Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
Zanzibar ikitaka kuendelea inatakiwa kuimarisha elimu ambayo ni ya hali ya chini sana. Zanzibar wakifikiria kwamba mafuta yatakuwa ya kwao ni kichekesho kwani hata UN hawaitambui Zanzibar kama nchi, haina jeshi, pesa, elimu, wafanyakazi, umeme. Hakuna kampuni ambayo ita sign na Zanzibar mkataba wa uchimbaji bila signature ya bara.
Hivi Latvia. Estonia, Bosnia herzogovina.na nyingi tu kabla ya 1990 zilitambulika kuwa ni nchi? Jifunze kutoka huko.
 
Huyu alikuwa Sultan Khalifa Bin Haroub, baba yake na Sultan Jamshid bin Abdullah aliyepinduliwa. Nitatafuta picha ya Sultani Jamshid na kuiongezea hapa kesho.

Huyo kwenye picha ya juu sie babaake Jamshid, babaake Jemshid ni Sulatan Abdallah ambae yupo kwenye picha ya chini pamoja na akina Mohammed Shamte akizungumza na Al-Muhsin.
 
LICHA ya kuwapo mchakato wa kuondoa mpasuko wa Muungano unaofukuta, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema suala la mafuta na gesi asilia halikuwepo katika orodha ya mkataba wa Muungano uliosainiwa na viongozi na waasisi wawili wa mataifa mawili Zanzibar na Tanganyika.


Akitoa tamko hilo lililochukua muda wa zaidi ya saa moja mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi jana, Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi, Mansoor Yussuf Himid alisema SMZ inataka kuondolewa kwa suala la mafuta na gesi asilia kwenye orodha ya mambo ya Muungano kwa sababu haliwanufaishi Wazanzibari na pia suala hilo halikuwemo kwenye mkataba wa Muungano mwaka 1964.


Alisema suala la mafuta na gesi asilia kuwemo kwenye mambo ya Muungano ni ukiukwaji mkubwa wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar ambazo zinapaswa kuheshimiwa.


"Mheshimiwa Spika, na waheshimiwa wajumbe wa baraza hili, sheria iliyoanzisha TPDC, na ile ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta haikuridhiwa na Baraza la Wawakilishi na hivyo kukosa uhalali wa kuwa suala la Muungano," alisema Waziri Himid.


Akiyataja mambo 11 ya Muungano Himid alisema suala hilo pia halikutajwa hata katika mkataba wa Muungano wenye mambo 11 ambayo aliyataja moja moja mbele ya wajumbe.


Waziri huyo alisema kwamba, TPDC limeundwa kwa mujibu wa amri ya Rais mwaka 1969 na kuundwa tena kwa mujibu wa sheria ya mashirika ya umma 1980, lakini sheria hiyo, haikuridhiwa na Baraza la Wawakilishi na hivyo ni batili linalokosa uhalali wa kuwa chombo cha Muungano.


Waziri Himid alisema Zanzibar na Tanganyika ni nchi mbili ambazo zimeanzisha Muungano wa kisiasa na kila nchi kubaki na utawala wake isipokuwa mambo maalumu yaliyoainishwa katika makubaliano ya mwanzo ya Muungano na ndio maana katiba ya Zanzibar sura ya pili inaeleza malengo na maamuru muhimu ya sera ya SMZ kudhibiti uchumi wa nchi yake, hivyo sio busara kuanza kuingiza suala la mafuta katika orodha ya Muungano.


Hata hivyo, Waziri huyo aliwaambia wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwamba serikali ilimpa kazi mshauri mwelekezi, lakini ushauri uliotolewa na mshauri mwelekezi huyo umesheheni upotoshaji mkubwa kwani badala ya kutatua tatizo hilo, yeye amejiegemeza kutaka suala hilo kubakia kwenye mambo ya Muungano kinyume na matakwa ya Wazanzibari.


Alisema endapo ushauri alioutoa Mshauri Mwelekezi utatekelezwa, basi Zanzibar itaishia kwenye mgongano wa Kikatiba na kero mama ya Muungano kuendelea kuwaumiza Wazanzibari na kusisitiza ni muhimu kuondolewa na kusimamiwa na SMZ suala hilo.


