Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kero zake: Je, tuuvunje?
hakuna cha Muungano kuvunjika!

sababu za Visiwani kuwa sehemu ya Muungano sii za kiuchumi..ni kwa ajili ya usalama wa Bara pia!

Huo ndo ukweli!
 
hakuna cha Muungano kuvunjika!

sababu za Visiwani kuwa sehemu ya Muungano sii za kiuchumi..ni kwa ajili ya usalama wa Bara pia!

Huo ndo ukweli!

Pole mzalendohalisi lakini kwenye kifo kila mtu hulia mama yangu na sio mama yetu ,pia ukumbuke ukweli ukidhihiri uongo hijitenga .time has come ,kulikuwa na miungano yenye nguvu za kilimwengu leo ipo wapi ? wacha mungano huu wa nchi omba omba .kwa mfano kulikuwa na nchi inayoitwa senegambia leo ipo wapi wakati tu haujawadia kuna kitu kinaitwa (winds of change )na tayari umeanza kupulizia maeno tuliopo .Change is gonna come ukitaka usitake kama sio leo kesho ,hizi sisi za uongo na kweli za kuwafanya hawa poor people wazidi kulala na wachache watumie mirija yao kwa kuwanyonya haian mahali tena
 
si hayo tu mkuu hata yale mambo yoooote yaliyoingizwa katika mambo ya muungano kwa mkono wa kushoto yatapitiwa upya subiri tu utaona "dawa inachemka" watatujua kama tuba adabu au hatuna.shabaaaash
 
Pasco ! nafikiri na wewe umepandwa na jazba ,kumbuka kwa nini baadhi ya viongozi wa nchi hii wamepewa majina kama mafisadi ?Mafisadi maana yake nini? ukishapata jawabu lake hapo rudi na ujiulize maana ya mtu mwizi nini?hao viongozi wanoitwa mafisadi wamemuibia nani?wananchi wamefurahiswa na ufisadi huo(wizi) uliofanywa na viongozi ambao wananchi wamewachagua?ni miongoni mwa viongozi wanaotuongoza ndio mafisadi (wezi )wa mali ya uma na jamii kwa ujumla lakini hilo wewe hulioni na wala halikuumi inawezekana unatokana na familia ya hao wanaomiliki uchumi wa nchi kwa maslahi yao .mwiba aliposema wezi watanganyika kwa mtu mwenye akili yake timamu anaelewa anamainisha ni akina nani hakuna wengine isipokuwa hao waliokua wanafisidi uchumi wa nchi bila kuwa na huruma ya wananchi waliowachagua kwa imani nzuri na kama utasoma kuna sehemu mwiba ameandika kuwa Mafisadi wamefidi Tanganyika na sasa wanakuja nchi ya pili hapa alikuwa anzungumzia hao wenyewe uwezo wakufisidi na kuchota mali za uma na sio watu wakawaida unajaribu ku twisti isssue
Pasco eh suala la kumaliza mpasuko ni gumu kidogo kwa sababu chanzo chake hasa kinachochewa na serikali ya muungano kwa kuwalazimisha wazanzibari lazima ccm ibaki madarakani japo wananchi hawataki, ukifika uchaguzi mamia ya askari na jeshi tutaletewa utafikiri zanzibar hakuna askari, yote hayo ni kuilinda ccm ibaki madarakani na kuulinda muungano huu wa kifisadi,lakini sasa tumejua janja yenu...mtatujua vijukuu vya mapinduzi
 
Binafsi nimeshajiuliza sana swala la Zanzibar. Ni kweli hawa ni ndugu zetu, pia ni kweli muungano wetu kama ulivyounganishwa na Nyerere na Karume unautata, vile vile ni kweli kuungana ni kitu kizuri katika kukuza uchumi na mahusiano baina ya zilizokuwa nchi mbili. Hatahivyo kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajibiki na hao wanaosuruhisha maswala ya muungano.

Haikuniingia akilini nilivyosikia Zanzibar ilikuwa inatumia umeme toka Bara bila kulipa mpaka ilipoingia Net Group Solution ambapo waliambiwa walipe or else wanakatiwa umeme. hapo ndipo nilipochoka maana walipiga mkwala kuwa wakikatiwa umeme wanavunja muungano, ukweli ni kwamba serikari ya bara ililipa lile deni la Zanzibar na mambo yakawa shwari. Hata hivyo bado hawa jamaa wanalazimisha tuvunje muungano lakini CCM haitaki na imekula yamini kuulinda kwa nguvu zote.

Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Hataukimpa offer nyingi nyingi kama hana mapenzi na wewe itakuwa ngumu kuwa rafiki yako. Kinachoendelea Zanjibar na Bongo sasa hivi ni kama baba na mtoto. Zanzibar kila itakachotaka Bara itabidi tukikubari ili mulinda muungano. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????
Unanikumbusha ile hadithi ya shk shaaban Robert ya 'kusadikika' kuwa "lila na fila hawatangamani" kinywa cha lila kikisema sikio la fila linajifanya halisikii, ndo mambo ya muungano huu yalivyo, wanzanzibari wakilalamika dhulma, manyanyaso na bugdha, serikali ya muungano haiskilizi haswaaaa! mpaka wanafika kututukania "viongozi wetu" na kuwaita "watovu wa adabu" AAAAGH, yaani nnahasira ww
 
Muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za Katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la Uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.
No lengo la kuunganisha vyama lilikuwa ni kuizika ASP, ambayo ilikuwa ndo "mouthpiece" ya wazanzibar katika mambo ya muungano jambo lililokuwa likimtisha Nyerere kutimiza azma yake ya kuimeza zanzibar kwa kisingizio cha muungano baada ya kushindwa kuwashawishi waingereza waunganishe uhuru wa Tanganyika na Zanzibar kuwa kwa pamoja kwa kuwa Zanzibar akidai kuwa ni sehemu ya Tanganyika,alipo shindwa hilo akachochoea vurugu zinazoitwa "Mapinduzi matukufu ya 1964" ambayo yaliiondoa serikali halali iliyochaguliwa katika uchaguzi halali na wazanzibar wenyewe, alipofanikiwa hilo akashawishi "muungano" ambao baada ya kumtisha Karume kuwa "hatadumu na serikali kwa kuwa wamanga wanafedha watampindua" alifanikiwa, hatua iliyofuata ni kuuvunja umoja wa wazanzibari na kuwaziba midomo ndo akapata "advantage" ya kifo cha Karume 1972, ambapo miaka minne tu baada ya kifo chake,akaleta wazo la kuunganisha vyama vya ASP na TANU, kwa kisingizio cha umoja na kuivunjilia mbali sauti ya Wazanzibari (ASP), hii ilikuwa ni hatua muhimu kwa Mwalimu kuelekea kuimeza zanzibar na aliposhtukiwa na Jumbe na Ramadhani Faki, akatengeneza 'confusion' aliyoiita "mchafuko wa kisiasa" zanzibar na kuwagonganisha vichwa wazanzibar, hapa ndipo alipo watumia vibaya watu shupavu kama Maalim Seif Shariff bila ya kujijua walimgeuka mwenzao, alipofanikiwa kumtoa Jumbe alitengeza "strategies" za kuwagawa wazanzibar kwa UUNGUJA n UPEMBA wao na kutengeneza chokochoko za makusudi za kuwatibua Wapemba kwa makusudi wagombane na ndugu zao wa miaka na mikaka wa Unguja, hapa ndipo akina Maalim Seif na wenzake walipo uvaa mtego wa Nyerere na kujikuta wakitangazwa maadui Zanzibar na wakitangazwa wapinzani hata mfumo wa vyama vingi bado, mpaka leo wazanzibar wanaungulika na kusulubika kwa dhulma hii ya kufitinishwa na kugombanishwa na siasa chafu za Mwalimu Nyerere, ukitazama vizuri utaona kuwa muda wote huo zanzibar ilifikiri mambo yake kwa kichwa cha Nyerere na kuamuliwa kila kinachohusu mustakbali wao na yeye, hili alilifanya kwa kuhakikisha kuwa kila atakae tawala zanzibar ni lazima awe mtu ambae atamkubali yeye tu na ataapa kulinda azma yake ya kuimeza zanzibar kwa kisingizio cha kulinda muungano, utaratibu huu aliusimamia hata alipoondoka madarakani na kuurithisha kwa waliomfuatia, haya yote na mengine aliyafanya Mwalimu kwa makusudi.
Utakumbuka katika hotuba yake moja anasema " ....hata masafa kutoka bara kwenda Unguja ni karibu kuliko kutoka Unguja kwenda Pemba..."
Hicho kinachoitwa "mpasuko wa kisiasa zanzibar" ni "mythism" tu ya kuendelea kutia chokochoko na fitna kwa wazanzibar kupitia vibaraka wao waliopandikizwa ndani ya SMZ, na wengine wapo huko huko bara wamepewa vyeo vya uwaziri na ulaji kibao kwa lengo la kuwazunguka wazanzibar.si hayo tu mengine......(cont..)
 
