Binafsi nimeshajiuliza sana swala la Zanzibar. Ni kweli hawa ni ndugu zetu, pia ni kweli muungano wetu kama ulivyounganishwa na Nyerere na Karume unautata, vile vile ni kweli kuungana ni kitu kizuri katika kukuza uchumi na mahusiano baina ya zilizokuwa nchi mbili. Hatahivyo kumekuwa na maswali mengi ambayo hayajibiki na hao wanaosuruhisha maswala ya muungano.
Haikuniingia akilini nilivyosikia Zanzibar ilikuwa inatumia umeme toka Bara bila kulipa mpaka ilipoingia Net Group Solution ambapo waliambiwa walipe or else wanakatiwa umeme. hapo ndipo nilipochoka maana walipiga mkwala kuwa wakikatiwa umeme wanavunja muungano, ukweli ni kwamba serikari ya bara ililipa lile deni la Zanzibar na mambo yakawa shwari. Hata hivyo bado hawa jamaa wanalazimisha tuvunje muungano lakini CCM haitaki na imekula yamini kuulinda kwa nguvu zote.
Binafsi naungana na wazanzibar, inawezekana kabisa kukawa na ukweli kuwa sisi tunaitawala Zanjibar isivyo (wanyonyaji/wezi). Muungano ni kama urafiki wa aina yoyote ile. Huwezi lazimisha mtu fulani kuwa rafiki yako kama yeye hataki kuwa rafiki yako. Hataukimpa offer nyingi nyingi kama hana mapenzi na wewe itakuwa ngumu kuwa rafiki yako. Kinachoendelea Zanjibar na Bongo sasa hivi ni kama baba na mtoto. Zanzibar kila itakachotaka Bara itabidi tukikubari ili mulinda muungano. Kwanini haya mambo yasiwekwe hadharani au tukawakubalia wavunje muungano then tuungane upya kama tutakubaliana????????