Waziri huyo alitaja mapendekezo matatu ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa Baraza la Wawakilishi kuwa, Ardhi na bahari ya ndani ya Zanzibar, maeneo ambayo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar sura ya kwanza 2 (1) ni milki ya Zanzibar, katika maeneo hayo usimamizi, udhibiti na uendeshaji wa shughuli zote za utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia uwe wa Zanzibar pekee na sio sehemu nyingine kwa kuwa hata Tanzania Bara wana mali asili zake kama vile almasi, dhahabu na mambo mengine ambayo Zanzibar hainufaiki navyo.


Pendekezo la pili ni kuwa, sasa wakati umefika kwa Zanzibar kuwa na chombo chake cha kusimamia mambo yote yanayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na mengineyo yanayoendana na hayo , chombo hicho kitakuwa sawa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).


"Hii ni njia pekee ya kuondosha migongano ya madaraka na masilahi na pia ni njia pekee ya kuhakikisha haki za Zanzibar na watu wake zinalindwa kwa sasa na baadaye kwani Zanzibar haina cha zaidi ya rasilimali zake," alisema Himid.


Pendekezo la tatu ni kwamba kwa upande wa bahari kuu (EEZ), Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, inashauri kukubali ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa eneo hilo pekee kwa makubaliano maalumu na sio muundo wa sasa wa Taasisi na sheria kwamba Zanzibar itakuwa ni mshiriki sawa.


Katika ripoti yake, Mshauri Mwelekezi anapendekeza kuundwa kwa wizara itakayoshughulikia mafuta chini ya Jamhuri ya Muungano, kuundwa upya kwa TPDC ili iwe yenye sura ya Muungano na kusisitiza vyombo hivyo kuwa ndiyo viwe vyenye mamlaka ya kusajili makampuni yote jambo ambalo halikuridhiwa na SMZ.


Waziri Himid alisema suala la kuundwa kwa Taasisi hizo mbili likikubalika, Zanzibar itakosa mapato yote yatokanayo na usajili wa makampuni hayo na uchimbaji wa mafuta, pia SMZ itakosa mapato ya leseni pamoja na “Renewal ya leseni hizo kila mwaka kama ilivyo hivi sasa.


Waziri huyo alisema licha ya gesi kuchimbwa na kuuzwa, lakini SMZ haijapata mapato ya aina yoyote licha ya kuwa kwa sasa ni jambo la Muungano,"rasilimali ya mafuta na gesi asilia inatokana na ardhi, kinachoshangaza ni kuona Tanzania Bara ina mali asili nyingi zinazotokana na ardhi ambazo hazijaingizwa katika orodha ya Muungano.


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilitafuta Mshauri Mwelekezi kwa ajili ya kupata mgawanyo mzuri wa rasilimali za mafuta na gesi asilia itakayozalishwa nchini.


Kampuni ya AUPEC ya Uingereza ndiyo iliyoshinda zabuni na kupewa kazi hiyo chini ya Mtaalamu wake, David Reading kutoka Scotland ambaye katika ripoti yake alishauri mafuta na gesi asilia kuendelea kubaki kwenye orodha ya Muungano ripoti ambayo iliyobezwa na kutiwa kasoro nyingi na SMZ.


Ripoti ya Mshauri Mwelekezi huyo iliwasilishwa mbele ya Baraza la Mawaziri (Baraza la Mapinduzi) na kujadiliwa na hatimaye kutolewa mapendekezo ambayo ndio yaliyowasilishwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na kutolewa maamuzi.


Kwa mara ya mwisho wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa pande mbili kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), waliungana na kutoa tamko la kuishauri serikali kutokubali suala la mafuta na gesi kuwemo katika orodha ya Muungano kwa kuwa hati halisi ya mambo 11 ya Muungano suala hilo halikuwemo.



Awali, Mshauri Mwelekezi alisema kwamba mafuta yaliyopo katika visiwa vya Zanzibar ni kidogo na huenda yakawa sio ya kibiashara kama inavyotarajiwa na wajumbe hao lakini kauli hiyo ya Mshauri ilionekana kuwapandisha hasira wajumbe hao na kusema hata kama mafuta yatakayoonekana yatakuwa sawa na kichupa cha pombe 'kinibu' basi yabaki kama ni rasilimali ya Wazanzibari na vizazi vyao hata kama ni ya kujipaka, lakini yasiingizwe katika orodha ya Muungano.