Nimefurahi kusikia CCM na CUF wamekubaliana kwa asilimia 100% kwenye hili. Nasubiri kuona kama na mpasuko watauziba kwa asilimia 100% nani ya baraza hilohilo la wawakilishi. Vinginevyo ndiyo ile hadithi ya kujenga jumba la kifalme hewani.
Chonde chonde tuazime busara sasa..huu muungano una umuhimu mkubwa sana kwa zanzibar kuliko wanavyojidanganya
 
Muungano upo kwa faida ya watu wachache sana,ni ngao inayotumika katika kuhakikisha mirija yao inaendelea kunyonya na kusqueeze vilivyo.
Muungano uliopo hauna faida kubwa kwa mwananchi masikini si wa Tanganyika wala wa Zanzibar ,Tanganyika kuilipia umeme Zanzibar sio ukarimu bali mkumbuke kuwa kuna deni kubwa ambalo hesabu zake zikipigwa litakuwa si dogo ,ukianzia uanzishwaji wa BOT ,na zaidi pale waliposituka WaZanzibari kuwa grid inayopeleka umeme Zanzibar inachotwa pale sehemu za Bagamoyo na kuhesabika kuwa unatumiwa Zanzibar hivyo deni la umeme huo likiingizwa kwenye deni la Zanzibar.

Halafu nyie mnaosema kuwa Bunge lina nguvu kuliko Wawakilishi wa Zanzibar naona mna matatizo ya kiuelewa maana chochote kinachopitishwa Bungeni Tanganyika ni lazima kikubalike ndani ya Baraza la wawakilishi ,hapo ndipo mliponasa maana hayo ya mafuta kusimamiwa na TPDC mnasema yalikubaliwa bungeni hayakupelekwa kwenye baraza la wawakilishi na mambo mengi ambayo yalipitishwa kwenye katiba hayakupata ridhaa kutoka Baraza la wawakilishi ,hayo Wazanzibari wanayahesabu kuwa ni mambo yaliopitishwa kinyemela kwa maana hayakufuata zile article za Muungano na makubaliano yaliomo kwenye Katiba ya leo hivyo wala hayakufuata taratibu zozote za kisheria mnajiamulia wenyewe kwa wenyewe,ni rahisi sana kuyafanya ajuari na ndipo huko wanakoelekea kila ambacho hakikupata ridhaa ya Baraza la Wawakilishi kitaondolewa sasa kaeni mkipanga hesabu ni mangapi hamkuyapeleka Baraza la Wawakilishi kupata baraka lazima mtafahamu kuwa popo ni mnyama na si ndege.
 
Nimefurahi kusikia CCM na CUF wamekubaliana kwa asilimia 100% kwenye hili. Nasubiri kuona kama na mpasuko watauziba kwa asilimia 100% nani ya baraza hilohilo la wawakilishi. Vinginevyo ndiyo ile hadithi ya kujenga jumba la kifalme hewani.
Chonde chonde tuazime busara sasa..huu muungano una umuhimu mkubwa sana kwa zanzibar kuliko wanavyojidanganya

Muda mwingine watu wanakubaliana kutokukubaliana. Hebu jiulize kama Zanzibar or Tanganyika si nchi bali Tanzania, na kama huu muungano ni halali kwanini suala la mafuta yaliyoko zanzibar iwe ni mali ya zanzibar peke yake???? Binafsi hainiingii akilini hapa kuna kauhuni fulani kanaendelea hakajawekwa wazi. Mbona resource zote zinazopatikana Tanganyika huchukuliwa kama mali ya Tanzania (Tanganyika & Zanzibar)na watanganyika wala viongozi wake hawalalamiki???????????
 
