Rais wa Zanzibar madaraka ya kugawa mikoa na wilaya ambayo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ni madaraka ya Rais wa Muungano.

Kumekuwa na mjadala mkubwa juu ya mabadiliko hayo, lakini hivi katibuni Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe, alisema kuwa haoni mgongano wowote kwenye mabadiliko hayo kisheria.


 
Hata kwenye muungano kiliswagwa:glasses-nerdy:


taratibu mheshimiwa, ukubwa pua si wa makamasi. cha msingi ni watu wazima kukaaa na kuzungumza kwa uwazi na kila mmoja kutupa karata chini halafu tuangalie jee tuendeleee na game na kwa mtindo upi, tuanda rules of the game na haiwezekani tukunje karata kwa ustaarabu tupeane mikono na utani uendlee maana sisi ni ndugu. maaana tunamuingiliano mkubwa sasa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na mengineyo
 
Mabadiliko ya katiba Zanzibar yaidhinishwa
Saturday, 04 September 2010 20:18

Salma Said, Zanzibar

SHERIA namba 9 ya mwaka 2010 ya marekebisho ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya 1984 ambayo inaitambua Zanzibar kuwa ni nchi na muundo mpya wa serikali ya umoja wa kitaifa imetiwa saini rasmi na Rais Amani Abeid Karume.


Sheria hiyo imetungwa baada asilimia 66.4 ya ya kura za maoni zilizopigwa Julai 31 mwaka huu kukubali mfumo mpya wa muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar baada ya uchaguzi ujao.

Habari ambazo zimelifikia Mwananchi Jumapili jana zimeeleza kwamba Rais Karume alisaini sheria hiyo Agosti 13, 2010 mwaka huu.

Kutokana na idhinisho hilo, sasa kipengele cha katiba kilichokuwa kinaeleza kwamba Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, sasa kitasomeka: “Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar. ”


Marekebisho hayo ya 10 ambayo yamefunua mjadala mkali miongoni mwa wataalamu wa sheria nchini pia imempa mamlaka rais wa Zanzibar kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengine kwa kufuata utaratibu uliwekwa na sheria iliyotungwa na baraza la wawakilishi bila ya kuzingatia sheria nyengine.

Vile vile kabla ya marekebisho haya ya 10 rais wa Zanzibar alipaswa kushauriana na rais wa Jamhuri ya Muungano kabla ya kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengine kufuata utaratibu uliowekwa.

Gazeti hili limefanikiwa kupata nakala ya sheria hiyo ambayo pia inaainisha katika kifungu cha 39 (1) (2) kuwa kutakuwa na rais wa Zanzibar na makamu wawili wa rais ambao watajulikana kama makamu wa kwanza wa rais na makamu wa pili wa rais.

Makamu hao wa rais, wanaelezewa kuwa watatakiwa kuteuliwa kushika nyadhifa hizo ndani ya siku saba mara baada ya rais kushika madaraka.

Kwa mujibu wa sheria hiyo makamu wa kwanza wa rais atateuliwa na rais baada ya kushauriana na chama kilichotokea nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa rais.

Hata hivyo endapo ndani ya siku saba baada ya rais kushika madaraka, chama kinachostahili kutoa makamu wa kwanza wa rais kitashindwa kuwasilisha kwa rais jina la uteuzi wa makamu wa kwanza wa rais, basi rais ataacha wazi nafasi hiyo.

Makamu wa kwanza wa rais, kwa mujibu wa sheria, atakuwa ni mshauri mkuu wa rais na atatekeleza kazi zote atakazopangiwa na rais.

Nafasi ya makamu wa pili wa rais itatolewa kwa mtu ambaye atatoka chama kilichotoa rais na itakuwa imechukua nafasi ya waziri kiongozi.


source: Mabadiliko ya katiba Zanzibar yaidhinishwa

NIONAVYO MIMI:
Tuache kulazimisha visivyowezekana, ni wakati muafaka sasa wa serikali tatu, maadam serikali ya Zanzibar sasa ina nguvu zaidi, iwepo ya Tanganyika, na pia ya Muungano...
 
..Zanzibar ni nchi sasa kulingana na mabadiliko ya katiba yaliyofanyika.

..kuna kila sababu na haki za kuwa na mabalozi wenu wenyewe nje ya nchi.

..Zanzibar wadai upya kuwa wanachama wa Fifa.
 
yea hata mm natamani tuwe hapo, nnaamini tutaweza kuleta changa moto nzuri ya kimaendeleo Afrika mashariki
 
Back
Top Bottom