Awali, akitoa tahadhari, Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha kabla ya kuwasilishwa kwa tamko hilo la serikali aliwakumbusha wajumbe wa baraza hilo kutoa maoni yao kwa uwazi na bila ya kutumia jazba za kisiasa ili maoni hayo yaweze kuwanufaisha Wazanzibari wote juu ya rasilimali zake.


From mwananchi 4/4/2009
 
Kwani Wazanzibari hawana haki ya kuliza kitu wanachokiona hakipo katika Muungano? Iwapo wana haki basi tuwaache waseme? Kwani hilo linahatarisha muungano wetu? Ni bora kusema kuliko kunyamaza kimya kimya.
 
Je mafuta hayo yapo au ni maneno tu?
Acha kushabikia mali na wewe. hatuendi huko. Aliyoeleza waziri Mansour ni mambo ya msingi . Sasa mafuta yawepo au yasiwepo siyo hoja. Lakini hii namna jinsi rasilimali zitakavyogawanywa kwetu na kwa vizazi vitakavyotufuata katika hii JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ndiyo muhimu. Na namuunga mkono Mansour moja kwa moja (kwa asilimia 100) .
 
Wazanzibari wanayo haki kudio hilo. Kwani wanafaidika na dhahabu, alimasi, tanzanite na madini mengibne yanayochimbwa Bara? sisi watu wa Bara (nami mmoja wao) tusiwe na tamaa ya kiasi hicho.
 
Wazanzibari wanayo haki kudio hilo. Kwani wanafaidika na dhahabu, alimasi, tanzanite na madini mengibne yanayochimbwa Bara? sisi watu wa Bara (nami mmoja wao) tusiwe na tamaa ya kiasi hicho.

Fact: zanzibar mwaka jana wamekusanya kodi $20m kwa mwaka na wamesamehe $19m. (ilikua ni mzozo sana mwaka jana kwenye baraza la wawakilishi). bara wanakusanya kodi $300m kwa mwezi na sio $20m kwa mawaka. Kwa hiyo ukae ukijua bajeti ya zanzibar inafadhiliwa na bara.
 
..sasa kulikuwa na haja gani ya kumleta huyu Mshauri mwelekezaji?

..Zanzibar wameingia gharama bure tu wakati ushauri wake wala walikuwa hatuuhitaji.

..nadhani hili la mafuta kila upande uchimbe ya kwake.
 
Ndio hivyo jeuri yao wanasema hata yakiwa ni kijichupa tu basi watajipaka.Na fahamuni kuwa kuna dondoo hapo kuwa Nchi hizi zimeungana kisiasa tu na huyo baba yenu wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere alisema ikiwa WaZanzibari itafika siku siku na kusema huu Muungano uishe basi hatakuwa na uchoyo na kukubali bila ya tatizo ,ila hawa mafisadi tulionao leo wanasema wataulinda ,maana wanajua fika Muungano ukikatika leo basi mirija yao itakosa hewa na watakufa vibudu.
 
Tuwapongeze wenzetu kwa kuwa wako makini na raslimali zao sio sisi huku bara tunagawa raslimali kama njugu. Kuishi kwa ujanja ujanja hakutatufikisha mahali popote watu wa bara bali kutazidi kututumbukiza kwenye umaskini. Mfano ni hiyo gesi, watu wametuingiza kwenye mikataba feki kiasi kwamba faida ni kidogo mno. Faida kidogo imesababisha selikari ya bara ishindwe hata kuwapa gawio watu wa Zanzibar pamoja na kuwa suala la gesi ni la Muungano. Selikari ya bara wangekuwa makini, na kwa vile dalili za kuwepo mafuta Zanzibar zilikuwepo toka zamani, wangehakikisha kuwa kile kidogo kinachopatikana kwenye gesi wanaigawia selikari ya zanzibar ili hapo mafuta yatakapoanza kuchumbwa, Zanzibar wasije wakawa na pa kutukatalia kutupatia sehemu ya faida ya mafuta. 'Tungewaambia haya ni mambo ya muungano, gesi tunakula wote na mafuta pia tutakula wote'. Kama hatujawapatia chochote kutokana na uzalishaji wa gesi kwanini tuwalazimishe wao watupatie kutoka kwenye mafuta? Wacha wa komae ni uzembe na ufujaji wetu umetufikisha hapa
 