Muungano wa 1964 ni wa nchi siyo wa vyama. Wa vyama ulikuja 1977. Katika muungano walikubali kuunganisha nchi kuwa nchi moja kama ndoa za Katoliki. Hakuna mwisho hadi kifo.
Kwa mujibu wa Katiba yetu, kufikiria kuuvunja muungano, ni kosa la Uhaini na adhabu yake ni kifo kwa kunyongwa mpaka ufe!.

Pasco Masharti ya ndoa ya kikatoliki au kikristo ni kwamba huwa haivunjiki mpaka kifo kiwatenganishe. Lakini kama ikitokea mambo hayaendi kabisa basi huwa wanandoa wanatenganishwa kwa muda then wanarudiana. So shida iliyopo hapa ni kubwa sana otherwise na sisi wa bara tutaanza kuandamana resource zetu zisitumike kwa maendeleo ya Zanzibar.
 
hakuna cha Muungano kuvunjika!

sababu za Visiwani kuwa sehemu ya Muungano sii za kiuchumi..ni kwa ajili ya usalama wa Bara pia!

Huo ndo ukweli!

Huo usalama wa Bara ndio kitu gani katika ulimwengu wa sayansi na technologia. Watu wana makomboya ya masafa marefu wala hawahitaji kuja kuweka base Zenji. Kwani ulimwenguni kisiwa kipo kimoja tu (Zenji)?? Cuba ili pale ni kisiwa, Madagasca ni kisiwa, etc mkuu hizo wala siisababu za msingi kwa karne hii
 
Nimeshasema zamani.
Kama huu muungano una faida kwetu Watanganyika, nyie Wazenji mlie. Naipenda hii kuwa Tanganyika tuna kakoloni. Kakoloni kengine kanaita huko Comoro hihiiii. Kwanza ubabe wa kupigana hamna. Tangu mzaliwe hamjawahi kupigana nyie kama nchi. Pia kabla hamjafikiri sana, hebu jiulizeni kwanini Comoro wanalilia kuwa Tanzania?
Tamaa mbele mauti nyuma. Hayo mafuta yapo kwanza? Pia waarabu watawaruhusu muyachimbe? Lowassa na ROstam wataacha tu mgawane mamilioni? Hivi wakija na kumuahidi Mwiba uwe rahisi, wanaenda kuchukua Wanyamulenga na kuja kukavamia kakisiwa kenu, mtaweza kuwazuia watusi nyie? Yule Mganda aliwachinja miaka hiyo na hamkufurukuta. Nyie akina Yakhe, mnaenda bapaya. Mmeshaambiwa kuwa serikali ya Muungano itasimamia tu ila faida yote ni yenu, sasa hii ya kusema sisi tutakuibieni inatoka wapi? Hivi pesa ya mahoteli inakwenda wapi? nayo tunaiba siyo?

Msiwe na wasiwasi. Dawa yenu inatokota jikoni. Soon atakuja rais mwenye kuipenda Tanganyika na mtaachiwa huru. Mkikwama chochote TUSIJUANE. Halafu tuone tunavyokufa kwa kukosa mafuta yenu. Mkiyakosa, msijie anza kujipendekeza kwetu. Muuwane hukohuko. Kuanzia leo, nyie si ndugu zangu tena. Si Wamanyema tena, si Wanyamwezi tena..... STOP.
 
Muda mwingine watu wanakubaliana kutokukubaliana. Hebu jiulize kama Zanzibar or Tanganyika si nchi bali Tanzania, na kama huu muungano ni halali kwanini suala la mafuta yaliyoko zanzibar iwe ni mali ya zanzibar peke yake???? Binafsi hainiingii akilini hapa kuna kauhuni fulani kanaendelea hakajawekwa wazi. Mbona resource zote zinazopatikana Tanganyika huchukuliwa kama mali ya Tanzania (Tanganyika & Zanzibar)na watanganyika wala viongozi wake hawalalamiki???????????