Tuwapongeze wenzetu kwa kuwa wako makini na raslimali zao sio sisi huku bara tunagawa raslimali kama njugu. Kuishi kwa ujanja ujanja hakutatufikisha mahali popote watu wa bara bali kutazidi kututumbukiza kwenye umaskini. Mfano ni hiyo gesi, watu wametuingiza kwenye mikataba feki kiasi kwamba faida ni kidogo mno. Faida kidogo imesababisha selikari ya bara ishindwe hata kuwapa gawio watu wa Zanzibar pamoja na kuwa suala la gesi ni la Muungano. Selikari ya bara wangekuwa makini, na kwa vile dalili za kuwepo mafuta Zanzibar zilikuwepo toka zamani, wangehakikisha kuwa kile kidogo kinachopatikana kwenye gesi wanaigawia selikari ya zanzibar ili hapo mafuta yatakapoanza kuchumbwa, Zanzibar wasije wakawa na pa kutukatalia kutupatia sehemu ya faida ya mafuta. 'Tungewaambia haya ni mambo ya muungano, gesi tunakula wote na mafuta pia tutakula wote'. Kama hatujawapatia chochote kutokana na uzalishaji wa gesi kwanini tuwalazimishe wao watupatie kutoka kwenye mafuta? Wacha wa komae ni uzembe na ufujaji wetu umetufikisha hapa

zanzibar hawana hela za kujiendesha wenyewe wanaishi kutokana na (kodi na mapato mengine) yatokayo bara.

miaka yote wa bara walikua wanalipia umeme ghali, ili zanzibar watumie bure mbona hawakuwa wanalalamika

kwani hata bara siwanataka hiyo rasilimani mbona ujasema na wao wanaangalia, kutaka iwe yako ni swala jingine na kuangalia ni swala jingingine usichanganye habari.
swala la zanzibar kuangalia rasimali yake sidhani kama ni liatatokea kama wameweza kutoa msamaha wa kodi $19m na wao mapato yao ni $20m.
 
Last edited:
miaka yote wa bara walikua wanalipia umeme ghali, ili zanzibar watumie bure mbona hawakuwa wanalalamika

Ninavyojua mimi Zanzibar wanalipia umeme kwa muda mrefu. Bei wanayolipa ni halali kabisa, kama watu wa bara tumeamua kukubali kulanguliwa bei ya umeme kiasi kwamba tunashindwa hata kupikia shauli yetu na ni uzembe wetu.
 
Ninavyojua mimi Zanzibar wanalipia umeme kwa muda mrefu. Bei wanayolipa ni halali kabisa, kama watu wa bara tumeamua kukubali kulanguliwa bei ya umeme kiasi kwamba tunashindwa hata kupikia shauli yetu na ni uzembe wetu.

Umeme unakwenda Zanzibar ulikuwa unafanyiwa ufisadi na bili yote ikiiangukia Serikali ya Zanzibar ,kuna sehemu gidi yake imegidwa na kupewa mitaa flani flani inayokatisha hapo Dar ,jina la ile sehemu nimelisahau ,ila matumizi yake yakiorodheshwa katika bili ya umeme wanaotumia Zanzibar.
Halafu kuna tabu gani si kateni umeme wenu tu tuone kama watafariki ,mbona walikosa umeme miezi mitatu na hakuna aliekufa genereta mpaka ikulu na Karume alisema kelele za jenerators hazimnyimi usingizi. 😀
 
Jamani, huu Muungano wetu na Zanzibar tuufanye kama Ndoa ya Kiserikali ya kizungu, inajengwa kwa msingi wa upendo, maridhiano na haki sawa. Mke akitaka madaraka zaidi katika kutumia anachozalisha, anapewa uhuru huo. Hata ikifika wakati akajiona mume huyu hana maslahi naye tena, pendo limenyauka, wanavunja mkataba, wanashikana mikono, wanabaki marafiki.

Kama kuna gesi na mafuta ni mali halali ya Zanzibar, kitu ambacho Bara tunapaswa kufanya, ni kuwapa Wanzanzibari kila wanachokitaka bila kuwaburuza.

Hizo pesa za gesi na mafuta kama ni za kutosha, tusiwape pesa za kuendesha serikali yao, yaani wajitegemee. Ufike wakati walipe mpaka umeme na kupunguza kuibeba Zanzibar. Hata uanachama wa OIC tuwape.

tanzania Bara isiwe kama Mume mwenye wivu, akiona mke anafanikiwa, anamdidimiza ili aendelee kuwa tegemezi.

Wapenda haki, waliyoyasoma yale mambo 11 kwenye hati za Muungano za 1964, na namna jinsi yalivyoongezwa mpaka sasa ni 28, atasymphasize na haki za Wazanzibari, hata Hayati Karume akifufuka, akasikia rais wa Zanzibar sio Makamo, ataacha laana kwa bara.

Pamoja na muungano wetu, Tanganyika kufuta utaifa wake na kuitwa Tanzania, Zanzibar ilibaki na utaifa wake kama nchi isiyo na nguvu za dola.

Kuwaachia mafuta yao ni hatua muhimu kuelekea kwenye muungano wa haki sawa wa serikali tatu ambao utaondoa kero
Zote, ama tuiachie Zanzibar ifanye uchaguzi huru, wapinzani wachukue nchi na kuuweka rehani muungano.
 
Pasco una mawazo . Kujiingiza katika Muungano (26 April 1964) kusiondoe uhuru wa Zanzibar hii. Kurekebisha mambo Pasco anzia na kwenye vyama. Waache Wazanzibari waunde vyama vyao ( wapige kura na kuchaguana kupitia vyama vyao- siyo CCM au CUF au vyenginevyo vilivyopo sasa). Pasco Zanzibar ni Nchi Tulishauliza hapa?
 
zanzibar hawana hela za kujiendesha wenyewe wanaishi kutokana na (kodi na mapato mengine) yatokayo bara.

miaka yote wa bara walikua wanalipia umeme ghali, ili zanzibar watumie bure mbona hawakuwa wanalalamika

kwani hata bara siwanataka hiyo rasilimani mbona ujasema na wao wanaangalia, kutaka iwe yako ni swala jingine na kuangalia ni swala jingingine usichanganye habari.
swala la zanzibar kuangalia rasimali yake sidhani kama ni liatatokea kama wameweza kutoa msamaha wa kodi $19m na wao mapato yao ni $20m.

Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009
 
Tanganyika ni lini ilifuta Utaifa wake kisheria sio longolongo ,WaZenji wanaikaba hii hoja kisheria sio mmeshiba feza ya ufisadi basi mnalopoka tu vile kasumba inavyowapeleka tunajua WaZanzibari ni walevi wa tende au wamelewa kwa ulevi wa Tende lakini huko madongo kupolomoka mmelewa kwa feza ya wizi feza ya ufisadi ndio inayowapa kiburi.Kila kitu mnakitolea mimacho vyengine vitawatokea puani.
 
Pasco una mawazo . Kujiingiza katika Muungano (26 April 1964) kusiondoe uhuru wa Zanzibar hii. Kurekebisha mambo Pasco anzia na kwenye vyama. Waache Wazanzibari waunde vyama vyao ( wapige kura na kuchaguana kupitia vyama vyao- siyo CCM au CUF au vyenginevyo vilivyopo sasa). Pasco Zanzibar ni Nchi Tulishauliza hapa?
Tusilete tena mjadala wa Zanzibar ni nchi au si nchi, lengo la post ni sisi wabara kuwarudishia Wazanzibari mamlaka zao tulizopora zaidi ya yale 11 kwenye mkataba wa Muungano.

Kama Zanzibari ingeachiwa iwe bandari huru, Watanzania tusingekuwa tunahangaika na kununua magari Dubai na Japan, mambo yote yangekuwa Zenj.

Ndivyo itakavyokuwa kwa mafuta, badala ya kuagiza uarabuni, tunanunua kwa jirani nchi ya Zanzibar.
 
Back
Top Bottom