Poleni jirani zetu Tanganyika,but you have got to belive yourself you are going to do just fine without us untill than relax .ukweli unauma .[ame=http://www.youtube.com/watch?v=57CzNqgm8Fc]YouTube - Scorpions - Wind Of Change[/ame]
 
Hivi, hawa Wazenj wakija kuta kwamba chimbuko la hayo mafuta (ambayo kwa sasa ni mafuta hewa) ni Tanga, watachimba shimo hadi Tanga? Kwa nini tunaanza kuhesabu vifaranga il hali hata yai halijakomaa?
 
Hivi, hawa Wazenj wakija kuta kwamba chimbuko la hayo mafuta (ambayo kwa sasa ni mafuta hewa) ni Tanga, watachimba shimo hadi Tanga? Kwa nini tunaanza kuhesabu vifaranga il hali hata yai halijakomaa?

Mtegemea chandugu hufa maskini. mlipopewa shubiri mlichukuwa pima wameligunduwa hilo WAZANZIBAR

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=o0FiCxZKuv8]YouTube - Martin Luther King, Jr.'s last speech[/ame]
 
Halafu nyie mnaosema kuwa Bunge lina nguvu kuliko Wawakilishi wa Zanzibar naona mna matatizo ya kiuelewa maana chochote kinachopitishwa Bungeni Tanganyika ni lazima kikubalike ndani ya Baraza la wawakilishi ,hapo ndipo mliponasa maana hayo ya mafuta kusimamiwa na TPDC mnasema yalikubaliwa bungeni hayakupelekwa kwenye baraza la wawakilishi na mambo mengi ambayo yalipitishwa kwenye katiba hayakupata ridhaa kutoka Baraza la wawakilishi ,hayo Wazanzibari wanayahesabu kuwa ni mambo yaliopitishwa kinyemela kwa maana hayakufuata zile article za Muungano na makubaliano yaliomo kwenye Katiba ya leo hivyo wala hayakufuata taratibu zozote za kisheria mnajiamulia wenyewe kwa wenyewe,ni rahisi sana kuyafanya ajuari na ndipo huko wanakoelekea kila ambacho hakikupata ridhaa ya Baraza la Wawakilishi kitaondolewa sasa kaeni mkipanga hesabu ni mangapi hamkuyapeleka Baraza la Wawakilishi kupata baraka lazima mtafahamu kuwa popo ni mnyama na si ndege.
Kama ni kweli, hilo ni kosa kubwa la kikatiba la bara. Tatizo la sisi bara ni ubabe, jee unajua makabrasha yaliyotayarishwa na Wolfgang Dourado na kuridhiwa na Aboud Jumbe kuhusu haki ya Zanzibar akijitayarisha kuishitaki Tanzania UN yalisababisha nini?. Hali ya kisiasa ilichafuka na watu wakafungwa midomo.

Ubabe ndicho mkitakacho na punde si punde mtakipata na kujua kama maharage ni mboga au futari.
 
Pasco eh suala la kumaliza mpasuko ni gumu kidogo kwa sababu chanzo chake hasa kinachochewa na serikali ya muungano kwa kuwalazimisha wazanzibari lazima ccm ibaki madarakani japo wananchi hawataki, ukifika uchaguzi mamia ya askari na jeshi tutaletewa utafikiri zanzibar hakuna askari, yote hayo ni kuilinda ccm ibaki madarakani na kuulinda muungano huu wa kifisadi,lakini sasa tumejua janja yenu...mtatujua vijukuu vya mapinduzi
Kama ni kweli, ichagueni CUF, iyakane Mapinduzi matukufu, ivunje Muungano na hatimaye muanze kuchinjana!. Siye bara hatumo!.
 
Nimefurahi kusikia CCM na CUF wamekubaliana kwa asilimia 100% kwenye hili. Nasubiri kuona kama na mpasuko watauziba kwa asilimia 100% nani ya baraza hilohilo la wawakilishi. Vinginevyo ndiyo ile hadithi ya kujenga jumba la kifalme hewani.
Chonde chonde tuazime busara sasa..huu muungano una umuhimu mkubwa sana kwa zanzibar kuliko wanavyojidanganya

Nachowapendea viongozi wa Zanzibar ni jinsi wasivyo na ubinafsi wa kivyama na wanavyoweka maslahi ya ''taifa lao'' mbele - angalau kwa hili.
 
Back
Top Bottom